Lukuvi: Nina Hofu na Uislaam aka "Islamophobia".

Lukuvi: Nina Hofu na Uislaam aka "Islamophobia".

Status
Not open for further replies.
Lukuvi leo kadhihirisha kinaga ubaga kuwa Serikali inaendeshwa kimfumo kristo. Haya tuliyajadili sana kwenye nyuzi ya Mohamed Said, watu wakapinga sana na kutubeza sana Waislaam. Lakini leo Lukuvi kadhihirisha na kasema ana "hofu" na hiyo hofu (phobia) yake kwa Uislaam hakuna wa kumzuwia.

Kikwete, ndio waziri wako huyo, ana hofu na Uislaam, jee hana hofu na wewe?

Hoja ya serikali 2 hawa ccm wameidandia kwa Pengo.
 
Last edited by a moderator:
Lukuvi alikuwa ana lengo la kutisha na kuchonganisha ili matakwa yao yaweze kutimia ndio maana aliongelea kanisani ili aonekane yupo pamoja na wakristo katika kufanikisha matakwa yao, we si unaona Askofu aliyesimikwa alivyokuja ku bold maneno ya Lukuvi ili record ikae sawa, sasa wewe unataka angeongelea bungeni malengo yangetimiaje!?

Akisha chonganisha waislam na wakiristo wakaripuka hayo matwaka yake ndio yatakuwa yametimia watu wakiingia mitaani na kupigana yeye anajiamini nini watamlinda au atakimbia nchi je familia yake italindwa au nayo itakimbia nchi? Shangzi yake,mjomba, mama mdogo mkubwa ,baba mdogo mkubwa nk wote hao atawapeleka wp na familia zao? Sioni kama ametamka na alipo tamkia maneno yake kama ni sahihi na sioni kama anayo nafasi yakujitakasa.nashawishika kuwaambia wsislam na hata wasio kuwa waislam ambao wanaitakia mema nchi hii watakao kuwa ktk jimbo ambalo huyu Lukuvi atagombea wasimpe kura achilia mbali ccm tukose jimbo hilo.Hatuwezi kuwa na viongozi wanao tugombanisha.
 
Kwa uchache, Lukuvi ameudhihirishia umma kuwa ana "Islamophobia" au hofu ya Uislaam.

Na leo Lukuvi kahitimisha kwa kuniunga mkono yale ninayoyasema humu kila siku kuwa huu Muungano upo kwa ajili ya Kanisa. Na unaongozwa na Kanisa. Huwa mnajifanya hamnielewi lakini leo yamebainika bayana.

Wanaonisikitisha zaidi ni wale Wazanzibari waliobaki kuipigia makofi hoja hii ya Lukuvi, halafu wanajiita wao Waislaam. Waislaam mnaambiwa hampewi nchi yenu kwa kuwa Lukuvi ana hofu mkipewa mtaifanya dola ya Kiislaam na nyinyi mnashangilia? Yaani Lukuvi anawaambia kinaga ubaga kuwa mtabaki ndani ya mfuko Kristo mkitaka msitake na mkikataa basi ni bora nchi hii ishikwe na jeshi na akafikia mpaka kuwapa mfano wa Islamic Brotherhood ya Egypt.

Ndugu yangu hao Wakristo unawapakazia bure, Kiini cha CCM kung'ang'ania Serikali mbili ni kujiwekea Kinga baad ya kuiba na kupora Raslimali za Wanyonge na zingine kuhamishia ughaibuni....
Nimefurahia kwamba sasa ndo ule wakati muafaka wa wananchi kuchukua hatua kamili ya kujikomboa toka mikononi kwa mkoloni dhalimu CCM.

Ingawa huwa sikubaliani nawe katika mengi, ninaanza kuona kwamba umeanza kupata uelewa baada ya kuguswa suala la Imani ya Dini ya Mwenyezi Mungu. Lakini tunapowambia CCM ni Janga la Taifa kwenye tasnia ya Kijamii, Kiuchumu, Kisiasa na Kimazingira nk...

Tatizo sio CCM maana ata Warioba ni CCM tatizo KITIMBAKWIRA ndani ya CCM
 
Tatizo Watanzania wengi ni wanafiki, leo ndio mnajifanya kushituka na kauli Za Lukuvi na ccm yake. Mbona vyama vya siasa wakati vinalalamika kuhusu kupakaziwa udini na ccm mlishangilia na kuunga mkono hoja za udini.

