Kabla ya kutoka bungeni baadhi ya wabunge wa UKAWA jana, Professor Lipumba aliweka wazi aliyoyaongea kanisani waziri mmoja wa Serikali ya Muungano. Lipumba alisema kuna waziri kaenda kuhutubia kanisani kuwa "ikiwa Zanzibar itapewa mamlaka kamili basi mjuwe itaanzisha dola ya Kiislam".
Jana nikauliza ni waziri gani huyo? sikupata jibu humu JF.
Lakini kwa kuwa Mungu hamfichi mnafik, huyo waziri kajitokeza mwenyewe bungeni leo hii na kwanza kukiri kuwa katumwa na Waziri Mkuu na kusema kuwa hiyo ni hofu, "phobia" yake na akaendelea kusema "hakuna yeyote wa kunizuia hofu yangu hii".
Akazunguka wee na maneno lakini akashindwa kukisema kile alichokieleza Lipumba.
Kwa uchache, Lukuvi ameudhihirishia umma kuwa ana "Islamophobia" au hofu ya Uislaam.
Kiongozi unaefikia kutangaza Kanisani na Bungeni kuwa hutaki kuwapa mamlaka kamili Zanzibar kwa ajili ya dini yao, kweli hiyo si Serikali ya Mfumo Kristo tunayoilalamikia siku zote humu?
Na leo Lukuvi kahitimisha kwa kuniunga mkono yale ninayoyasema humu kila siku kuwa huu Muungano upo kwa ajili ya Kanisa. Na unaongozwa na Kanisa. Huwa mnajifanya hamnielewi lakini leo yamebainika bayana.
Wanaonisikitisha zaidi ni wale Wazanzibari waliobaki kuipigia makofi hoja hii ya Lukuvi, halafu wanajiita wao Waislaam. Waislaam mnaambiwa hampewi nchi yenu kwa kuwa Lukuvi ana hofu mkipewa mtaifanya dola ya Kiislaam na nyinyi mnashangilia? Yaani Lukuvi anawaambia kinaga ubaga kuwa mtabaki ndani ya mfuko Kristo mkitaka msitake na mkikataa basi ni bora nchi hii ishikwe na jeshi na akafikia mpaka kuwapa mfano wa Islamic Brotherhood ya Egypt.
Kinachonishangaza hii hofu yanini kwa Lukuvi? ikiwa nchi anayoiongelea ni Zanzibar na Wazanzibari 99% ni Waislaam ikiwa wataamuwa nchi yao kuwa ya Kiislaam yeye anapatwa na hofu ya nini?
cc
Ritz,
gombesugu kahtaan
Moderator tafadhali usiiunganishe hii na nyuzi nyingine hii maudhui yake inajitegemea.
FaizaFoxy,
Mara tu lilipodhihiri tatizo la serikali mbili au tatu niliweka mada kadhaa katika
website yangu na katika nyingine mbili nikisema kuwa hapatawezekana kamwe
mtu yeyote kuweza kufanya tafakuri ya maana na kuweza kuchangia katika
mada hiyo bila ya kujua historia ya kweli ya mapinduzi ya Zanzibar.
Ukishajua historia ya kweli ya mapinduzi ya Zanzibar hapo mtu anaweza kuwa
katika hali ya siyo tu kuchangia bali hata kujua kwa nini kwanza, hii leo historia
ya mapinduzi imetiwa mkono na kubadilishwa.
Pili atajua kwa nini hao mashujaa khasa wa mapinduzi yenyewe hawatajwi; na
tatu kutokakana na kujua hayo mawili yalotajwa ataelewa kwa nini Zanzibar leo
haitakiwi kuwa huru.
Katika sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya mapinduzi zimetolewa medali kadhaa
kwa wale mashujaa wa mapinduzi.
Ikiwa unaijua historia ya kweli ya mapinduzi utashangazwa kwa kukosekaaa majina
ya wapangaji wa mapinduzi.
Na hakika kuna wengi wameshangaa mbona kinara wa mapinduzi
Abdallah Kassim
Hanga hakuenziwa?
Hanga kafutwa katika historia ya Zanzibar.
Ukimsikia
Hanga anatajwa basi atatajwa na wale ambao wameumizwa jinsi
alivyouliwa kishenzi mwaka 1967 au 1968 hakuna mwenye uhakika ni lini aliuliwa.
Mbona
Oscar Kambona hakuenziwa?
Mbona
Victor Mkello hakuenziwa?
Mbona
Aboud Mmasai hakuenziwa?
Mbona
Mohamed Omar Mkwawa hakuenziwa?
Vipi kuhusu
John Okello?
Vipi
Mwalimu Nyerere aliyetoa msaada mkubwa kutoka Tangayika, msaada wa
fedha na ''logistics'' hatajwi popote wala hakuenziwa?
Wako wengi waliostahili medali hawakupewa medali.
Hebu tuanze na kujiuliza kwa nini mambo yako hivi?
Hapa kinafichwa kitu gani?
Kwa wenye kujua historia ya kweli ya Zanzibar na kwa nini serikali ya
Sheikh
Mohammed Shamte ilipinduliwa hawashangai kusikia
William Lukuvi kenda
kanisani kusema aliyosema kuwa kuna hofu Zanzibar itaimarisha Uislam ikiwa
itaachiwa kuwa huru.
Kwa sasa nitaishia hapa niwaache wana jamvi wahangaishe akili na fikra zao.
Lakini ningependa
Willia m Lukuvi ajifunze kidogo historia ya Waislam na Uislam
katika kupigania uhuru wa nchi hii Tanganyika.
Nimeweka picha ya
Mzee Mkwawa alivyo sasa picha hii nimempiga mimi mwaka
2012 nyumbani kwake Sahare Tanga.
Mzee Mkwawa ndiye aliyekuwa akiwavusha mamluki kutoka mashamba ya mkonge
Sakura na Kipumbwi kwenda Zanzibar kuipigia kura ASP mwaka 1961 na kupindua
serikali mwaka 1964.
Ningependa pia
William Lukuvi ajifunze historia ya Nyerere atakuwa mwerevu.
Nimeweka picha nikiwa studio za Radio Al Noor Zanzibar nikifanya kipindi ''mubashara''
kuhusu historia ya Zanzibar.
Kuna picha
Mzee Hassan Nassor Moyo akisoma kitabu, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri
Uhuru'' nyumbani kwake Fuoni na nyingine nikizungumza na
Salim Rashid Katibu wa Baraza
la Mapinduzi Zanzibar, 1964.
Ipo picha niko na
Mzee Aboud Jumbe.
Kuna picha ya Waislam waliokuwa na
Nyerere bega kwa bega wakati wa kuikomboa
Tanganyika katika miaka ya 1950.
Wakati huo maaskofu walikuwa wakiwakataza wafuasi wao wasijiunge na TANU.