Lukuvi: Nina Hofu na Uislaam aka "Islamophobia".

Lukuvi: Nina Hofu na Uislaam aka "Islamophobia".

Status
Not open for further replies.
tatizo mleta mada ni mdini sana inamana hujui kuwa uamsho ndyo wanaochoma makanisa?na haohao ndyo wanaodai jamhuri ya zanzbr mbona hujawahi kuwalaani wanaochoma makanisa.tatizo hamtaki ukweli .mi binafsi nataka serekali 1

Ikiwa kuwa Muislaam ndio udini basi mimi ni mdini sana tu.

Jee, Lukuvi unamweka kundi lipi kwa hayo aliyokiri?
 
C.C.M Catholic Church Movement......Insha-Allah dada wache wapange na Mwenyezi Mungu anapanga...Na yeye ni mzuri wa Kupanga...Allah azidi kutufahamisha hili na jengine...Bado waislam wa Zanzibar tunafuraha ya kuwa pamoja na waislam walioko Bara...hakijaharibika kitu Dada....kama ukichunguza kwa mbaali Naona kheri haiko mbali inakuja...Allah akikupa siri ilioko nyoyoni mwa adui yako..hii ni moja hatua ya ushindi...
 
tatizo mleta mada ni mdini sana inamana hujui kuwa uamsho ndyo wanaochoma makanisa?na haohao ndyo wanaodai jamhuri ya zanzbr mbona hujawahi kuwalaani wanaochoma makanisa.tatizo hamtaki ukweli .mi binafsi nataka serekali 1

Ndugu yangu uwamsho ni waznz na makanisa yanayo chomwa moto ni ya waznz isitoshe hata huku kwetu Tanganyika nako yanachomwa moto na hata mbomu yanaripuliwa na uhalifu na mauwaji yanafanyika kila siku na si uwamsho wanaotekeleza hayo. Na ukumbuke muwamsho ni taasisi ya dini iliyo sajiliwa kama taasisi zingine...
Nataka nikuambie kiongozi wa aina ya Likuvi hakustahili kuongea aliyo ongea hasa kwenda kuongelea mustakabali wa nchi ktk kanisa na kujaribu kuwafarakanisha waTanzania kwa tofauti ya Uislam na ukiristo. Mm ni muislam na mwanachama wa ccm lakini leo hii ananifundisha nini kiongozi wangu ktk mustakabali wa imani ya dini yangu? Je ananilazimisha niamini wanayo sema waislam wenzangu kama nchii inaongozwa na mfumo kiristo? Nalazimika sasa kutafakari yanayo zungumzwa na wenzangu kuhusu mfumo kiristo nikiamini ccm nitaiyacha hapa Tz lakini uislam nitaendanao mpaka mwisho siku ya hukumu..
 
Nioneshe ni wapi niliitetea Serikali mbili? mimi sijali iwe moja, mbili au tatu.

Lakini leo hujamsikia lukuvi? ansema na hofu na Uislaam kuwa Zanzibar ikiwa na mamlaka kamili itakuwa Dola ya Kiislaam.

Tena kakiri kuwa maneno hayo kayasema kanisani na kakiri kuwa alitumwa na Waziri Mkuu.

Tunaposema, Tanzania tunaendeshwa na mfumo kristo , huwa mnabisha, haya bisheni sasa.

Unasemaje UHAMSHO kuyaita Mapinduzi ya Zanzibar kuwa ni Haramu, au hilo ujalisikia ila hili la Kanisa ndiyo limekuwasha makalio?
 
Unasemaje UHAMSHO kuyaita Mapinduzi ya Zanzibar kuwa ni Haramu, au hilo ujalisikia ila hili la Kanisa ndiyo limekuwasha makalio?

Wapi wamesema hivyo hebu tuekee ushahidi tafadhali!
Na kama huna ushahidi itakuwa umewazulia uongo Masheikh na utapata laana km iliyompata Mrema si unamuona alivyo!
 
Hebu fikiria endapo kauli kama hiyo ingetolewa na Lipumba, Tundu Lissu, Mbatia au wale wote wanaounga Rasimu ya katiba. Ingekuwaje?
Kungekuwa na thread nyingi za kuwahamasisha waombe radhi, halafu wajumbe kutoka Zanzibar kila ambae angesimama kuchangia lazima kila mmoja angekuwa analaani kwanza, hapo Ritz angekuwa na thread moja ndefu matata page zingekuwa zimepita kama 5 hivi, views wangekuwa kwenye 7600, hapo FaizaFoxy angewaka kama mara 2 hivi...
 
Last edited by a moderator:
Hilo ni swali zuri sana, nnauhakika tutapata majibu huu mjadala unapoendelea.

Kwa sasa swali lako zuri sipati jibu la haraka-haraka.

Nashukuru kwa jibu lako murua!! Maana wengine siye tumechoka na muundo wa Muungano huu na ndiyo maana haya ya Lukuvi labda ni mmoja ya maslahi mapana ya CCM kwenye muundo wa sirikali mbili. Maana unapoona mawaziri au viongozi wandamizi wanakuja na hofu kama hizo basi ujue kuna ghiriba nyingi ziko kuhusu Muungano huu na bado tutasikia mengi.
 
