Lukuvi: Nina Hofu na Uislaam aka "Islamophobia".

Lukuvi: Nina Hofu na Uislaam aka "Islamophobia".

Status
Not open for further replies.
Kumbe jamaa Lukuvi ana majigambo hivi? Halafu upotoshaji mwingi mno, aangalie maneno yake yasije kumshtaki baadae...au ni raha ya kushika microphone!
 
Ni kweli alichosema Lukuvi Somalia imeachwa halafu itoke tena Somali nyingine huko Zanzibar hii miji mikubwa ys east africa tutaishije hali uislamu unamini kuua tu asie mwislamu
 
Mheshimiwa Rais Kikwete,

Kwa heshima na taadhima na mapenzi ya hali ya juu niliyonayo katika uongozi wako, siyo siri, ni dhahiri shahiri na kila mwana JF anaweza kuwa shahidi yangu kwa hilo.

Kikwete, nnaamini wewe ni mchapa kazi, nnaamini wewe una muono mpana na mrefu, nnaamini wewe unatimiza wajibu wako kwa kadri ya uwezo wako aliokujaalia Mwenyeezi Mungu.

Nakuomba yasikilize maneno ya William Lukuvi kwa umakini na ujifikirie, huyu William Lukuvi anaitakia mema Tanzania hii?

William Lukuvi amma kwa ujinga wake amma kwa werevu wake, ameutia dosari kubwa utawala wako. Ameenda Kanisani kuwaeleza Wakristo wenzake, tena kwa kujigamba na kejeli na kuonesha kibri ya hali ya juu, kuwa hana imani na Waislaam. Kumbuka iwe Muislaam wa Zanzibar au wa Tanganyika au kokote duniani, Waislaam ni kama kiwiliwili kimoja, unapokiumiza kidole kimoja basi mwili wote unasikia uchungu na unapatwa na maumivu.

William Lukuvi, yuko kwenye Serikali ambayo haina dini! lakini yeye mwenyewe ana dini na alienda kuongea kwenye nyumba ya dini na huko ndipo alipowaudhi Waislaam.

Hiyo ni dosari kubwa sana katika utawala wako. Tunakuomba muachishe kazi haraka sana William Lukuvi kabla hajazua balaa lingine, maana hata alipowahi kwenda kujitetea bungeni alionesha kibri zaidi ya kile alichoonesha Kanisani na akatamba na kuwachiwa muda na Mwenyekiti (mkristo pia) zaidi ya mbunge mwingi yeyote aliyechangia mijadala kwenye bunge maalum, ili ajitetee. Nilifikiri kuwa William Lukuvi ataomba radhi lakini cha kustaajabisha hajaomba radhi na karudia tena na tena na tena kuwa ana hofu na alichokieleza kanisani ni hofu yake na hakuna anaeweza kuhoji hilo.

Sisi tumemuelewa na hatumuhoji yeye, tunakuhoji wewe Rais wetu, jee, kiongozi wako ametugawa au ametuunganisha Watanzania kwa kauli zake hizo?

Jibu lako, mimi silijuwi, lakini jibu letu, ni wazi kabisa kuwa William Lukuvi katugawa Watanzania badala ya kutuunganisha, na si kuwa katugawa Watanganyika na Wazanzibari, la hasha, katugawa Waislaam na Wakristo. Na hilo ni hatari kubwa sana kwa Taifa letu.

Tunakuomba chukuwa hatua za haraka sana, umstaafishe huyu Waziri wako kabla hii athari na mpasuko alotuwekea kuzidi zaidi ya hapa alipotufikisha.

Msikilize:

[video=youtube_share;5gvZyIJkTFY]http://youtu.be/5gvZyIJkTFY[/video]

Nnamalizia kwa kutoa shukrani zangu ikiwa utapata wasaa wa kuyaona haya niliyokueleza.
 
Wakati mwingine una akili zilizotulia na kujaa busara. Huu ushauri ni muhimu sana kwa JK. Akiupuuza atachukua lawama kwa yatakayotokea. Lukuvi ni kipofu na hatuwezi tukamwacha akatembea hovyo hovyo bila kuongozwa, arejee nyumbani apate kuongozwa asije akajikwaa tena. Arudi nyumbani iwe ni ishara dhahiri kwamba JK amemwondoa mchochezi katika serikali yake na hivyo kutuliza hasira waliyopata wenzetu waislamu. Arudi kwao atuachie undugu wetu baina yetu.
 
linapokuja suala la chama mpo pamoja ila kwa kuwa kagusa imani yako tayari ni doa...ndiyo maana tunasema suluhu ya yote haya ni kuwa wamoja kwa kuwa na nchi moja yenye serikali tatu badala ya hii danganya toto ya CCM ya kutuambia nchi moja na serikali mbili huku nyuma ya pazia tukijua ni nchi mbili serikali mbili na mambo mengine yakiendeshwa kimagumashi kuiwakilisha serikali kivuli iliyo likizo (waweza kuuita Tanganyika kama utaona inafaa)
 
Kama haujasukumwa na UDINI kuandika haya, then you have a point to make.

Tiba

Kama Uislaam wangu ndio udini basi Uislaam wangu ndio ulionisukuma kuandika haya, kama umeona nna point ahsante na kama kwa kusukumwa na Uislaam wangu kuandika haya utaifuta hiyo point yako pia sawa.

William Lukuvi amegongelea peg kwenye ufa. Tusipoziba ufa tutajenga ukuta.
 
linapokuja suala la chama mpo pamoja ila kwa kuwa kagusa imani yako tayari ni doa...ndiyo maana tunasema suluhu ya yote haya ni kuwa wamoja kwa kuwa na nchi moja yenye serikali tatu badala ya hii danganya toto ya CCM ya kutuambia nchi moja na serikali mbili huku nyuma ya pazia tukijua ni nchi mbili serikali mbili na mambo mengine yakiendeshwa kimagumashi kuiwakilisha serikali kivuli iliyo likizo (waweza kuuita Tanganyika kama utaona inafaa)

Linapokuja swala la William Lukuvi na aliyoyaongea Kanisani?
 
Mpango wowote haramu hauwezi kuzaa matunda halali. Hawa kama taasisi au kamati ya chama walikaa na kukubaliana jinsi ya 'kumjibu' jaji Warioba, kwa sababu hoja za tume zimejikita kwenye ukweli/facts ni vigumu wenyewe kuzijibu kwa facts zilezile. Hivyo wakaanza 'divide and rule' lakini wengine sababu ya ufupi wa fikra zao either wanaweza kujikuta wana'rule' miti na vichuguu baada ya waliotaka kuwadivide kumalizana au wenyewe ndio wakajikuta wameisha. Muda kidogo tu tutaona.
 
Maneno ya Lukuvi yamebadilisha muelekeo wangu, Naipenda sana CCM, lakini kama huyu Lukuvi hakuenguliwa na Kikwete basi si kura yangu tu ila hata wale wanaonizunguka tutapigia Rais au Mbunge wa upinzani na hasa kama watasimamisha Mgombea mmoja! Hili nimeapa!
 
Faiza wakristo hawatajibu maana nao wameona huyu alivyochafua hewa. Kwani huko zenj waislamu wakiwa asilimia mia tatizo liko wapi? Siku hizi mtu akitaka kukuvamia sio lazima akusogelee. Ni kiasi cha kuset tu computer na anakumaliza. Gone are the days when there was a cold war. Sasa hivi ni ulimwengu wa sayansi na teknologia. Aliacha kusoma speech ya waziri wake ye akaamu kuchafua hewa!!! Huyu alifanya kitendo cha kichochezi kabisa. Wala wakristo hatuungi mkono uchochezi huu. Dini yetu ni ya upendo kwa kila mtu irrespective of colour, religion or race. Nashangaa hajawajibishwa mpaka sasa.
Mheshimiwa Rais Kikwete,

Kwa heshima na taadhima na mapenzi ya hali ya juu niliyonayo katika uongozi wako, siyo siri, ni dhahiri shahiri na kila mwana JF anaweza kuwa shahidi yangu kwa hilo.

Kikwete, nnaamini wewe ni mchapa kazi, nnaamini wewe una muono mpana na mrefu, nnaamini wewe unatimiza wajibu wako kwa kadri ya uwezo wako aliokujaalia Mwenyeezi Mungu.

Nakuomba yasikilize maneno ya William Lukuvi kwa umakini na ujifikirie, huyu William Lukuvi anaitakia mema Tanzania hii?

William Lukuvi amma kwa ujinga wake amma kwa werevu wake, ameutia dosari kubwa utawala wako. Ameenda Kanisani kuwaeleza Wakristo wenzake, tena kwa kujigamba na kejeli na kuonesha kibri ya hali ya juu, kuwa hana imani na Waislaam. Kumbuka iwe Muislaam wa Zanzibar au wa Tanganyika au kokote duniani, Waislaam ni kama kiwiliwili kimoja, unapokiumiza kidole kimoja basi mwili wote unasikia uchungu na unapatwa na maumivu.

William Lukuvi, yuko kwenye Serikali ambayo haina dini! lakini yeye mwenyewe ana dini na alienda kuongea kwenye nyumba ya dini na huko ndipo alipowaudhi Waislaam.

Hiyo ni dosari kubwa sana katika utawala wako. Tunakuomba muachishe kazi haraka sana William Lukuvi kabla hajazua balaa lingine, maana hata alipowahi kwenda kujitetea bungeni alionesha kibri zaidi ya kile alichoonesha Kanisani na akatamba na kuwachiwa muda na Mwenyekiti (mkristo pia) zaidi ya mbunge mwingi yeyote aliyechangia mijadala kwenye bunge maalum, ili ajitetee. Nilifikiri kuwa William Lukuvi ataomba radhi lakini cha kustaajabisha hajaomba radhi na karudia tena na tena na tena kuwa ana hofu na alichokieleza kanisani ni hofu yake na hakuna anaeweza kuhoji hilo.

Sisi tumemuelewa na hatumuhoji yeye, tunakuhoji wewe Rais wetu, jee, kiongozi wako ametugawa au ametuunganisha Watanzania kwa kauli zake hizo?

Jibu lako, mimi silijuwi, lakini jibu letu, ni wazi kabisa kuwa William Lukuvi katugawa Watanzania badala ya kutuunganisha, na si kuwa katugawa Watanganyika na Wazanzibari, la hasha, katugawa Waislaam na Wakristo. Na hilo ni hatari kubwa sana kwa Taifa letu.

Tunakuomba chukuwa hatua za haraka sana, umstaafishe huyu Waziri wako kabla hii athari na mpasuko alotuwekea kuzidi zaidi ya hapa alipotufikisha.

Msikilize:

[video=youtube_share;5gvZyIJkTFY]http://youtu.be/5gvZyIJkTFY[/video]

Nnamalizia kwa kutoa shukrani zangu ikiwa utapata wasaa wa kuyaona haya niliyokueleza.
 
Lukuvi hana haya. Angekuwa ameumbwa na haya angeachia ngazi kwa uchochezi alioufanya. Hata hivyo rais naye amekuwa hachukui hatua mapema mpaka mambo yameharbika ndipo anaamka. Mtu kama Lukuvi katika nchi zilizostaarabika na zenye serikali imara angekuwa alishaachia ofisi na kama si yeye basi aliyemtuma. Lakini hapa kimya. Kwanza aliyemtuma mwenyewe naye anamdomo mchafu na anakesi mahakamani ya kutoa maneno ya uchochezi. Mkuu mwenyewe wa kuwawajibisha naye anatoa maneno ya uchochezi kutaka kutumia jeshi kulazimisha muungano. Mwendawazimu mwingine naye anatangaza bungeni kuwa serikali tatuzikipita anakwenda msituni. Hakuna mwenye nafuu hapo!
 
Linapokuja swala la William Lukuvi na aliyoyaongea Kanisani?

Hii ni namna alivyoona inafaa yeye kuipigia chepuo serikali yenu ya chama chenu kwa kuwapandikiza ddana hiyo wakristu, huenda angeyasema sheikh fulani ndani ya msikiti leo hii ingekuwa mjadala kwa upande wa wakristo kwamba kwanini Sheikh aseme hivi msikitini but all in all...

Sioni tofauti ya approach aliyotumia Lukuvi kueleza hisia za moyoni na jinsi hawa vijana wasio na malezi ya pande mbili bungeni huko wanavyotumia vibaya mbawa za kuikinga CCM kwa kutoa kejeli kwa wazee wema waliomaliza kazi walizostahili kuzifanya!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom