Mwamba Usemao Kweli
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 744
- 186
Kwa kitendo cha kujifanya ni mjuaji wa hali ya juu ndugu yangu tundu lisu anaendelea kuvuruga na kuuporomosha upinzani wa kisiasa tanzania. Kumdhihaki kwa sauti ya juu hayati mwl nyerere hata kama ni binadamu na anamakosa ktk utumishi wake wa umma hakutakuacha hivi hivi ndugu yangu.
Hekima na busara ya kawaida kabisa inahitajika kuwaenzi wazee wetu iwe ni katika ngazi ya familia au hata ya taifa. Ikumbukwe tu kuwa hayati nyerere ameishi na kuitumikia nchi hii kwa uadilifu wa hali ya juu na hakuwahi kujilimbikizia mali wala kuwa fisadi kama tunavyoshuhudia viongozi wa leo.
Hayati mwl nyerere aliishi kwa umaskini mkubwa na kutumia muda wake wote kuwapigania wanyonge wa ndani ya taifa hili na nje ya nchi hii. Amehakikisha tanzania imekuwa ni nchi ya mfano kwa amani na umoja katika africa.
Kwa vyovyote vile katika medani za siasa za nchi hii, yeyote anayemdhihaki kwa matusi, dharau na fitna hatasalimika kisiasa.
Ni ujumbe kwa tundu lisu na wenzako kuwa tunahitaji katiba bora yenye kuwajali na kutatua kero za watanzania. Lakini ni vema iwe kwa staha na kwa hekima si kwa fujo wala matusi.