Mbunge wa Mtera(CCM),Livingstone Lusinde ameitaka TFF kuandaa barua ya kumfuta kazi kocha wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike ili akishuka tu uwanja wa ndege akabidhiwe.Lusinde ametoa kauli hiyo kufuatia Taifa Stars kulala bao 1-0 dhidi ya Lesotho mjini Maseru na kujiweka kwenye mazingira magumu ya kufuzu Afcon 2019 nchini Cameroon.
"Hii serikali INA mawaziri wanaotumbuliwa wakikosea tu kidogo,sasa huyu kocha anazoa wachezaji na kuwapanga anavyotaka yeye halafu tumwache.Namwomba Waziri Mwakyembe awaandikie TFF akiwa huko ili wavunje nae mkataba haraka" amedai Lusinde.
Lusinde alidai pia sifa ya Amunike in nidhamu ambayo wachezaji wanaweza wakafundishwa hata jeshini lakini sio suala la soka ambalo amedai limemshinda.
Lusinde pia amedai kuwa Amunike amekuwa na upendeleo katika upangaji wa kikosi na badala yake anapanga watu kwa kuangalia matakwa ya wapenzi na sio kitaalamu