Mkuu usajili wa wachezaji ni kamari, hakuna kitu kigumu sana kama usajili kukulipa. Huko ulaya kuna majopo ya watalaam wa scouting lakini nao wanafeli kwenye usajili. Labda usajili wa wachezaji kutoka Simba nitaungana na wewe kuwa kuna sajili za kukomoana ambazo zilikuwa hazina maana ila katika sajili hizo za kutoka Simba zisizo na maana muondoe Mkude. Mkude bado ana kitu cha kuisaidia Yanga kwenye eneo la kiungo. Angalia mechi zake anazocheza yeye anavyoipa balance timu ni tofauti na Mauya na Sure boy.