Kuna masuali mengi tu na wasiojuwa inabidi tuwaambie. Inaonekana wazi mh JK kalazimika kubadili msimamo katikati ya safari nadhani ni kwa hizi hofu za watu (Phobia) kama mtakumbuka suali la kadhi yule waziri Membe alipoitwa tu na muadham kardinali aligeuza msimamo kuhusu mahakama ya kadhi na JK naye alitoboa siri katika hutuba yake ya bunge kuwa kuna kiongozi wa dini mmoja ( anajulikana) alimpa ushauri wa serikali mbili na yeye kukubaliana naye kuwa bora tujaribu huo mtazamo wa mtu wa mungu. Jk kalazimika HAFLA KUBADILI MWELEKEO WA UMMA AMBAO ALISHAUJENGEA MATUMAINI KWA VITENDO VYAKE. kumbuka nani alimlazimisha kuleta mchakato kwani? kumbuka kauli zake za kuwataka watu wake wajiandae kisaikolojia, kumbuka jinsi alivyokwamua mchakato kila mawaziri wake walipopinga hatua za maridhiano? kumbuka kauli za kuhamasisha maridhiano na ile image yote ya kuipongeza tume ya WARIOBA leo ziko WAPI? hivi hamjajuwa tu? lazima kuna kitu na tayari picha imeanza kuonekana. Kwa mimi hata kama CCM wana maslahi yao kwa hili lakini na hili la upendeleo wa dini liko wazi.(Samahani kwa wale wakiristo) Haya ni mambo ya mjadala kwa sasa na kila kitu kina maana kipindi hiki. Tusidharau kitu. Hii kauli ya LUKUVI INATUCHONGANISHA SANA. Msitetee kwa ushabiki .Imeleta na kusadikisha kile ambacho siku nyingi kinasemwa huo ndio ukweli.

Mi naona Lukuvi ametumia ufisadi wake wa elimu kuleta honja mkorogano. Kwanza alienda kumwakilisha waziri mkuu katika hafla sijui ya kanisa gani???? Huko Dodoma, kisha akaanza siasa zake uchwara huko kanisani. Nilitarajia Waziri Mkuu kukemea tabia hiyo ya kutumia makanisa na misikiti kwa maslahi ya siasa. Katika hili ana udini, si tofauti na ule aliofanya Prof. Lipumba mwaka 2010 kama mkakati eti wa dini fulani lakini kumbe ni maslahi ya JK. Na hata sasa sijaelewa Lipumba anapolinganisha CCM na Interahamwe, maana nalo naona kama ni 'out of context' isipokuwa kama yeye anataka kutuambia kuwa anashabikia pia yale PK anayomfanyia JK na vitu vya namna hiyo, vinginevyo hakuna uhusiano wa Lukuvi (kanisani), na CCM katika serikali mbili....maana huko Rwanda makanisani sidhani kama ndiko walikouawa wengi kuliko mjini Kigali na vijijini....na bahati mbaya sana wote si viongozi wa dini na hata dini zenyewe ni washabiki tu kuliko waumini wa kweli. Kwao ni madaraka tu na si kingine. Mfumo kristo unaolalamikiwa ni kusema Lukuvi na Pinda ni viongozi wa dini wakati kule wengine si ajabu wana kibano sana juu ya wanavyofanya katika imani yao.
 
FaizaFoxy acha kupotosha umma wa Jf.tupo chonjo sana kufatilia juhudi zenu za kutaka ku- associate stutus quo ya kinacho endelea ktk BMK na udini.tatizo linajulikana lipo wapi;ni CCM ambayo wewe siku zote umekuwa ukiiunga mkono.usisahau kwamba hata W/lukuvi ni mwana ccm mwenzako.
huwa najiuliza,kama kauli hiyo ungetamkwa na mbowe au lissu hali ingekuwaje!.
 
Last edited by a moderator:
Kabla ya kutoka bungeni baadhi ya wabunge wa UKAWA jana, Professor Lipumba aliweka wazi aliyoyaongea kanisani waziri mmoja wa Serikali ya Muungano. Lipumba alisema kuna waziri kaenda kuhutubia kanisani kuwa "ikiwa Zanzibar itapewa mamlaka kamili basi mjuwe itaanzisha dola ya Kiislam".

Jana nikauliza ni waziri gani huyo? sikupata jibu humu JF.

Lakini kwa kuwa Mungu hamfichi mnafik, huyo waziri kajitokeza mwenyewe bungeni leo hii na kwanza kukiri kuwa katumwa na Waziri Mkuu na kusema kuwa hiyo ni hofu, "phobia" yake na akaendelea kusema "hakuna yeyote wa kunizuia hofu yangu hii".

Akazunguka wee na maneno lakini akashindwa kukisema kile alichokieleza Lipumba.

Kwa uchache, Lukuvi ameudhihirishia umma kuwa ana "Islamophobia" au hofu ya Uislaam.

