Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
JWTZ ni jeshi la wananchi wa Tanzania hivyo lipo pale kulinda maslahi ya wananchi ambao wao ndio wanaowalipa mishahara. Kama hivi sasa mishahara yao inapatikana kwanini isipatikane tukiwa na serikali TATU? Ikumbukwe kwamba matumizi ya serikali ya muungano yatatokana na bajeti itakayopitishwa na bunge lake likiwa na vyanzo mahususi vya mapato!! Luluvi na wote wanaotumia propaganda ya kuwatisha wananchi kuwa jeshi litachukua/pindua serikali iwapo kutakuwepo serikali TATU wajue kuwa wanawatukana wanajeshi wetu kuwa hawajui wajibu wao na vitendo hivi vya wakina Lukuvi ni vya kihaini!!!
JWTZ ni jeshi la wananchi wa Tanzania hivyo lipo pale kulinda maslahi ya wananchi ambao wao ndio wanaowalipa mishahara. Kama hivi sasa mishahara yao inapatikana kwanini isipatikane tukiwa na serikali TATU? Ikumbukwe kwamba matumizi ya serikali ya muungano yatatokana na bajeti itakayopitishwa na bunge lake likiwa na vyanzo mahususi vya mapato!! Luluvi na wote wanaotumia propaganda ya kuwatisha wananchi kuwa jeshi litachukua/pindua serikali iwapo kutakuwepo serikali TATU wajue kuwa wanawatukana wanajeshi wetu kuwa hawajui wajibu wao na vitendo hivi vya wakina Lukuvi ni vya kihaini!!!
Vita akapigane kwao,Tanganyika lazima irudi!
![]()
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Uratibu na Bunge), William Lukuvi.PICHA|MAKTABA
Na Habel Chidawali na Fidelis Butahe, Mwananchi
Jumatatu,Aprili14 2014 saa 9:37 AM
Kwa ufupi
Ataka Watanzania kuwaombea ili serikali mbili zipite.
Dodoma/Dar. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Uratibu na Bunge), William Lukuvi ameanza kampeni kanisani kuwataka wananchi kupinga serikali tatu zilizopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, vinginevyo nchi itatawaliwa na jeshi kwa kuwa Serikali ya Muungano itashindwa kuwalipa mishahara wanajeshi.
Alisema hayo jana katika Kanisa la Methodist, Jimbo la Dodoma alipokuwa mgeni rasmi akimwakilisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Katika hotuba yake, Lukuvi aliwaeleza waumini waliofurika katika ibada ya kumsimika Mchungaji Joseph Bundala kuwa askofu wa kanisa hilo katika jimbo kuwa waendelee kuliombea Bunge lifanye uamuzi sahihi wa serikali mbili.
Aliwataka Watanzania kuipuuza Rasimu ya Katiba katika suala la Muungano na Serikali tatu kwa madai kuwa kutaka kuwapo mfumo huo ni kutaka Watanzania waingie vitani.
"Serikali tatu zikipita ni wazi kuwa hata makanisa yatafungwa kwani nchi haiwezi kuwa na amani tena, angalieni nchi ya Korea Kusini na Korea Kaskazini ambao waligawanyika na sasa ni maadui wakubwa wanaokaa mipakani wamenyoosheana bunduki," alisema na kuongeza:
"Waumini ndugu zangu wapendwa, kwa sasa tupo katika hali mbaya sana hapo bungeni, tunaomba mtuombee kuna watu ambao wanataka madaraka kwa nguvu na wameanza kutafuta jinsi ya kuvunja Muungano na kudai kuwapo kwa Serikali tatu, nawaomba sana wapuuzeni wale wote ambao wanataka serikali tatu."
Alisema watu wa aina hiyo wanaonekana kuwa wana huruma na Watanzania na wanadai kuwapo kwa Serikali ya Tanganyika wakati hiyo Tanganyika wanayoidai ni jina tu ambalo Wajerumani walikaa mezani wakabuni na kutuletea.
Lukuvi alisema Wazanzibari wanaotaka kuwa na nchi yao hawawezi kujitegemea, bali wanataka Serikali ili wapate nafasi ya kujitangaza kuwa ni nchi ya Kiislamu.
Alisema wanaopiga kelele wana ajenda za siri na nia yao kutaka kufanya fujo na kusababisha machafuko... "Kwani ukiwa na mke mmoja akakushinda unafikiri utatuzi ni kuoa mke mwingine?"
Baadaye alipotakiwa kufafanua kauli yake, Lukuvi alisema alichokizungumza kanisani hapo ni mawazo yake binafsi ambayo yanafanana na Watanzania wengi, akiwamo Rais Jakaya Kikwete.
"Unajua jeshi haliwezi kukaa na bunduki bila fedha. Hiyo Serikali ya tatu ambayo jeshi litakuwa chini yake haina vyanzo vya mapato vya kueleweka, sasa hao wanajeshi watalipwa nini? Wenye mitutu watakubali kuishi bila fedha?"
Alisema hata vyanzo vya mapato ambavyo vimeandikwa katika Rasimu ya Katiba ni lazima visimamiwe na pande mbili za Muungano, akiwa na maana ya Tanganyika na Zanzibar na kwamba kama upande mmoja ukishindwa kuchangia hali itakuwa mbaya.
"Kama tunataka serikali ya tatu ni lazima tuhakikishe kuwa inakuwa na vyanzo vya uhakika vya mapato. Jambo hili siyo ubishi wala ushindani ni suala la kujenga hoja na kujadili kwa kina, ni ngumu sana katika utekelezaji wake," alisema.
Rais Kikwete wakati akizindua Bunge la Katiba mjini Dodoma aligusia suala hilo ambalo Lukuvi alilieleza katika ibada hiyo.
Kwa upande wake, Askofu Bundala alisema kanisani hapo kwamba ili kudumisha Muungano ni vyema Katiba ya Zanzibar ifutwe ili iwepo moja ya nchi moja ambayo inadumisha Muungano.
Alisema angetamani kumshauri Rais alivunje Bunge la Katiba kutokana na Bunge hilo kukosa mwelekeo na kukosa adabu.
Alipotakiwa kufafanua baadaye kuhusu kauli ya Lukuvi, askofu huyo alisema kuwa Waziri huyo hakutakiwa kutoa kauli nyepesi kama ile ukizingatia yeye ni mtu aliyepo madarakani.
"Kauli ya Lukuvi ilikuwa nyepesi sana kuzungumzia kwamba nchi itaingia kwenye vita. Ilitakiwa aende mbele zaidi kama mtu mwenye madaraka kwa kufafanua zaidi," alisema.
"Mimi nataka serikali mbili kwa sababu tumeshazoea kusali chini ya miti tukiwa na amani na tukiwa na serikali tatu tutasali kwa mtutu. Kama umeshindwa kuwatunza wanawake wawili ulionao je, huyo wa tatu ambaye humjui tabia yake utamtunzaje?" alisema.
Chanzo Mwananchi
hivi huyu lukuvi ana elimu gani?