Kitaaluma timu ilikuwa imepangwa nzuri.
Sababu zilizotufanya tufungwe.
1. Uwanja mbovu ambao wenyeji walikuwa wanajua namna ya kuutumia.
2. Hatukuwa na bahati. Tulipata nafasi nyingi tukashindwa kuzitumia.
3. Kukosekana kwa Mbwana Samata kulichangia kwa kiasi kikubwa tushindwe kushambulia kwa kutumia mbinu ya kila mchezaji kumtumia mwenzake katika kufunga. Kuna dogo moja alikuwa anacheza namba saba, huyu hajui kabisa kuwa kuna wachezaji wenzake mbele. Akipata mpira yeye ni kuangalia goli liko wapi tu. Msuva alikosa mtu wa kumchezesha na kutengenezea nafasi.
4. Upepo ulivuma sana kipindi cha pili kuelekea goli la Tanzania kiasi cha kusababisha goli kwa sababu mpira ulikuwa na kasi ya ajabu ilipopigwa kona.
Kwa kifupi, kocha wetu bado anahitaji muda ili kujenga kikosi cha kudumu cha Taifa. Anawatumia vijana wengi na wazee wachache ili kuunda timu ambayo itafika mbali baada ya miaka michache ijayo. Hata tukienda AFCON inayokuja, tutakuwa wasindikizaji tu.
Bora tubaki ili tuandae kikosi bora kwa ajili ya AFCON ijayo.