Enyi mawakili mliomtetea Lulu sidhani kama kazi hiyo mumeifanya kwa moyo wa uzalendo kama hakuna kilicho nyuma ya pazia,kwanini nasema hivyo,wako wengi sana wanapata shida,wanasota kwa kukosa msaada na wana kesi kama hiyo ya Lulu kuna matabaka ya watu hapa Tanzania ambao wako juu ya sheria,tumeona mfano wa Lulu na Ditopile wao kesi zao zimeshughulikiwa kwa haraka na suluhisho kupatikana wakati wako watu ambao wanayo zaidi ya miaka 5 hawana dalili ya kutoka huko gerezani simply hawana fedha au hawana wa kuwasemea kwenye jamii inayotuzunguka,tuna create matabaka kati ya watanzania nna dhambi hiyo haitatuacha itatutafuna sana kwani tayari kuna pengo la walio nacho na wasiokuwa nacho na ambao wako juu ya sheria na walio chini ya sheria ambao kesi zao ni rahisi kubadilishwa kutoka kuua na kuua bila kukusudia sababu wanauwezo,Ole wao masikini na wasiokuwa na kitu Tanzania utakoma