Kwanini sio kila mwezi uwe mwaka?Kampuni ya vodacom imeanzisha mfuko wa uwekezaji ambapo mwekezaji atapata faida 13% kwa mwaka .
M-wekeza ni huduma inayomuwezesha mteja wa M-Pesa kuwekeza kima cha chini kabisa kuanzia TZS 1000 na zaidi kutoka M-Pesa na kupata faida nzuri bila gharama ya ziada.
Wateja wote wa M-Pesa wanaweza kujiunga na kusajili Akaunti za M-wekeza na kuanza kuwekeza Unachotakiwa kufanya ni kupiga *150*00#>Huduma za Kifedha>M-wekeza.
M-wekeza ni huduma ya kidigitali inayorahisha uwekezaji kiganjani mwako bila gharama za ziada.
Pia kupitia M-Wekeza mteja anaweza kuwekeza Kiwango chochote na kupata faida mpaka 13% endapo atawekeza fedha zake kwa mwaka mzima na unaweza pata taarifa ya kifedha ya uwekezaji wako muda wowote kiganjani mwako.^EK