Leo yamewageuka mnajifanya mnashituka, watanzania lazima tukubali adui yetu ni mmoja tu nae ni ccm na kila mtu ataguswa kwa namna yake.

Ccm wapo kimaslai Zaid hawana rafiki wa kudumu ila maslai ya kudumu.

Hawa jamaa wa ccm wanapigania tonge kupokonywa.
 
Kabla ya kutoka bungeni baadhi ya wabunge wa UKAWA jana, Professor Lipumba aliweka wazi aliyoyaongea kanisani waziri mmoja wa Serikali ya Muungano. Lipumba alisema kuna waziri kaenda kuhutubia kanisani kuwa "ikiwa Zanzibar itapewa mamlaka kamili basi mjuwe itaanzisha dola ya Kiislam".

Jana nikauliza ni waziri gani huyo? sikupata jibu humu JF.

Lakini kwa kuwa Mungu hamfichi mnafik, huyo waziri kajitokeza mwenyewe bungeni leo hii na kwanza kukiri kuwa katumwa na Waziri Mkuu na kusema kuwa hiyo ni hofu, "phobia" yake na akaendelea kusema "hakuna yeyote wa kunizuia hofu yangu hii".

Akazunguka wee na maneno lakini akashindwa kukisema kile alichokieleza Lipumba.

Kwa uchache, Lukuvi ameudhihirishia umma kuwa ana "Islamophobia" au hofu ya Uislaam.

Kiongozi unaefikia kutangaza Kanisani na Bungeni kuwa hutaki kuwapa mamlaka kamili Zanzibar kwa ajili ya dini yao, kweli hiyo si Serikali ya Mfumo Kristo tunayoilalamikia siku zote humu?

Na leo Lukuvi kahitimisha kwa kuniunga mkono yale ninayoyasema humu kila siku kuwa huu Muungano upo kwa ajili ya Kanisa. Na unaongozwa na Kanisa. Huwa mnajifanya hamnielewi lakini leo yamebainika bayana.

Wanaonisikitisha zaidi ni wale Wazanzibari waliobaki kuipigia makofi hoja hii ya Lukuvi, halafu wanajiita wao Waislaam. Waislaam mnaambiwa hampewi nchi yenu kwa kuwa Lukuvi ana hofu mkipewa mtaifanya dola ya Kiislaam na nyinyi mnashangilia? Yaani Lukuvi anawaambia kinaga ubaga kuwa mtabaki ndani ya mfuko Kristo mkitaka msitake na mkikataa basi ni bora nchi hii ishikwe na jeshi na akafikia mpaka kuwapa mfano wa Islamic Brotherhood ya Egypt.

Kinachonishangaza hii hofu yanini kwa Lukuvi? ikiwa nchi anayoiongelea ni Zanzibar na Wazanzibari 99% ni Waislaam ikiwa
wataamuwa nchi yao kuwa ya Kiislaam yeye anapatwa na hofu ya nini?

[video=youtube_share;PIAPAAd3Dck]http://youtu.be/PIAPAAd3Dck[/video]

cc Ritz, gombesugu, kahtaan, THE BIG SHOW, CHAMVIGA
Moderator tafadhali usiiunganishe hii na nyuzi nyingine hii maudhui yake inajitegemea.

Hivi Lukuvi ni wa chama gani na ameteuliwa na nani na kwa kauli yake alikuwa anamwakilisha nani. Aliyemteua Lukuvi kwake yeye ameonesha msimamo gani katika suala la kuandaa Katiba Mpya kama sio unafiki na kuhubiri dhihaka kwa Mhe Jaji Warioba kana kwamba Mzee Warioba alijiteua mwenyewe kuongoza ile tume.

Kwa sasa kimenuka na walioharibu wanajaribu kutafuta pa kutokea ili waonekane kuwa sio wahusika lakini kimsingi akina Lukuvi na wengineo wamecheza ngoma aliyoianzisha Kikwete mwenyewe na katika hilo wa kulaumiwa ni huyo aliyeanzisha ngoma na sio wachezaji na waghani mashairi.
 
yanishangaza eti mtu keshakiri kuwa anahofu nanyi na hasa dini yenu na tena kwakurudia hakuna mtu wa kumfanya chochote...bado mnapiga makofi na kushangilia...
bora unyimwe vyote lakini sio ufahamu....
 
