aminiusiamini
JF-Expert Member
- Aug 25, 2011
- 3,577
- 2,224
Kuna nchi na serikali nyingi tu duniani ambazo zina hofu na watu wenye msimamo mkali wa kidini; iwe Waislamu au watu wa dini nyingine. Zipo nchi za Kiislamu ambazo zina hofu na Waislamu wenye msimamo mkali, Saudia, UAE, Misri n.k ni mifano tu. Kwamba mtu ameonesha hofu hii kuhusiana na Zanzibar si suala la kushangaza kwani wapo pia wananchi wa Zanzibar ambao nao yumkini wana hofu hiyo hiyo. Huwezi kuita hii ni "phobia' isipokuwa hujui maana ya 'phobia' ni nini.
Unajua kaka,uhuru wa habari ni jambo jema sana. Lakin pale unapotumiwa kutoa na kupandikiza maneno kama hv ni hatari mno.
Ni juzi tu nilikuwa nawaza mambo haya. Nikakumbuka Rwanda,jinsi Kagame anabyothibiti habari na juzi Kenya wamepitisha bill inayozuia baathi ya habari kusambazwa.
Unajua nimekuka kuona huu uhuru ndio break through ya maadui wa ndani na nje ya nchi. Serikali za kigeni zinatumia watu kupropagate agenda fulani fulani. Na hii tukifumbia macho itakuwa sio. Watu wanasema marekani kuna uhuru wa habari nani amesema?? Ulishawahi kujiuliza??
Lakni tukija africa wanapiga mayowe kwanini hakuna uhuru. Sababu hizi hizi za mashetani kama huyu dada. Am very disappointed with her. Watu kama hawa there is no mercy.
The king.