Lukuvi: Nina Hofu na Uislaam aka "Islamophobia".

Lukuvi: Nina Hofu na Uislaam aka "Islamophobia".

Status
Not open for further replies.
Kuna nchi na serikali nyingi tu duniani ambazo zina hofu na watu wenye msimamo mkali wa kidini; iwe Waislamu au watu wa dini nyingine. Zipo nchi za Kiislamu ambazo zina hofu na Waislamu wenye msimamo mkali, Saudia, UAE, Misri n.k ni mifano tu. Kwamba mtu ameonesha hofu hii kuhusiana na Zanzibar si suala la kushangaza kwani wapo pia wananchi wa Zanzibar ambao nao yumkini wana hofu hiyo hiyo. Huwezi kuita hii ni "phobia' isipokuwa hujui maana ya 'phobia' ni nini.

Unajua kaka,uhuru wa habari ni jambo jema sana. Lakin pale unapotumiwa kutoa na kupandikiza maneno kama hv ni hatari mno.

Ni juzi tu nilikuwa nawaza mambo haya. Nikakumbuka Rwanda,jinsi Kagame anabyothibiti habari na juzi Kenya wamepitisha bill inayozuia baathi ya habari kusambazwa.

Unajua nimekuka kuona huu uhuru ndio break through ya maadui wa ndani na nje ya nchi. Serikali za kigeni zinatumia watu kupropagate agenda fulani fulani. Na hii tukifumbia macho itakuwa sio. Watu wanasema marekani kuna uhuru wa habari nani amesema?? Ulishawahi kujiuliza??
Lakni tukija africa wanapiga mayowe kwanini hakuna uhuru. Sababu hizi hizi za mashetani kama huyu dada. Am very disappointed with her. Watu kama hawa there is no mercy.

The king.
 
kusema ukweli kabisa... Lipumba ameongea vizuri sana

It is too much kwakweli
 
Lipumba yuko sahihi kabisa! Kila wakati mwanasiasa bora lazima atafute kinga toka kwa wananchi wake.
Nauliza, Lukuvi alikwenda kumwakilisha w.mkuu, ni serikali ni ccm kwa nini unapindisha kuikoa ccm na kuzamisha ukristo? Usitegemee mema kutoka ccm. Hawa ni watu wasiyo na matumizi.

ukiendelea kuwatikuza ccm utaendelea makubwa kuliko haya.

Kwanini nitie maneno yangu wakati Lukuvi mwenyewe kisha jieleza, kama hujamsikia nikipata clip yake ya aliyoongea jana ntakuwekea.

Mimi ni CCM vile vile lakini nna imani yangu kama ilivyo kwa Lukuvi na Waziri Mkuu, na wao wanasema wakiipa Zanzibar kujitawala wana "hofu" itakuwa nchi ya Kiislaam.

Cha kujiuliza, hawana hofu na Kikwete, na mimi na Waislaam wenine kwa mamilioni waliopo bara kwani wote sisi tunafata huo Uislaam ambao Lukuvi kwa niaba ya Waziri Mkuu ana hofu nao.
 
Kuna nchi na serikali nyingi tu duniani ambazo zina hofu na watu wenye msimamo mkali wa kidini; iwe Waislamu au watu wa dini nyingine. Zipo nchi za Kiislamu ambazo zina hofu na Waislamu wenye msimamo mkali, Saudia, UAE, Misri n.k ni mifano tu. Kwamba mtu ameonesha hofu hii kuhusiana na Zanzibar si suala la kushangaza kwani wapo pia wananchi wa Zanzibar ambao nao yumkini wana hofu hiyo hiyo. Huwezi kuita hii ni "phobia' isipokuwa hujui maana ya 'phobia' ni nini.

Hiyo phobia ya nini? Uislaam wa Zanzibar unamuhusu nini Lukuvi? hata awe na hofu? Nchi yenye Waislaam 99% wakiamua kuwa nchi ya Kiislaam ni kosa? mlitaka waseme wao hawana dini?
 
Kabla ya kutoka bungeni baadhi ya wabunge wa UKAWA jana, Professor Lipumba aliweka wazi aliyoyaongea kanisani waziri mmoja wa Serikali ya Muungano. Lipumba alisema kuna waziri kaenda kuhutubia kanisani kuwa "ikiwa Zanzibar itapewa mamlaka kamili basi mjuwe itaanzisha dola ya Kiislam".

Jana nikauliza ni waziri gani huyo? sikupata jibu humu JF.

Lakini kwa kuwa Mungu hamfichi mnafik, huyo waziri kajitokeza mwenyewe bungeni leo hii na kwanza kukiri kuwa katumwa na Waziri Mkuu na kusema kuwa hiyo ni hofu, "phobia" yake na akaendelea kusema "hakuna yeyote wa kunizuia hofu yangu hii".