Hapana sio mimi mkuu uliposikia wamekudanganya bwana Izz ila ni mteule wa Rais bwana Lukuvi, na ni mnadhimu wa serikali bungeni inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa Ndugu Jakaya Mrisho Khalfan Kikwete na makamo wake Dr Gharib Bilal, Lukuvi inawezekana akawa amepata maelekezo kutoka huko...

Angalia sasa mnavoumbuka mchana kweupe!

Wewe unaemuandikia huo UHARO huyo Lukuvi wako hamtoki, japo mshaanza kutafuta pakutokea kwa kuanza kutaja majina ya watu hovyo!

Kesho atakua kigango cha wapi katika huo muendelezo wenu wa KANISA?
 
Lukuvi leo kadhihirisha kinaga ubaga kuwa Serikali inaendeshwa kimfumo kristo. Haya tuliyajadili sana kwenye nyuzi ya Mohamed Said, watu wakapinga sana na kutubeza sana Waislaam. Lakini leo Lukuvi kadhihirisha na kasema ana "hofu" na hiyo hofu (phobia) yake kwa Uislaam hakuna wa kumzuwia.

Kikwete, ndio waziri wako huyo, ana hofu na Uislaam, jee hana hofu na wewe?

Ninakubaliana na wewe lakini sio kwa yote. Lukuvi hana mamlaka na staha ya kunisemea mimi na wale wote wanaoishi katika Ukristo. Yeye ni kiongozi wa CCM anayetamani madaraka bila ya kujali kingine, na anatugombanisha na wenzetu bila sababu yeyote. Sasa angalia hata zile hisia zinakuwa zimehidhirishwa na mpuuzi kama huyu. Mbona tumeishi wote siku zote kwa shida na raha. Huyu anatoka wapi.

Ningefurahi zaidi tukaliangalia hili kama la Lukuvi na walafi wenzie humo ndani ya CCM. Amini usiamini hata wale wa namna yake yaani wenye kutamani madaraka na ambao imani yao iko ndani ya uislamu wanaweza wakasema na kufanya kama alivyofanya huyu! Madaraka hulewesha! Huwafanya wakawa na vichwa visivyokuwa na muda wa kufikiri kabla ya kutamka!

Nakutakia Pasaka njema Faiza!
 
FaizaFoxy, Ritz CHAMVIGA
===>Tumshukuru sana Lukuvi,mara nyingine Mungu huwaumbua watu fulani kwa ajili ya kuwaonyesha watu wake wapi wanakosea
===>Mungu nimwema sana,Hongera sana Mh Lukuvi Umewaaambia watanzania yale mnayoyafanya mkiwa kwenye vikao vyenu vya siri
===>Hata Mggombea wa Urais Mitt Romney alishindwa hivi hivi baada ya kutamka maneno kama haya ya kibaguzi
===>Ashukuriwe sana Mungu.
 
Last edited by a moderator:
Mzee wetu Mohamed Said,

Huu mpini uloweka hapa ni hatari, kuna vilaza hapa watapata tabu sana kufahamu haya mambo!

Ukipata fursa japo kiduchu, tunakuomba uje upige msasa vichwa vyao, kwani itafika mahala watafahamu tu, maana wameenza "kuyaabula" wenyewe kwa wenyewe sasa!

Ahsanta

Izz,
Kwa hakika inapokuwa mtu kafungwa akili ataweza kupata tabu sana kuelewa
mchezo uliochezwa katika miaka 50 ya muungano.

Zanzibar wenyewe weshajua.
Ndiyo maana dini sasa inachukua nafasi yake katika siasa za visiwani.

Hapa kwetu nje ya wanasiasa Waislam ambao kwao Allah hana nafasi baadhi
wameanza kuelewa.

Ushahidi kuwa mambo yanabadilika ni huu hapa JF.
Soma Waislam wanasema nini humu.
 
Kabla ya kutoka bungeni baadhi ya wabunge wa UKAWA jana, Professor Lipumba aliweka wazi aliyoyaongea kanisani waziri mmoja wa Serikali ya Muungano. Lipumba alisema kuna waziri kaenda kuhutubia kanisani kuwa "ikiwa Zanzibar itapewa mamlaka kamili basi mjuwe itaanzisha dola ya Kiislam".

Jana nikauliza ni waziri gani huyo? sikupata jibu humu JF.

Lakini kwa kuwa Mungu hamfichi mnafik, huyo waziri kajitokeza mwenyewe bungeni leo hii na kwanza kukiri kuwa katumwa na Waziri Mkuu na kusema kuwa hiyo ni hofu, "phobia" yake na akaendelea kusema "hakuna yeyote wa kunizuia hofu yangu hii".

Akazunguka wee na maneno lakini akashindwa kukisema kile alichokieleza Lipumba.

Kwa uchache, Lukuvi ameudhihirishia umma kuwa ana "Islamophobia" au hofu ya Uislaam.

Kiongozi unaefikia kutangaza Kanisani na Bungeni kuwa hutaki kuwapa mamlaka kamili Zanzibar kwa ajili ya dini yao, kweli hiyo si Serikali ya Mfumo Kristo tunayoilalamikia siku zote humu?

Na leo Lukuvi kahitimisha kwa kuniunga mkono yale ninayoyasema humu kila siku kuwa huu Muungano upo kwa ajili ya Kanisa. Na unaongozwa na Kanisa. Huwa mnajifanya hamnielewi lakini leo yamebainika bayana.

Wanaonisikitisha zaidi ni wale Wazanzibari waliobaki kuipigia makofi hoja hii ya Lukuvi, halafu wanajiita wao Waislaam. Waislaam mnaambiwa hampewi nchi yenu kwa kuwa Lukuvi ana hofu mkipewa mtaifanya dola ya Kiislaam na nyinyi mnashangilia? Yaani Lukuvi anawaambia kinaga ubaga kuwa mtabaki ndani ya mfuko Kristo mkitaka msitake na mkikataa basi ni bora nchi hii ishikwe na jeshi na akafikia mpaka kuwapa mfano wa Islamic Brotherhood ya Egypt.

Kinachonishangaza hii hofu yanini kwa Lukuvi? ikiwa nchi anayoiongelea ni Zanzibar na Wazanzibari 99% ni Waislaam ikiwa
wataamuwa nchi yao kuwa ya Kiislaam yeye anapatwa na hofu ya nini?

[video=youtube_share;PIAPAAd3Dck]http://youtu.be/PIAPAAd3Dck[/video]

cc Ritz, gombesugu, kahtaan, THE BIG SHOW, CHAMVIGA
Moderator tafadhali usiiunganishe hii na nyuzi nyingine hii maudhui yake inajitegemea.

Hivi wapinga ngoma walipokuwa wakiimba cuf ni wadini si mlikata mauno yenu mkifurahia? Mlipoambiwa kuwa cdm ni wadini si mli nyanyua viwiliwili vyenu na kuicheza ngoma!? Leo unalia nini wakati mliambiwa adui yenu ni ccm mkamwacha na kupapambana na rafiki zenu!
Pole sana dada! Umechelewa sana kutambua ukweli!! Hata hivyo bado una nafasi ya kurekebisha mambo! Hamia upande wa kweli na haki, Mungu atakuwa upande wako!
 
Last edited by a moderator:
Ikiwa kuwa Muislaam ndio udini basi mimi ni mdini sana tu.

Jee, Lukuvi unamweka kundi lipi kwa hayo aliyokiri?

Kichaa,uroho na uoga wa kukosa madaraka. Yuko tayari kutumia mbinu yeyote kutetea ulaji wake.Yule mwizi tu
 
FaizaFoxy,
Tatizo ulilonalo ni you don't live in reality. Lukuvi alichosema ni kweli kwani tumeshaona dalili zote za islamic radicalization huko zenj. Hao waislam wanaomshangilia Lukuvi wanakula bata katika serikali ya CCM na lazima watetee kitumbua chao. Pia japo wewe na wenzako kina khartan hua mnajidanganya waislam wote ni ndungu. Ukweli ni japo zanzibar ni 99% waislam nitakuakikishia kuna wengi wanao ogopa zanzibar kuwa nchi ya kiislam kwasababu za uarabu vs ubantu ambazo umeziona hata apo bungeni. Mimi mtanganyika naombea tu muungano uvunjike mukatane mapanga kwasababu mnastahili kwa usababu ya ubaguzi wenu wa sisi wazanzibar huku mukimaanisha hamuwapendi wakristo.
 
