A
Anonymous
Guest
Kuna tatizo kubwa la upungufu na ukosefu wa maji kwa vitongoji kadhaa kwenye vijiji hivi viwili ambapo baadhi ya wananchi wanapata maji kwa mgao na wengine hawapati kabisa.
Mamlaka ya maji (IRUWASA) haipokei wala kuunganisha maji kwa wateja wapya wa Kijiji cha Luhindo kwa maelezo ya upungufu wa maji, wakiulizwa wanasema kuna mradi mkubwa wa maji unakuja ambao utamaliza tatizo kwa vijiji vyote vinavyoizunguka makao makuu ya Halmashauri yaani vijiji vya Luhindo, Lulanzi, Kilolo na Luganga.
Kiuhalisia mradi huo unategemewa kukamilika Mwaka 2029, hivyo wananchi tuvumilie kukosa huduma muhimu ya maji mpaka mwaka 2029.
Wakati hayo yote yanaendelea vijiji vya Luganga na Kilolo havina shida ya maji na chanzo cha hayo maji na ma-tank yake yapo hapa lulanzi ambako wakazi wake tunaambiwa na mamlaka tuwe na subira mpaka mwaka 2029 mradi mkubwa utakapojengwa na kukamilika.
Uamuzi wa Waziri wa Maji ~ Aweso: IRUWASA ikamilishe mradi wa muda mfupi ndani ya mwezi, Vijiji vya Luhindo na Lulanzi vipate maji
Nashauri mamlaka ya maji na Serikali kuunganisha maji toka kwenye ma-tank yanayopeleka maji Kilolo na Luganga kwa wananchi wa vitongoji vya Luhindo na Lulanzi visivyo na maji ili na sisi tupate maji huku tukisubiri huo mradi kwani tunateseka sana kufuata maji mabondeni ambako ni mbali wakati vyanzo vya maji vipo.
Pia kuna miundombinu na baadhi yetu wameunganishiwa mabomba na wengine tuna mwaka tumeomba kuunganishiwa lakini tumekataliwa.