Lukuvi: Tukipitisha serikali tatu jeshi litatawala nchi

Lukuvi: Tukipitisha serikali tatu jeshi litatawala nchi


Na Nuzulack Dausen, Mwanachi
Jumatano,Aprili16 2014
Kwa ufupi


"Rais Kikwete naye alikuwa mwanajeshi, sasa kuna ubaya gani kama mwanajeshi akitawala nchi. Kuna ubaya gani mwanajeshi mwenye akili akitawala nchi yetu. Mbona Komba (Kapteni John Komba), aliwahi kuwa mwanajeshi na sasa ni Mbunge wa Mbinga Magharibi. Jeshi ni la wananchi na hao wanajeshi wanaowasema wengine huwa tunakutana nao klabu za muziki."

Baadhi ya wasomi wasema Waziri Lukuvi hakustahili kutoa kauli hiyo katika eneo la ibada. Dar es Salaam. Siku chache baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu wa Bunge), William Lukuvi kudai kuwa iwapo mfumo wa serikali tatu utapita, jeshi litachukua nchi, wanazuoni wametafsiri kauli hiyo kuwa ni ya kuwajengea hofu wananchi.
Jumapili Lukuvi, akiwa katika Kanisa la Methodist, Jimbo la Dodoma alikokuwa mgeni rasmi akimwakilisha Waziri Mkuu, alisema muundo huo utasababisha nchi kutawaliwa na jeshi kwa kuwa Serikali ya Muungano haitakuwa na fedha za kulipa mishahara wanajeshi.

Lakini mhadhiri wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Mohammed Bakari amesema kauli hiyo ilitolewa katika jukwaa lisilo sahihi hususan kwa kiongozi kama Lukuvi.

"Kila kauli ina mahala pake. Haikutakiwa kwa mtu mwenye madaraka kama yule kuzungumzia mambo nyeti kama hayo kanisani," alisema Dk Bakari.
"Licha ya kwamba kauli yake si mpya ilishasemwa na Amiri Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Kikwete, lakini ilibidi ayaseme hayo ndani ya vikao vyao na si kanisani."

Alisema pamoja na kwamba kiongozi huyo alitoa maoni yake binafsi, ilitakiwa aangalie kwanza kauli yake kabla ya kuitoa. "Unapokuwa na nafasi ya juu ya uongozi, uhuru wako wa kutoa maoni binafsi unapungua. Kwa hiyo kupitia nafasi hiyo itabidi uzingatie masuala ya kuzungumza ukiwa raia, pia kiongozi," alisema.

Mwanasheria Harold Sungusia alisema watu wanaodai serikali mbili wamepungukiwa na hoja na ndiyo maana wanaanzisha masuala mengine yasiyo na tija. "Nimepitia sheria zote nikagundua kuwa mtu anayetetea hoja ya serikali mbili anakosa hoja za msingi ukizingatia tayari muundo huo wa Muungano umedumu kwa miaka 50."
Hata hivyo, mhadhiri wa Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Alexander Makulilo alisema Watanzania hawatakiwi kuacha kufuata hoja za msingi na kutishika na propaganda. "Hizo ni propaganda kwa sababu hakuna utafiti uliofanywa na kugundua kuwa serikali tatu zitaleta vurugu."

Mkazi wa Mbagala Mtongani, Isaiah Solomon alisema alichosema Lukuvi kinaweza kuwatisha raia hususan wale walio na uelewa mdogo juu ya masuala ya siasa.

"Si jambo jema kusemea mambo hayo kanisani. Pia alizungumzia kuhusu kugharimia jeshi, sifikiri kama ni wanajeshi pekee wanaoweza kuleta madhara iwapo fedha za kuwalipa zikiwa pungufu; wapo wafanyakazi wengine watakaoleta balaa," alisema Solomon.

Mwenyekiti wa chama cha UDP Mkoa wa Dar es Salaam, Joackim Mwakitinga alisema woga wa wanasiasa wanaotaka serikali mbili ndiyo unaofanya watoe kauli za kuogofya wananchi.