Akazunguka wee na maneno lakini akashindwa kukisema kile alichokieleza Lipumba.

Kwa uchache, Lukuvi ameudhihirishia umma kuwa ana "Islamophobia" au hofu ya Uislaam.

Kiongozi unaefikia kutangaza Kanisani na Bungeni kuwa hutaki kuwapa mamlaka kamili Zanzibar kwa ajili ya dini yao, kweli hiyo si Serikali ya Mfumo Kristo tunayoilalamikia siku zote humu?

Na leo Lukuvi kahitimisha kwa kuniunga mkono yale ninayoyasema humu kila siku kuwa huu Muungano upo kwa ajili ya Kanisa. Na unaongozwa na Kanisa. Huwa mnajifanya hamnielewi lakini leo yamebainika bayana.

Wanaonisikitisha zaidi ni wale Wazanzibari waliobaki kuipigia makofi hoja hii ya Lukuvi, halafu wanajiita wao Waislaam. Waislaam mnaambiwa hampewi nchi yenu kwa kuwa Lukuvi ana hofu mkipewa mtaifanya dola ya Kiislaam na nyinyi mnashangilia? Yaani Lukuvi anawaambia kinaga ubaga kuwa mtabaki ndani ya mfuko Kristo mkitaka msitake na mkikataa basi ni bora nchi hii ishikwe na jeshi na akafikia mpaka kuwapa mfano wa Islamic Brotherhood ya Egypt.

Kinachonishangaza hii hofu yanini kwa Lukuvi? ikiwa nchi anayoiongelea ni Zanzibar na Wazanzibari 99% ni Waislaam ikiwa
wataamuwa nchi yao kuwa ya Kiislaam yeye anapatwa na hofu ya nini?

[video=youtube_share;PIAPAAd3Dck]http://youtu.be/PIAPAAd3Dck[/video]

cc Ritz, gombesugu, kahtaan, THE BIG SHOW, CHAMVIGA
Moderator tafadhali usiiunganishe hii na nyuzi nyingine hii maudhui yake inajitegemea.

Kwa hiyo wale Wazanzibar wakereketwa wa KIJANI wanashangilia tu bila kujua kuwa wanaKIJANI wa bara wana nia yenye mrengo uliojificha, lakini mmoja wa wanaKIJANI wa bara kateleza hadi mrengo wao umejulikana? Kama ni hivyo , kweli Mungu ni mkubwa, malengo ya kuwang'ang'ani Wazanzibar ni kwa malengo hayo? Huyo mh. ni wa pili, maneno mengine niliyasikia kwa mzee Mrema.
 
Last edited by a moderator:
Lukuvi alitumwa kusema hayo maneno na pinda...so katumwa na serikali...endeleeni na bunge lenu la,intarahamwe
 
Unajua kaka,uhuru wa habari ni jambo jema sana. Lakin pale unapotumiwa kutoa na kupandikiza maneno kama hv ni hatari mno.

Ni juzi tu nilikuwa nawaza mambo haya. Nikakumbuka Rwanda,jinsi Kagame anabyothibiti habari na juzi Kenya wamepitisha bill inayozuia baathi ya habari kusambazwa.

Unajua nimekuka kuona huu uhuru ndio break through ya maadui wa ndani na nje ya nchi. Serikali za kigeni zinatumia watu kupropagate agenda fulani fulani. Na hii tukifumbia macho itakuwa sio. Watu wanasema marekani kuna uhuru wa habari nani amesema?? Ulishawahi kujiuliza??
Lakni tukija africa wanapiga mayowe kwanini hakuna uhuru. Sababu hizi hizi za mashetani kama huyu dada. Am very disappointed with her. Watu kama hawa there is no mercy.

The king.

Dissapointed na mimi? Lukuvi hujamsikia kwenye TV? au hujasikiliza hiyo hotuba ya Lipumba inam qute Lipumba akisoma gazeti la Mwananchi.

Ukweli siku zote ukidhihiri uongo hujitenga.
 
Hapa hamna gamba wala gwanda, hapa kuna mfumo kristo. Kusoma huwezi basi hata video imekushinda kusikiliza? utakuwa ndio wale wale.
nimeshakwambia mbwa amemla mwanae unacholia lia nini! wewe uislamu huna ni kafir tu! Mfumo kristo mfumo kristo, ndio nini? Mboga!? watu wanapigania haki zao na vizazi vyao wakiwemo waislamu, wakristo, na wapagani wewe unaleta fitna kuwakosa watoto wa baba mmoja laanatulahi0„30„3 Kajilipue basi usepe basi! hakuna asiye kufahamu wewe ni gamba lililo kubuhu mfuasi mtiifu!
 