Angalia sasa mnavoumbuka mchana kweupe!

Wewe unaemuandikia huo UHARO huyo Lukuvi wako hamtoki, japo mshaanza kutafuta pakutokea kwa kuanza kutaja majina ya watu hovyo!

Kesho atakua kigango cha wapi katika huo muendelezo wenu wa KANISA?
kwani mkuu Izz we upo eneo gani nikupe ratiba kulingana na eneo lako uweze kuhudhuria akija bwana Lukuvi? inaonekana bayana zake zimekukuna sana vilivyo...
 
Last edited by a moderator:
Lukuvi siku zote huwa anakera. Kwa hapa naamini kazidi. Anajilinganisha na mkuu wa nchi
 
Mara vitisho vya machafuko, ooh vita...mara jeshi sijui litachukua nchi....ooh islamphobia...kama ccm mmechoka kutawala kuweni wazi sio kutapatapa na kauli zenye utata daily!
 
Tatizo kubwa Tanzania uwa hakuna Mkirsto mdini lakini kutokana na kauli ya Lukuvi kuwafurahisha wakirsto wenzake hakuna tatizo.

Huu muungano upo chini ya Kanisa, angalia kauli za Mrema na Lukuvi.

Wazanzibar pambaneni muikomboe nchi yenu kutoka kwenye mikono ya Kanisa.

Udini unawatesa sana , naona hapo umeona aibu kuandika wajikomboe kutoka kwenye mikono ya ccm. Roho inakuuma kutumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja huku maslahi yanagongana.
 
Mkuu Ritz,

Huyo dogo kadoda11 mpini umemuingia!

hamna kitu hapo.wana CCM mnajaribu kuuzunguka mbuyu ilhali tatizo linajulilana.chanzo cha haya yote ni chama chenu.mmefikia hatua ya kutaka kuchonganisha wananchi na dini zao,ili waingiwe na hofu ya uwepo serikali 3.
 
Last edited by a moderator:
Lakini ieleweke kuwa viongozi wa dini ndio wasababishaji wakubwa wa mauaji ya kimbari na halaiki hasa katika bara la Afrika. Hii inachochewa na ukosefu wa uzalendo na hofu ya Mungu kwa hawa viongozi wa dini kushikamana na watawala dhidi ya matakwa ya wananchi walio wengi. Kuna mifano mingi ya dola zilizoshikamana na viongozi wa dini dhidi ya matakwa ya raia mfano Rwanda/burundi, Sudan, A. Ya kati nk.
Nimetoa maoni haya baada ya kumsikia yule mjumbe wa bunge maalumu askofu mstaafu akilaumu upande mmoja wa wabunge wenye msimamo wa s.3 kuwaita wabunge wenye msimamo wa s.2 kuwa ni INTARAHAMWE. Kilichompotezea uhalali wa uwakala wa usuluhishi huyu askofu na kubakia mshabiki mtetea upande mmoja ni pale aliposhindwa kuona matusi yaliyokuwa yanatolewa na wale wa serikali 2 dhidi ya 3. Wasira kawaita wajumbe MASHETANI. Hili siyo tatizo kwa huyu askofu ila lile lililotoka kwa wenye msimamo tofauti na yeye.
Nasema hivi mjjumbe hakukosea kuwaita hawa maaskofu wa namna ya Mtetemela INTARAHAMWE.
Hawa ndio namna ya viongozi wa dini wanaosababisha mauaji ya halaiki.
Waumini tunawaapuuza na hasa tunapoona wakishindwa kuwa wapatanishi kwa kutokuwa na upande, badala yake ni wakereketwa wa itikadi za chama cha siasa.
Hata huko mbeleni kukitokea machafuko kwa sababu ya kauli za hawa mafarisayo(Intarahamwe) tutashirikiana kuhakikisha kwamba wanaburuzwa kwenye mahakama za kisheria kwa uchochezi wa mauaji ili na wao watengwe na walio hai.
Absolutely: tatizo sii dini kwa maana ya uisilamu au Ukristo hapana! Tatizo ni mawakala wa vyama vya siasa waliojificha ndani ya dini kama viongozi wa dini kumbe kazi yao kubwa ni kufanikisha uharamia wa watawala ndani ya hizi dini.
.

.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom