M-wekeza kutoka Vodacom Riba 13%

M-wekeza kutoka Vodacom Riba 13%

Kidagaa kimemwozea

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2018
Posts
3,680
Reaction score
6,554
Kampuni ya vodacom &Sanlam imeanzisha mfuko wa uwekezaji ambapo mwekezaji atapata faida 13% kwa mwaka .

M-wekeza ni huduma inayomuwezesha mteja wa M-Pesa kuwekeza kima cha chini kabisa kuanzia TZS 1000 na zaidi kutoka M-Pesa na kupata faida nzuri bila gharama ya ziada.

Wateja wote wa M-Pesa wanaweza kujiunga na kusajili Akaunti za M-wekeza na kuanza kuwekeza Unachotakiwa kufanya ni kupiga *150*00#>Huduma za Kifedha>M-wekeza.

M-wekeza ni huduma ya kidigitali inayorahisha uwekezaji kiganjani mwako bila gharama za ziada.

Pia kupitia M-Wekeza mteja anaweza kuwekeza Kiwango chochote na kupata faida mpaka 13% endapo atawekeza fedha zake kwa mwaka mzima na unaweza pata taarifa ya kifedha ya uwekezaji wako muda wowote kiganjani mwako.

MAELEZO YA KINA

M-WEKEZA ni huduma inayomuwezesha Mteja wa M-Pesa kuwekeza kima cha chini kabisa kuanzia TZS 1000 na zaidi kutoka M-Pesa na kupata faida nzuri bila gharama ya ziada. M-WEKEZA inaweza kutumika na wateja wote wa M-Pesa wenye lengo la kuwekeza na kupata faida baada ya muda fulani. Kujiunga mteja utapiga *150*00# >Huduma za Kifedha>M-WEKEZA, faida za huduma hii M-WEKEZA ni huduma ya kidigitali inayorahisha uwekezaji kiganjani mwako bila gharama za ziada.
Pia kupitia M-Wekeza mteja anaweza kuwekeza Kiwango chochote na kupata faida mpaka 13% endapo atawekeza fedha zake kwa mwaka mzima na unaweza pata taarifa ya kifedha ya uwekezaji wako muda wowote kiganjani mwako.
Wateja wote wanaweza kufungua akaunti ya kuwekeza kwa ajili yako au kwa niaba ya rafiki mwenye namba ya Vodacom na mtumiaji wa M-Pesa. Hakuna makato yoyote ya mwezi au siku kwenye akaunti yako ya uwekezaji. Unaweza kuhamisha kiasi cha fedha au vipande kwenda kwenye akaunti nyingine ya rafiki bila makato ya ziada kupitia menyu ya M-WEKEZA. Fahamu kuwa wateja wote wana uwezo wa kupata taarifa ya kifedha muda wowote zinazoonesha , jumla ya pesa uliyowekeza, kiasi kilichopo ( Faida na Uwekezaji), taarifa za akaunti na kiasi kilichotoka na kuingia kwenye akaunti yako ya M-WEKEZA. Ahsante^JM
 
Bora nianzishe kausha damu ntajua nitakavyo pambana na BOT
Screenshot_20241121-172945.png
 
Back
Top Bottom