Jeshi la M23, limetembelea kambi ya Mubambiro. Baada ya mazungumzo (hawakuingia kambini, waliishia nje ya kambi). Wanajeshi wa Afrika kusini wameonyesha kuridhia ukarimu wa M23 na kuomba mambo matatu:
1. Kuruhusiwa kwenda Goma, kwa kutumia vifaru, wakakusanye vitu vyao vilivyopo kwenye kambi ya MONUSCO na kukaa navyo walipo kambini hapo.
2. Kuruhusiwa kurudi nyuma walipokuwa na positions za mapigano, wakusanye mabaki ya miili ya wenzao ili isafilishwe kuzikwa nchini kwao.
3. Kuruhusiwa kutumia uwanja wa Goma kusafilisha miili hiyo.
M23 imewaomba kuwasilisha maombi yao hayo kwa maandishi, ili viongozi wakuu wayapitie na wawajibu.
Soma Pia: Jeshi la Afrika Kusini pamoja na FARDC limefanikiwa kuwadhibiti M23 kuelekea GOMA
Pamoja na kutangaza vifo 13, inaonekana wazi Africa Kusini walipoteza wanajeshi zaidi ya idadi iliyotangazwa.
Wakati huo pia, M23 imewachukua waliokuwa wanajeshi wa FARDC na kuwapeleka kambini kwa ajili ya mafunzo ya uzalendo, huku wakiahidiwa kuendelea kulipwa kama wanajeshi, kwa mshahara mpya watakaopangiwa, na badae watakaopenda wataendelea na kazi yao. Upande wa wazalendo, wenyewe watafundishwa mbinu za ujasiliamari na kuruhusiwa kuanzisha maisha mapya uraiani.
Mpaka sasa, M23 imesharejesha umeme mjini Goma, kwa zaidi ya asilimia 75, maji yapo mbioni kusambaa mjini kote baada ya umeme kurudi, na Internet kwa sasa inapatikana,kupitia MTN ya Rwanda, ambapo mtandao kwa sasa unapatikana hadi umbali wa km 10 kutoka mpakani, jambo linalouweka mji mzima wa Goma katika hali ya kuweza kufikiwa na mawasiliano ya uhakika.
Hata hivyo, inasemekana bado mapigano yanaendelea Kivu kasikazini, ambapo lengo la M23 ni kukomboa Kivu kazikasini na kuhakikisha uwanja wa ndege wa Kavumu, jimboni humo, hautumiki.

Video inayoelezea kuhusu mazungumzo ya M23 na wanajeshi wa SADC