Lukuvi leo kadhihirisha kinaga ubaga kuwa Serikali inaendeshwa kimfumo kristo. Haya tuliyajadili sana kwenye nyuzi ya Mohamed Said, watu wakapinga sana na kutubeza sana Waislaam. Lakini leo Lukuvi kadhihirisha na kasema ana "hofu" na hiyo hofu (phobia) yake kwa Uislaam hakuna wa kumzuwia.
Kikwete, ndio waziri wako huyo, ana hofu na Uislaam, jee hana hofu na wewe?
Ninachokiona mimi ni kwamba 'chama' kina msimamo wake kwenye issue ya muundo wa serikali. Sasa wajumbe wa chama wanatumia kila mbinu ili kuunga mkono msimamo wa chama. Tumewasikia baadhi yao wakiwa ndani ya bunge hili hili wakitoa hoja za vitisho na maneno ya kejeli ili mradi ku-drive a point home. Sasa matokeo ya 'vijumbe' hawa ni kila mtu kutumia ushawishi wake kiasi kwamba ninaamini kama viboko vingeruhusiwa kuna watu wangechapwa viboko ili wakubaliane na muundo unaotakiwa na chama.
Sasa hapa tumekutana na waishiwa hoja ambao wameona sehemu dhaifu ya kwenda ni huko kanisani kutisha watu kupitia upande huo. Napata taabu kuamini kuwa aliyoyasema Lukuvi yanadhihirisha kuwa serikali ni mfumo kristo, sijui, ngoja niendelee kusoma katikati ya mistari labda nitaishia kwenye conclusion yako. Alichotumia Lukuvi ni kujenga watu hofu, nao wataenda kuwajenga wenzao wakifika nyumbani hivyo kuendeleza mlolongo mrefu wa watu wa dini hizi pendwa kuangaliana kichina china (utafikiri wanaliana timing!)
Hili ni moja, si bado wameendelea mbele kwa kusema jeshi litapindua nchi, sijui kodi za kichwa zitarudi (kumbuka hofu ya waliohadithiwa na babu zao adha ya kutokulipa kodi ya kichwa). Hayo yote si umeyasikia sis?
Na bado, tutasikia mengi kutoka kwa hao 'vijumbe' huku mtaani, tupe muda tu, tutafuatwa hadi nyumba kwa nyumba...