Wadau kwa jinsi nilivyo muona Waziri Lukuvi akiongea bungeni kwa jazba bila kutumia busara, in fact aliongea pumba na huyu ni mmoja wa washauri wa Jk. Najiuliza Jk akiwa mezani na washauri wake wawili, kushoto Lukuvi kulia Wasira, nini kitaendelea hapo??
[h=2]Askofu Kakobe kuzungumzia muundo wa Muungano katika Neno la Pasaka 20.4.14[/h]
Taarifa zilizopatikana kutoka kwa waumini wanaosali katika Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), linaloongozwa na Askofu Mkuu Zachary Kakobe, zinaeleza kwamba, Jumapili iliyopita katika Ibada Kuu ya Kanisa hilo, lililoko Barabara ya Sam Nujoma, Mwenge, Dar-Es-Salaam, karibu na Mlimani City; Mzee wa Kanisa anayehusika na matangazo, alitangaza kwamba, katika Ibada Kuu ya Sikukuu ya Pasaka, Jumapili hii tarehe 20.4.2014, Askofu Kakobe atahubiri Neno la Mungu, ambalo pamoja na mambo mengine ya rohoni, litazungumzia pia juu ya mustakabali wa nchi yetu, hususan kuhusu Bunge Maalum la Katiba, linaloendelea na vikao vyake, mjini Dodoma. Hata hivyo, taarifa za uhakika zilizopatikana jana, kutoka kwa baadhi ya Viongozi wa Kanisa hilo, zinafafanua kwamba, Askofu Kakobe, atachukua muda mrefu zaidi katika mahubiri yake, kuzungumzia juu ya muundo wa Muungano unaoifaa nchi yetu.
Ibada Kuu ya Pasaka katika Kanisa hilo, itaanza saa 3 kamili asubuhi, na kumalizika saa 6.30 mchana. Hata hivyo, kwa kuzingatia Kanuni za Maadili ya Mavazi, za Kanisa hilo; Viongozi hao wa Kanisa, wamewakumbusha watu wote watakaohudhuria, kumheshimu Mungu kwa mavazi watakayoyavaa. Watakaovaa vimini, jeans, milegezo, na nywele bandia; hawataruhusiwa kuingia katika Nyumba hiyo ya Mungu. Vilevile, wanawake hawapaswi kuvaa suruali, na wanatakiwa kufunika vichwa vyao. Vivyo hivyo, wanaume hawakubaliki kuingia Kanisani humo, wakiwa wamevaa kofia.