Kiongozi unaefikia kutangaza Kanisani na Bungeni kuwa hutaki kuwapa mamlaka kamili Zanzibar kwa ajili ya dini yao, kweli hiyo si Serikali ya Mfumo Kristo tunayoilalamikia siku zote humu?

Na leo Lukuvi kahitimisha kwa kuniunga mkono yale ninayoyasema humu kila siku kuwa huu Muungano upo kwa ajili ya Kanisa. Na unaongozwa na Kanisa. Huwa mnajifanya hamnielewi lakini leo yamebainika bayana.

Wanaonisikitisha zaidi ni wale Wazanzibari waliobaki kuipigia makofi hoja hii ya Lukuvi, halafu wanajiita wao Waislaam. Waislaam mnaambiwa hampewi nchi yenu kwa kuwa Lukuvi ana hofu mkipewa mtaifanya dola ya Kiislaam na nyinyi mnashangilia? Yaani Lukuvi anawaambia kinaga ubaga kuwa mtabaki ndani ya mfuko Kristo mkitaka msitake na mkikataa basi ni bora nchi hii ishikwe na jeshi na akafikia mpaka kuwapa mfano wa Islamic Brotherhood ya Egypt.

Kinachonishangaza hii hofu yanini kwa Lukuvi? ikiwa nchi anayoiongelea ni Zanzibar na Wazanzibari 99% ni Waislaam ikiwa wataamuwa nchi yao kuwa ya Kiislaam yeye anapatwa na hofu ya nini?

cc Ritz, gombesugu kahtaan
Moderator tafadhali usiiunganishe hii na nyuzi nyingine hii maudhui yake inajitegemea.



Hakika huyu ndio waziri aliyepewa mamlaka ya kuwa uwaziri kupitia CCM.

Afadhali kama moja tu limekugusa hasa kwa kuwa wewe huwatetea sana wana CCM.
 
Last edited by a moderator:
Lukuvi akiwa mmoja wa wanamtandao anajua fika kwamba linapokuja suala la ubaguzi, Salim Ahmed Salim alibaguliwa na mtandao wakati wa mchakato wa urais ndani ya ccm (2005). Je hapa palikuwa na suala la serikali tatu? Tanganyika na CUF au Chadema? Hapana, kulikuwa na CCM, iliyoshinda baadae kwa zaidi ya 80%.

Salim alibaguliwa kwa lugha ya:
Hizbu, Mwarabu, Mpemba.

CC Mzee Mwanakijiji, Nguruvi3, Mag3, MwanaDiwani, Ritz, Pasco, FJM, Nape Nnauye, Tumaini Makene, Mwigulu Nchemba


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

watu ni wasahaulifu sana,maneno ya kibaguzi yalitumika kuwaondoa watu ktk kugombea urais na leo yanatumika kutetea aina ya muungano,hapo ndipo huwa nashindwa kuelewa aina ya siasa tuliyo nayo hapa Tanzania.
mungu atuepushie,mbali na haya yanayoendelea huko bungeni
 
Na nikuulize: kumzuia Salim asipite 2015 kwa hoja kwamba yeye ni hizbu, mwarabu, mpemba, je mtandao wa kina Lukuvi ulikuwa unaogopa serikali ya kidini?

Lukuvi - hata mimi nimemsikiliza na kumrekodi. Anachojaribu kufanya ni kuunganisha hoja ya Tanganyika na uislamu, hakuna kingine. Katika utafiti wake amegundua kwamba zanzibar imeshabaini kwamba bila ya Tanganyika, mamlaka kamili katika masuala nje ya muungano haiwezekani. Na hilo likitokea, CCM haitakuwa na uhalali mwingine wa kutawala. Nani ataipa kura au kusikiliza kampeni za wagombea urais wa Tanganyika, wakati waliikana? Nani ataipa kura urais wa muungano wa shirikisho wakati waliukana? Nani ataipa kura zanzibar wakati CCM ilikuwa inawanyima mamlaka kamili nje ya masuala ya muungano kwa kuikataa Tanganyika?

Lukuvi and company wameshaona shida iliyopo mbeleni. That's the bottom line.



Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
La msingi ni kwamba hata wewe unapinga serekali za udini.kuwa wazi
 
Lukuvi leo kadhihirisha kinaga ubaga kuwa Serikali inaendeshwa kimfumo kristo. Haya tuliyajadili sana kwenye nyuzi ya Mohamed Said, watu wakapinga sana na kutubeza sana Waislaam. Lakini leo Lukuvi kadhihirisha na kasema ana "hofu" na hiyo hofu (phobia) yake kwa Uislaam hakuna wa kumzuwia.

Kikwete, ndio waziri wako huyo, ana hofu na Uislaam, jee hana hofu na wewe?

Umeona eeh,"wasaka tonge" CCM-Znz wanachekelea huku wanabaguliwa waziwazi ili mradi wasinyang'anywe tonge mdomoni,ama kweli adui wa muislam ni CCM kwa mujibu wa Lukuvi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom