Waziri wa Zamani wa Mambo ya Ndani Augustine Lyatonga Mrema, amelaani vikali zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa lilivyoendeshwa, huku akitolea mfano maofisa aliowashuhudia yeye mwenyewe wakisubiri watu mtaani na kuwapigisha kura.
Mrema anasema hajawahi kushuhudia uchafu kama huo, na akasema kama kweli sisi kama nchi tumefikia hapa basi anaweza kuacha siasa kabida maana haya ni mambo ya ajabu sana kutokea nchini.
Mrema aliyedai kuwa aliamua kushirili uchaguzi kama njia ya kumuunga mkono rais dhidi ya waliosusia, anasema ameshangazwa mno na jinsi zoezi lilivyoendeshwa, na ameonakana kukerwa mno na zoezi hilo.
Kwa kweli serikali, ikae, ijitafakari ione Je kwa mambo haya ya kuvuruga haki ya wananchi kupata viongozi wao halali ni heshima kwao kama viongozi wa nchi?
Ni aibu sana kwa viongozi kuvuruga mazoezi ambayo kupitia mazoezi ya aina hiyohiyo wao waliweza kuingia madarakani. Hii ni aibu ya karne kwa serikali, Ni aibu ya karne kwa chama cha Mapinduzi.