....Ukizidi kuitetea CCM kwa msimamo huo itasambaratika !!!!

Unammanisha kitadumu pale tu kinapofanya kampeni za mfumo kristo kanisani na tukae kimya? tusioneshe uozo uliokuwepo?
 
Cha ajabu ni kuwa hao wanaolalamikia hegemony ya kikristo (wanaouita mfumo kristo) hawana matatizo na hegemony ya kiislamu! Hawataki haki kwa wote bali wao wapewe haki zaidi. Na haki hiyo iwe pamoja na kutowatendea haki wasio wa dini yao kwa kuwapiga risasi, kwamw'agia tindikali, kuchoma sehemu zao za ibada na matendo mengine kama haya yatakayompendeza mungu wao. Halafu wanamshangaa Lukuvi?

Amandla...

Amandla......
 
Mfumo Kristo umetapakaa kila pahala, hakuna chama utachokwenda ambapo hakuna hilo. Mimi ntapiganana huo mfumo nikiwa ndani ya CCM. Uwanja wa mapambano.

Unajidanganya na usiudanganye umma, huwezi kupinga chochote ukiwa ndani ya CCM utaishha hapa jf tu.
 
kusema ukweli kabisa... Lipumba ameongea vizuri sana

It is too much kwakweli

Kama suala ni kupiga vita udini Dr angetumia mikutano yake ya hadhara kufafanua haya aliyosema pia ktk nyumba za ibada
 
Lakini Lipumba akifanya hivyo msikitini mnakaa kimya maana si uozo!

Amandla......

Lipumba hajasema mambo ya majeshi au christian state.lukuvi amesema wanaotaka serikali 3 wataunda islamic state znz na pia makanisa yatafungwa tanganyika ..huyu ni mchochezi wa kuogopwa kama ukimwi
 
Lipumba hajasema mambo ya majeshi au christian state.lukuvi amesema wanaotaka serikali 3 wataunda islamic state znz na pia makanisa yatafungwa tanganyika ..huyu ni mchochezi wa kuogopwa kama ukimwi

Wote nia ilikuwa ni kujenga uoga na chuki katika waumini wenzao dhidi ya wale ambao sio wa imani yao. Mbona mnajichanganya? Kwani alisema kuwa Tanganyika nayo itakuwa Islamic State hadi makanisa yafungwe huku?

Amandla.......
 
Tumeambiwa humu kuwa Lipumba anaenda Zanzibar kumshtaki Lukuvi. Itakuwa vyema kama akiwa huku akikemea na kuwaasa waislamu wenzake wachache ambao wanawaua na kuwapiga risasi wakristu, kuwamwagia tindikali mabinti wa kikristu, wanaochoma makanisa, wanaovunja sehemu halali za biashara za wasio waislamu n.k. Itakuwa vyema akiwaambia vitendo kama hivi ndivyo vinawatia hofu wakina Lukuvi kuwa serikali ya kiislamu wanayoitaka ni ile inayotakiwa na akina Boko Haram, Al Shabab na watu kama hao. Lakini hatasema hayo bali atasema kuwa huu ni mfano wa mfumo kristu ambao lengo lake kuu ni kuudhalilisha uislamu. Kama muislamu safi hawezi kumkosoa muislamu mwenzake. Ndio maana ametumia mfano wa uovu wa Interahamwe na sio wa Janjaweed ambao ni waislamu wenzake. Hatufai huyu Profesa.

Amandla.....
 
Mawazo yako hayana tofauti na makafiri wa zamani
 
Nathani wenye akili washaona kitu gani kitatokea iwapo Zanzibar itakuwa dola kamili inayojitegemea.

Watu wanakurupuka tu sababu ya uislam. Hawana agenda zaidi ya kulinda dini ambayo hakuna mtu anayoichukua. Kingine nani anajua ukubwa wa Zanzibar?? Wao wajiite nchi kamili lakni wakae kwetu ila wabara hawawezi kukaa Zanzibar bila fitina.

Huu udhalimu na fitina wa kulaumiwa ni Seif na wenzake. Wao wanachotaka znz iwe dola kamili waingie kwa Jumuia ya waislam huku waarabu wakitaka kurudi kwa mgongo wa historia huku tukijua wazi wanataka mafuta.

Tusipokuwa waangalifu tutakuta tumeingia kwenye machafuko ya hali ya juu. Na hawa waarabu wanaharamu ndio wanalotaka. Hakuna mtu wa nje mwenye nia njema na nchi yetu. Sio magharibi wala uarabuni.

Mtu anaongelea Zanzibar kupata dola kamili wakati hana hata hiyo elimu kutwa kukaa vibarazani.

Nashangaa kwanin kina Seif bado wanaishi hawa watu.

The king.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom