Lukuvi: Nina Hofu na Uislaam aka "Islamophobia".

Status
Not open for further replies.
Kwa hiyo unakiri kuwa Lukuvi kafanya vibaya au?

Hakuna anayepinga kwamba Lukuvi hajafanya vibaya ila wewe huo uzi wako umeuleta kiuchochezi, kitu kimefanywa na mtu mmoja wewe unaunganisha mambo ya Lukuvi na Ukristo. Mbona Viongozi wa Kiislamu wanavyoshinda Misikitini wakipanga mikakati mibaya dhidi ya Ukristo hamsemi?
 
Tatizo ni pale mtu Anafanya kazi kwa kulinda cheo ama kusifiwa na wakubwa wake na kuikuaka misingi ya utawala ndio maana unaona watu wa natumiwa kwa kuua watu wanaokuwa wako kinyume na viongozi kama vile mambomu ya arusha,iringa na kuteswa kwa baadhi ya watu haya sio kwamba kikwete anapanga bali kuna viogozi wasiopungua watatu wana latibu hayo kwa kutumia vibaya vyombo vya dora tume zinazoundwa kuchunguza haya zinashindwa kutoa ripoti kwa sababu wanaoguswa katika matukio hayo yote ni viogoz wa Serikali. Kama kikwete asipokuwa makuwa makini watu wataendelea kuuwawa na hakuna hatua yyt itakayo kukuliwa
 
Kama jei kei angewatumia
mkapa,warioba,butiku,sumaye.
Kidogo hadhi na heshima yake ingekuwa juu zaidi na taifa lingeimarika kiustawi.
Lakini kwa watu kama mwigulu,wassira,lukuvi aaah! Hovyo kabisa.
hapo mtu wa maana hapo ni warioba tu. wengine uliowataja hamna kitu. labda mkapa kwa mbaaaali.
 
Kawaida wajanja huchaguana, na wabovu hivyo hivyo.Hiyo inafuata law of attraction which states that LIkES ATTRACTS LIKES.
hiyo ni law ya wapi. unlike charge attract each other. wewe hiyo umeitoa mfukoni kwako?
 
na wewe una hofu na ukristo. unawezaje kusema hivyo wakati cream nzima ya uongozi TZ ni waislam???tuachane na mada zenye mwelekeo wa udini.
 
This will endless cost our president. Mbona wapo lukuki washauri wazuri, either watu wa usalama wameshindwa kumtaarifu Mh. Rais kuhusu wasifu wa watu wa kumshauri ama alikataa ushauri na kuchukua washkaji zake ili waneemeshe matumbo yao.
hiki kizungu hiki hatari sana.
 
Huu ulikuwa wakati mzuri sana wa kuyakarabati makosa yaliyofanywa huko nyuma katika historia yetu na kwa pamoja tungezika tofauti zetu na kupanga njia bora ya kufuata bila kulalamikiana,na hiyo imeishafanywa na tume. hizi tofauti tunazoziona ni za kibinafsi na woga wa mabadiliko ambao hauna msingi wowote ule.
 
hapo mtu wa maana hapo ni warioba tu. wengine uliowataja hamna kitu. labda mkapa kwa mbaaaali.

Pole sana kaka kwa kutojua ni Kwanini BEN MKAPA yuko kimya sana nakuomba sana usitafiti ukimya wa ben mkapa kama wewe ni mzarendo wa Tz .ila kama sio mzarendo na kuruhusu uendelee kutafiti (sirikali=serikali)
 
Kama jei kei angewatumia
mkapa,warioba,butiku,sumaye.
Kidogo hadhi na heshima yake ingekuwa juu zaidi na taifa lingeimarika kiustawi.
Lakini kwa watu kama mwigulu,wassira,lukuvi aaah! Hovyo kabisa.

Jamaa ana inferiority complex hawezi kuwatumia watu wenye akili zaidi yake!!!
 
Kwa hiyo unakiri kuwa Lukuvi kafanya vibaya au?
Wote Lukuvi na Lipumba ni mbumbu. Ila aliyeharibu zaidi ni huyu aliyemuita mwenzake na kundi lake intarahamwe halafu na kuonesha utoto wa kutoka.
 
Kiukweli Rais wetu Mh Kikwete ana kazi kubwa sana., hilo jopo lake la washauri ni watu wasio na BUSARA kabisa. Mfano hiyo Mh Lukuvi mtu Wa karibu Rais wetu hakutakiwa kujibu mapigo kwa njia ile, naona Kama alizidi kupandikiza chuki tu. Cha kushangazi Mh Sitta kamwachia tu aendeleze kupunda chuki. Pole sana Rais wangu Kikwete.
 
Naungana na FF, kuwa Lukuvi alichokifanya ni makosa makubwa na anastahili ajihuzulu mara moja!

Huwezi kuwa kiongozi wa wananchi wote halafu ukawabagua wananchi unao waongoza, tena kibaya zaidi ni kwa kuwabagua kwa misingi ya imani zao!

Pili, ameonyesha kuwa ni mchochezi mkubwa sana....huwezi kuongea kwa kukosoa imani hii mbele ya imani ile....yaani kama kiongozi hawezi kuwakosoa au kuwatenga waislamu mbele ya imani ya dini ingine ya kikristo! Angeenda Zanzbar au msikitini alafu akaseme alichosema....aone atajibiwaje!
 
Pole sana kaka kwa kutojua ni Kwanini BEN MKAPA yuko kimya sana nakuomba sana usitafiti ukimya wa ben mkapa kama wewe ni mzarendo wa Tz .ila kama sio mzarendo na kuruhusu uendelee kutafiti (sirikali=serikali)
eleza huo ukimya wa ben acha kuzunguka mbuyu. "jf, where we dare to talk openly''
 
Wakuu,baada ya kumwangalia Lukuvi akitutisha sisi wananchi wenzake juzi pale bungeni,iko kama vile watawala wame panick,kuna kitu gani wanachoogopa kwenye S3(serikali tatu) ambacho wanashindwa kutueleza sisi ndugu zao?Maana kwa akili za kawaida,ikiwa utashi wa kisiasa utakuwepo,kwa pamoia ndio tunao wajibu wa kutafuta njia ya kuhakikisha kuwa kunakuwa na vyanzo vya mapato vitakavyotosheleza mahitaj(ikiwamo hitaji la kuendesha majeshi)ya serikali ya Shirikisho!Hivyo swala la hizo S3 kushindwa kuligharania jeshi halitakuwepo tena.Hata hivyo,mwisho wa siku:Tanganyika itazaliwa kwa nguvu za wapigania uhuru wa Zanzibar,hata vijana na wazee wa Tanganyika wakionyesha uchovu wa namna gani!
 
Narudia tena kukujuza hapa nilipo bold hao Boko Haram na AL-Qaida hawawakilishi Waislam katika harakati zao hizo wanapigania maslahi yao ya kidunia, ebu pata darsa kiduchu kuhusu Uislam.

Na hapa chini msome kiongozi wako wa dini ambae ni shoga.

Tarejea barzani....
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…