Lulu arudi chuo, anachukua telecommunication engineering

Lulu arudi chuo, anachukua telecommunication engineering

yuko UDSM? hehee labda atumie njia mbadala kupennya. Tena kasema ' anachukua' sio anasoma mweee!
 
Iyo filamu ishatoka? Itauzwa kopi bei gani? Au ni title ya filamu tu?.
 
Lulu naye! Anadhani hatujui anasoma hapo Magogoni hicho chuo kinaandaa masekretari.. Na wako kwenye mitihani kuanzia wiki jana.

Siku hizi ukisoma MS Word na XL Unasoma Engineering???[emoji23] [emoji23]
Hapo sasa ndipo wanaponishangaza!
 
Huyu binti anasoma Telecommunication engineering? Aisee!! Isije ikawa hata hajui anasoma nini maana akili zake ni hatua saba mbele. Na chuo kipi? Maana siku hizi mpaka Dar Star College, Amazon College, English Fountain wanatoa kozi hizi. Ikiwa huyu binti anasoma hii course na kwenye reputable institution, basi nachana cheti cha MBA na kurudi shule upya kwenye eneo la Telecommunication engineering.
 
Yaani hawa wasanii uchwara wanavyoropokaga hadi kero.... Kwenda hapo magogoni secretary ndo keshakuwa engineer?!.. Majizzo ana kazi asee
 
Hahahah akiweza zile tan na cos basi atasoma hadi phd
 
Lulu naye! Anadhani hatujui anasoma hapo Magogoni hicho chuo kinaandaa masekretari.. Na wako kwenye mitihani kuanzia wiki jana.

Siku hizi ukisoma MS Word na XL Unasoma Engineering???[emoji23] [emoji23]
Haaaaaa[emoji2][emoji2]
 
Msanii mahiri wa filamu Elizabeth Micheal ‘Lulu’ amerudi chuoni na kuamua kuchukua kozi ya Telecommunication engineering.

Muigizaji huyo ameweka wazi anachosomea baada ya mashabiki katika mtandao wa Periscope, kutaka kujua anasomea nini baada ya kupost video mbalimbali katika mtandao huyo huku akizungumzia maswala ya chuo.

“Jamani nimechoka kuulizwa nasomea nini, nasomea nini, nachukua Telecommunication engineering,” alisema Lulu.

Muigizaji huyo hakupenda kuweka wazi ni chuo gani anasoma, lakini aliweka wazi wiki hii naingia katika mitihani.

Lulu ni miongoni mwa wasanii wachache wa filamu walioamua kurudi darasani na kuongeza maarifa.

Source ;Bongo 5

Acheni utani na taaluma za watu jamani,

Haya kwa kuanzia tu, weka matokeo yake ya kidato cha nne hapa na A level.
 
Back
Top Bottom