Lusinde amvaa Amunike kweupe

Kitaaluma timu ilikuwa imepangwa nzuri.
Sababu zilizotufanya tufungwe.
1. Uwanja mbovu ambao wenyeji walikuwa wanajua namna ya kuutumia.
2. Hatukuwa na bahati. Tulipata nafasi nyingi tukashindwa kuzitumia.
3. Kukosekana kwa Mbwana Samata kulichangia kwa kiasi kikubwa tushindwe kushambulia kwa kutumia mbinu ya kila mchezaji kumtumia mwenzake katika kufunga. Kuna dogo moja alikuwa anacheza namba saba, huyu hajui kabisa kuwa kuna wachezaji wenzake mbele. Akipata mpira yeye ni kuangalia goli liko wapi tu. Msuva alikosa mtu wa kumchezesha na kutengenezea nafasi.
4. Upepo ulivuma sana kipindi cha pili kuelekea goli la Tanzania kiasi cha kusababisha goli kwa sababu mpira ulikuwa na kasi ya ajabu ilipopigwa kona.
Kwa kifupi, kocha wetu bado anahitaji muda ili kujenga kikosi cha kudumu cha Taifa. Anawatumia vijana wengi na wazee wachache ili kuunda timu ambayo itafika mbali baada ya miaka michache ijayo. Hata tukienda AFCON inayokuja, tutakuwa wasindikizaji tu.
Bora tubaki ili tuandae kikosi bora kwa ajili ya AFCON ijayo.
 
Hata ukiwauliza viongozi wa nchi hii kama tatizo ni nini hatufanikiwi kisoka naamini hawana hata majibu
Magamba walikuwa wamejipanda haswa kujitwalia utukufu endapo Stars ingeshinda mechi ya jana lakini Mungu alighairi. Maana hizo sifa ambazo angeimbiwa mh. ingekuwa kero na wapinzani wangetukanwa matusi ya nguoni kwa kukwamisha maendeleo ya soka nchi hii tangu uhuru!
 
Mnachanganya mpira na siasa!!....mmeipeleka timu ikulu na kuharibu sociology ya wachezaji kwa vitisho na amri,mpira haupo hivyo pelekeni jeshi likacheze na Uganda basi kama mpira ni amri!
 
Kwa mara ya Kwanza nampa heko Lusinde
 
NINGEMUOONA WA MAANA KAMA ANGETAKA serikali ianzishe academy kila mkoa na chama chake kiweke nyasi bandia ktk kila kiwanja chake hapo angekuwa mpenzi wa soka vinginevyo ni pumba tuuu. kwani anepitisha bajeti ya michezo ni nani kama sio yeye huku akijuwa miundombinu ya mpira nchi hii ni zero
 
Jamaa ana pointi sana.

Mechi ijayo refa awe Jecha..
 
Hahahaha
 
Tutabadilisha sana makocha huku hatuna mkakati endelevu wa kupata ushindi. Mpaka sasa na kwa muda ambao Amunike amekochi taifa stars sioni justifikation ya kumfaya huyu kocha. Hebu tuone takwimu za performance yake kwanza na kuangalia factors zote zinazisababisha kushinda au kushindwa. Tusisahau mchango wa wachezaji wenyewe katika kushindwa au kushinda!
 
Kuweni na Amani ya Bwana,Taifa Stars itakwenda Cameroon mwakani liwe jua liwe wingu nene.

Cape Verde atamfunga Lesotho mchana peueeeee na sisi tutampiga Uganda Taifaaaaaa

Kama naota vile,laini acha tusubiri maajabu ya Musa hapo Machi mwakani lolote linaweza kutokea tena uzuri michezo yote inachezwa wakati mmoja,hakuna kupanga matokeoooooo
 
Kikosi cha Jana do kilimfunga capevede,hamkusema picha hafai, ila kufungwa jana tu bas hafai,capevede wao niviwete?
 
Amunike ndie alikuwa ana cheza?? Wachezaji wanatakiwa wachapwe bakora
 
Academy mbona zipo nyingi tu.Je zinatiliwa maanani?Walimu wenye vigezo vya kitaalamu wapo.Je wanapata sapoti?Tff inatakiwa kusapoti na siyo kumiliki Academy.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…