Interlectual capacity, vast knowledge tactically and tentatively , Tanzanian come to concrete, definite and profound conclusion that, We are like Children who are being brought up under tough environment by hard working Dad for our future benefit.
Waheshimwa Wabunge, Mawaziri, Waziri Mkuu na Mh. Rais wanafanya kazi kwa juhudi kubwa kwa manufaa ya Inchi ambayo itaendelea kuepo na wanayoyafanya yatadumu kwa karine nyingi zizajo kwa manufaa ya vizazi vijavyo na pengine kwa mateso ya kizazi cha sasa.
Kinachotutesa wanainchi sasa ni kwa nini kizazi hiki kiteseke kwa kiasi kikubwa kwa maisha mazuri ya kizazi kijacho.
Wanainchi na hasa vijana wanahisi kuwa wanaowaletea matatizo ya kuwa na maisha magumu ni viongozi wao wa Juu. Hili limeanza kuwaletea chuki kwa Wabunge wao.
Viongozi wao wanatumia muda mwingi kuongea mafanikio ya miradi mikubwa ya kitaifa bila kuonyesha mchakato wa kuondoa mateso yao ya kila siku ya kukosa chakula kizuri na cha uhakika, mavazi na mahala pa kulala baada ya kusomeshwa kwa gharama kubwa za wazazi wao na Taifa.
Vijana wanataka maendeleo yawe balanced kati ya vitu na watu.
VItu vinavyoleta mavufaa kwa Vijana ndani ya muda mfupi na directly ndivyo vyenye tija kwao.
Kwa mfano Serikali ikishiriki katika ujenzi wa viwanda vikubwa ambavyo vitaleta ajira kubwa ndani ya muda mfupi ndiyo kitu chenye tija kwao. Miradi ambayo inaongeza kipato cha Taifa kwa ujumla,kumwelezea mtu mwenye njaa ni sawa na kimpigia mbuzi gitaa.
Sisi Wakristo, Yesu Kristo wakati anaelekea kuteswa, aliwaandalia wanafunzi wake karamu ya mwisho na kuwaambia " Twaeni mle wote huu ndiyo mwili wangu utakaotolewa kwa ajili yenu kwa ajili ya maondoleo ya dhambi, ufufuko wa mwili na uzima wa milele ijayo, fanyeni hivi kwa kunikumbuka mimi"
Tumeendelea kumkumbuka Yesu Kristo kwa sababu ya chakula na kinywaji, Yesu kristo hakuwa na nyumba ya kuishi wala kibanda cha chips lakini anaheshimika kwa sababu ya upendo wake kwa watu na kutuachia Amani.
Viongozi wa sasa walisheni na kuwanywesha Watanzania ili wawakumbuke.