"Naona ni woga tu wa wanasiasa wanaotaka kuleta mambo ambayo hayapo katika hoja za muundo wa Muungano," alisema. Mjumbe wa Bunge la Katiba, Joseph Mbilinyi alisema kauli hiyo inadhihirisha jinsi wanaopigia debe serikali mbili walivyo waongo.

Akichangia mjadala bungeni jana, Mbilinyi alisema: "Rais Kikwete naye alikuwa mwanajeshi, sasa kuna ubaya gani kama mwanajeshi akitawala nchi. Kuna ubaya gani mwanajeshi mwenye akili akitawala nchi yetu.

Mbona Komba (Kapteni John Komba), aliwahi kuwa mwanajeshi na sasa ni mbunge wa Mbinga Magharibi. Jeshi ni la wananchi na hao wanajeshi wanaowasema wengine huwa tunakutana nao klabu za muziki."

Chanzo Mwananchi
 
Wakuu kama kweli kauli hii imetolewa na kuna ushahidi huyu jamaa anaweza kufikishwa mahakamani kwa kutoa vitisho, uchochezi, chuki dhidi ya jeshi la wananchi na kulipaka matope, na hata kusema kuwa litapindua nchi. Inabidi pia aeleze nani amempa mamlaka ya kuwa msemaji wa jeshi, wakati jeshi lina msemaji wake, na wakati anajua kabisa katiba yetu hailiruhusu jeshi kujihusiha na mambo ya siasa.
 
Huyu Waziri Mwenyezi Mungu kamuumbua kwa kudhihirisha Chuki zake dhidi ya Waislam
Anapaswa kushtakiwa kwa Kesi ya Uchochezi
 
Wasaliti wakubwa wa nchi yetu tanganyika ni wabunge wa ccm kutoka tanzania bara, lukuvi pia yumo katika kundi hilo! Hivi anaposema watanzania waombe mungu serikali mbili zipite, kwani kwa sasa zilizopo ni serikali ngapi? Kweli nimeamini, waliozoea kuishi kwa uwongo hawawezi kujifunza katika kweli!
Yaani wanavyoitamka hiyo serikali 2 na kuipigia debe utafikiri ni INNOVATION mpya kabisa ya ccm kumbe ni ili waendeleze upuuzi wao
 
Wakuu salaam.
Nimekuwa nikitafakari juu ya kauli ya "Jeshi linaweza kuchukuwa madaraka ikiwa serikali tatu zitapita",ikumbukwe kuwa kauli hii imeongelewa mara mbili tofauti na viongozi wawili waandamizi wa Chama na serikali. Awali alianza Rais na mwenyekiti wa ccm ikiwa Bungeni kuzindua Bunge alinukuliwa akisema maneno hayo, Kama vile wananchi hawakusikia vizuri Lukuvi akiwa kanisani alirudia kauli hiyo tena kwa msisitizo akishadidia hoja ya mwenyekiti wa chama chake.

Sasa sote tunajua kuwa pamoja na wanajeshi wetu kutolipwa vizuri kulingana na umasikini unaotukabili kama nchi Wanajeshi wetu wamekuwa wazalendo kiasi cha kupigwa mfano. Hatujawahi kusikia malalamiko wala mgomo wa wanajeshi wakipinga kutolipwa au kucheleweshewa malipo ya mshahara wao. Mara zote wamekuwa wakijituma kila wanapokwenda kushiriki oparesheni mbali mbali wamekuwa wakishiriki kwa mafanikio makubwa.

Sasa hii ya kulalamika jeshi kuchukua madaraka limetoka wapi? Je tumefikia hatua ya kuwaona wapiganaji wetu ni waroho wa madaraka kiasi cha kupindua utawala uliopo madarakani? Kwanini tuishiwe ushawishi kiasi cha kulisingizia jeshi letu ambalo linaheshimika duniani kote mambo ya ajabu kiasi hicho. Hivi Mwamunyange akisikia uzushi kama huo atajisikiaje? Mtu ambaye amekuwa akililea na kulitunza jeshi kwa uadirifu mkubwa leo anaambiwa jeshi lake linaweza kupindua utawala ulioko madarakani kwasababu tu ya serikali tatu?

Hapana nasema HAPANA hii haikubaliki ni lazima tuwakemee hawa wanasiasa uchwara wanaotaka kutuchonganisha na jeshi letu makini ktk ukanda huu wa africa.
Ieleweke mtu hukisema kile kiujazacho moyo wake hii si kauli ya bahati mbaya ilipangwa kwa muda mrefu kunawatu wamechoka na utulivu tulionao kwa muda mrefu sasa wanaanza kupandikiza chuki kwa maslahi ya wao kuendelea kuwepo madarakani hii inapaswa kukemewa na kila mpenda amani popote Tanzania.

Nashangaa hata viongozi wa dini kutokemea kauli za namna hii tena kiongozi mwingine akiwa kanisani na Lukuvi alidiriki kusema Zanzibar wanapaswa kufuta katiba yao ili iendane na katiba ya muungano hii ilidhihirisha wazi alikubaliana na kauli hiyo mufirisi toka kwa Lukuvi hii haikubaliki tunaandaa maangamizi yetu wenyewe kwaajili ya wanasiasa majinuni walio ishiwa ushawishi na hoja kwa wananchi.
Kwakweli nina hasira sana naomba niishie hapa. TAFAKARI

BACK TANGANYIKA
 
LUKUVI "Tunataka muundo wa serikali mbili ili kuwadhibiti Waislamu"

Dalili mbaya za Bunge Maalum la Katiba kuondoka Dodoma bila kutungwa Katiba mpya zimeanza kuonekana, baada ya wajumbe wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kususia kikao jana na kutoka nje ya bungeni.

Wajumbe hao wanaounda umoja huo kutoka vyama vya CUF, Chadema, NCCR-Mageuzi na wa vyama vingine, walichukua hatua hiyo baada ya kuanza kwa kikao cha jana jioni.

Sababu iliyosababisha kutoka nje kwa wajumbe hao kauli ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, waliyodai kuwa ni za ubaguzi na vitisho akiwa kanisani kwamba Wazanzibari wanaotaka serikali tatu wanataka ijitenge ili iwe nchi ya Kiislamu......................

.................“Hii ni Rasimu ya Tume ya Rais na si rasimu ya Wapemba, lakini katika mjadala wetu hapa umekuwa na utaratibu wa ubaguzi, watu wamebaguliwa humu na viongozi wakubwa wanapiga makofi, Bunge hili limekuwa kama Bunge la ‘Intarahamwe’, hii ni hatari kwa nchi yetu,

“Wapemba, Waarabu, Wahindi, Wakongo, hii hatuitaji katika nchi yetu, tunahitaji katiba ambayo itahakikisha kila mwananchi anapata haki yake wote tuwe sawa, bila kujali, rangi zetu, makabila yetu, dini zetu, hii ndiyo nchi aliyotuachia Mwalimu Nyerere,” alisema.

Kabla ya kufunga kikao hicho, Prof. Lipumba, alitoa fursa kwa mjumbe anayetaka kusema chochote, ambapo Mchungaji Mtikila, alieleza kuwa, alipata taarifa kuwa Lukuvi aliwaambia waumini wakanisa hilo kuwa wanataka muundo wa serikali mbili ili kuwadhibiti Waislamu.

“Hili linakwenda kinyume cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotoa uhuru wa kuabudu kwa wananchi, hili ni lazima tulifanyie kazi ni kubwa,” alisema Mchungaji Mtikila.

Ninawakilisha

Movie nzima utaipata hapa
[h=2]Ukawa wajiengua Bunge la Katiba[/h]
Home
 
Mkuu ndicho umeona cha maana kuandika hapa sijaona hoja hata moja pengine jipange vizuri utulie na ujenge hoja kwa kutueleza nini unachokitaka kutueleza vema lakini kwa hizi hoja ni nyepesi sana.
 
Hakuna chochote kitachozuia mm kusema,nitasema kweli na nitarudia kusema kweli nikweli cku ,,,tbc wanakataka matangazo jamani kudadedeki tbccc,,,,
 
Kwa sababu jeshi wameshapewa 'go on' na watawala sasa huu ni wakati wao nao kula matunda ya nchi, wachukue nchi tu wakamate watawala wawauwe wote wakalie nchi nao.
Wameshapewa uhakika wa kuchukua nchi, watawala wame-surrender.
Jeshi kamateni nchi sasa.
 
Zanz na tangayika wanaweza kugeuka kuwa km korea kusin na kask,,luga hyohyo watu wale wale, tutaleta ubaguzi nawakati cc ndugu,sisi tunajua n serikali 2 km nyie hamjajiandaa kwajili ya serikali 3 shauri zenu.serikali ni 2 nahakuna lingne zaidi ya hyo,,nivitisho kwakwenda mbele
 
Hakuna mahala ambapo jeshi limechonganishwa na watanzania lakini wewe kwa matakwa yako binafsi unataka kutengeneza mgogoro ambao wewe unadhani ni sahihi lakini hapana hapana hapana hapana hapana.
 
Lukuvi anaonge sasa bungeni sijaelewa anajibu hoja alizotuumiwa jana na UKAWA, anachangia hoja kuuu au anajibu kama waziri wa nchi?

Sijaelewa lengo lake sasa ana dakika kumi na tano zaidi ya kumi kuu anatamba tuuuu.... sijamuelewa kabisa.

"Uamusho ni taasisi ya kidini". "Cuf wanataka kuiongoza zanzibar kwa kushirikiana na uamusho". Ni maneno yaliyosema na mgonjwa jamani. Sijui Mungu atatukwamuua vipi/lini na hawa wagonjwa.
 
inashangaza,,lukuvi ameitwa kuja kujibu tuhuma za uchochezi wa kidini kanisani,,
lakini mbona amejikita kwenye muundo wa serikali na mambo mengine,,,,amajilita kwenye vijembe na mipasho,,,

ajibu tuhuma na sio kukwepa,,,,
 
Hakuna chochote kitachozuia mm kusema,nitasema kweli na nitarudia kusema kweli nikweli cku ,,,tbc wanakataka matangazo jamani kudadedeki tbccc,,,,
Lukuvi uje useme na vijiweni basi.
 
Tatizo la wabunge wa CCM ni kama wamechukuliwa msukule!! yani hawana ulimi hata kidogo wa kuongea wanachofikiri kwamba ni sahihi kwao kusema!!! yani nikisikiliza wanavyochangia kwenye bunge la katiba nacheka sana maana wamelishwa maneno ya kusema kama makinda ya ndege. Ndugu zangu mi niambie watu wanaoharibu mchakato wa katiba ya watanzania ni watu wachache sana yani hawazidi hata 5 Lukuvi akiwa mmojawapo ila sasa yeye anaendeshwa kama Robot maana ni kilaza wa kufa mtu na haelewi matokeo ya ujinga anaotumwa kufanya na ni namna gani yanaweza kumuathiri yeye hata na familia yake baadae in case mambo yakichafuka hapa. Anafikiri kwa sababu hiyo kauli aliitoa Kikwete basi ni kauli sahihi na ni ukweli mtupu.ukijaribu kuangalia Kikwete yeye wakati anatoa kauli ile alikuwa makini sana na maneno yake maana alikuwa anaelezea situation/possibilities lakini ukimsikiliza Lukuvi yeye anasema kwa uhakika kabisa as if ni jambo ambalo limeshajadiliwa na vikao Fulani na maamuzi yameshafanyika kwamba ni lazima ifanyike hivyo. mi naamini hata kama kulishafanyika vikao kama hivyo ni kwamba Lukuvi atakuwa ameharibu maana ametoa siri bila kujua kwamba hakustahili kutoa siri hiyo katika nyakati kama hizi!!!! Hii ni akili ndogo tuu inamsumbua huyu mzee!!!!!!BASI NA TUSUBIRIE TUONE MWISHO WA HII MOVIE YA LUKUVI NA CCM YAKE!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom