Lukuvi: Tukipitisha serikali tatu jeshi litatawala nchi

Lukuvi: Tukipitisha serikali tatu jeshi litatawala nchi

Naomba mnisaidie kidogo; alichosema Lukuvi kina tofauti gani ya kimaana na alichosema Kikwete mbele ya Bunge la Katiba juu ya jeshi kutwaa utawala?
 
Naomba mnisaidie kidogo; alichosema Lukuvi kina tofauti gani ya kimaana na alichosema Kikwete mbele ya Bunge la Katiba juu ya jeshi kutwaa utawala?
Tatizo maeneo waliosemea mmoja kasemea bungeni mwingine kanisani.
 
Tatizo maeneo waliosemea mmoja kasemea bungeni mwingine kanisani.

..kwa hiyo huoni tatizo kuhusu alichokisema JK, kwasababu tu amekisema ndani ya bunge?

..Lukuvi alipohojiwa amesema msimamo wake unafanana na wa Raisi Kikwete.

..pia Lukuvi alikuwa pale kumuwakilisha Waziri Mkuu, au serikali ambayo Raisi na Amiri Jeshi wake mkuu ni Raisi Kikwete.

..Je, Raisi hana tatizo na alichokisema Lukuvi kwa niaba ya serikali yake? Je, Raisi atamchukulia hatua gani?

cc gombesugu, FaizaFoxy, THE BIG SHOW, Nguruvi3
 
Last edited by a moderator:
Anasema kwa habari alizonazo ambazo wengine waliomo ambao wamebaki kwenye BMK ,habari alizonazo ni kuwa CUF na CHADEMA wanamikataba kati yao ,CUF itapewa Serikali ya Zanzibar na CHADEMA watapewa serikali ya Tanganyika na CCM wataachiwa ya Muungano ,naamini kabisa Lukuvi hajui atendalo.:A S 39:
 
..kwa hiyo huoni tatizo kuhusu alichokisema JK, kwasababu tu amekisema ndani ya bunge?

..Lukuvi alipohojiwa amesema msimamo wake unafanana na wa Raisi Kikwete.

..pia Lukuvi alikuwa pale kumuwakilisha Waziri Mkuu, au serikali ambayo Raisi na Amiri Jeshi wake mkuu ni Raisi Kikwete.

..Je, Raisi hana tatizo na alichokisema Lukuvi kwa niaba ya serikali yake? Je, Raisi atamchukulia hatua gani?

cc gombesugu, FaizaFoxy, THE BIG SHOW, Nguruvi3
Lukuvi, kasema mengi sana tofauti na JK, hivi si nyie mapovu yalikuwa yanawatoka Lipumba kuongea Msikitini, leo hii Lukuvi kuwapa wakisrto maelekezo wachague serikali mbili, mmekaa kimya,,daa!!!! chini hii kuna wazalendo wengi sana wabandia.
 
Waziri Lukuvi avujisha kimakosa siri ya ccm kupinga serikali tatu, wakati anajibu kwa jazba kubwa tuhuma za ukawa dhidi yake kuwa ametumia udini na vitisho vya jeshi kuchukua nchi kama gia ya kupinga serikali tatu huku akipigia debe serikali mbili.

Hata hivyo, kwa bahati mbaya sana katika maelezo yake alitoa siri ambyo ninaamini alitoa katika hali ya jazba na sasa anajutia jambo hilo. Waziri lukuvi alisema, namnukuu,

Tuna taarifa za siri kuwa ushirikiano wa ghafla kati ya chadema na CUF una lengo la kusaidiana baina yao, ili CUF wachukue Zanzibar na Chadema wachukue Tanganyika, halafu Serikali dhaifu ya Muungano watatuachia CCM. Kwa taarifa yenu hiyo ndo siri ya ushirikiano kati ya Chadema na ccm. Hakutaja NCCR, sijui sababu.

Swali ni je, kama CCM wanapigania serikali mbili kwa sababu ya kuhofia chadema kuchukua Tanganyika na CUF kuchukua Zanzibar, je huo sio ubinafsi.

Kama hiyo ndo sababu yao kupigania serikali mbili, kwa nini wanamtukana Mzee Warioba na tume yake? Na kwa nini wanawadanganya wananchi kuwa Jeshi litachukua nchi? Au wanaibua hoja dhaifu ya gharama kubwa ya kuendesha serikali tatu?

Sasa nimejua sababu halisi ya ccm kupinga tume Amina Salum wa Zanzibar, Jaji Kisanga, Jaji Nyalali, Jaji Warioba ambazo zote kwa pamoja zilipendekeza serikali tatu. Sababu kubwa ni hii, wanalinda mkate wao. Mungu haachi kumfichua unafiki wa Mwongo.
Hata hivyo, mimi kama mtanzania sijawahi kuwasikia ukawa wakisema kuwa wanaunga mkono serikali tatu kwa sababu alizotaja Lukuvi. Ukawa wanaung mkono rasimu ya Warioba. Full stop.

Hoja hii nimeibuka nayo baada ya rafiki yangu moja ambaye ni kada mzuri sana wa ccm kulalamikia sana kauli akidai kuwa Lukuvi amewauza kwa kutoa siri hiyo kimakosa.

Nawasilisha.
 
Sikuwahi kumdharau Lukuvi ila leo alipotoa uteterzi wake. Alisema mambo ambayo mtu mzima tena waziri hangetakiwa kuyasema!
 
chili bunge maalumu la katiba limepwaya kuliko kawaida.natamani rais awaze vema
tena kwa kichwa chake mwenyewe Vila kushirikisha ushauri was akina lukuvi afute bunge hili na aunde jingine lisilo na wanasiasa. maccm wameharibu mwenendo wrote.
kinacbijadiliwa hakipo hata katika rasimu was hakikuwa maoni ya watanzania. hakuna name sijui hio rasimu wameipata wapi wanayoijadili , kwani rasimu ni ya serikali tatu.
 
Tunajua kuwa Mungu yuko upande wetu na atatupigania na kututetea na atatukabidhi Tanganyika yetu. acha waendelee kuwewesema nabado njia ya mwongo ni fupi...... bado kutuambia na hati nibandia watasema yote wazhungu walisema time will tell.
 
Siku ya kufa nyani miti yote huteleza. Sijawahi kuona mtu wa ajabu kama LUKUVI, inakuwaje ameshindwa kukiri ama kukanusha tuhuma dhidi yake Kanisani. Ama kweli CCM una wenyewe na wenyewe ni akina LUKUVI na washika dau wao
 
Problem: Znz ikiwa na serikali huru.
itaanzisha dola ya Kiislam

Fact: Wakristo waishio Znz hawafiki

%1

Solution: Wakristo waishio Znz

wahamishiwe Ukerewe,
kama suala ni kuishi.
visiwani!

Justification: Refer Pakistan-

Bangladesh migration,




Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Ajabu ya mambo eti MaCcm yanadai UKAWA ni waroho wa madaraka, ili Hali wao ndio wasaka tonge na hawataki katiba ya wananchi kwa maslahi yao. Kwao CCM, uongo ndio ukweli na ukweli ndio uongo.
 
Lukuvi ni Janga la kumi na moja la Taifa baada ya hili jipya la mvua...akiwa daraja moja na ujinga, maradhi, Umasikini, ukimwi, U-CCM etc etc etc.
 
Hakika Lukuvi amechemka sana ingekuwa nchi nyingine mpaka sasa angekuea ameshajiuzulu, kauli yake ni aibu sana
 
Back
Top Bottom