Ma brother wa miaka 35+ hebu tupeni wadogo zenu, ushauri wowote wa kuhusu maisha

Ma brother wa miaka 35+ hebu tupeni wadogo zenu, ushauri wowote wa kuhusu maisha

1. Suala la uchumi, aisee chagua Nuru au Giza. Mimi nilichagua Nuru hivyo nimeona mambo yakienda kupitia maombi japo kuna muda utaona ka Mungu amekusahau lkn itakua sauti ya chini moyoni ikisema endelea kuvumilia mi ndimi Mungu wako nitakusaidia.
2. Ishu ya mahusiano, hapa bwana uwe makini ngoma ipo na inaua na wengi wameukwaa. Nina mengi ya kuzungumza hapa ila niseme tu tundu utakaloingiza hakikisha mahali hapo umepima h.i.v au umevaa salama.
tuendelee mkuu, maana uli sema una mengi ya kuzungumzia.
 
Ukali wa wembe hauwezi kupasua kuni wala shoka kunyoa nywele” lengo la ujumbe huu ilikuwa ni kunusuru ndoa zetu! Maana ukiisha ingiza haki sawa kwenye ndoa kwisha habari yako! Kinachoongoza ndoa ni utii na akili basi. Yaani mwanamke aishi na mume wake kwa utii na mwanaume aishi na mke wake kwa akili. Yaani kwa tafasiri ya haraka ni kwamba kama hauna akili usioe na kama hauna utii usiolewe! Huo ndiyo ukweli na ukiamua kuupuza subiri kushughulikiwa maana ukweli siku zote huwashughulikia wanaoupuuza!
 
1. Usioe bila kuwa na uhakika wa Pesa ya kumlisha mkeo
2. Tafuta sana pesa kadri uwezavyo. Dunia haina huruma kwa maskini. Na uta heshimiwa kwa mali/pesa unazomiliki
3. Kuwa na kiasi kwenye maisha yako
4. Ukimwi upo na unaua.
5. Usiamini sana watu
Madini🫡 nawaona wawekezaji wakisogea
 
-kama umeoa hakikisha mkeo
hakushikii akili yko.
-usijenge wala kununuwa kiwanja ukweni.
-Usijenge kwenye kiwanja Cha mkeo.
-usijenge kwenye kiwanja cha urithi kama mmezaliwa wengi.
-Tafuta maisha Kwa bidii ukiwa bado upo under 30 umri,kadiri unavyokuwa mtu mzima ndy majukumu yanaongezeka.
-ifikirie zaidi kesho yako kuliko Leo.
-jikite sana kwenye kununuwa mashamba na viwanja hakika ndy pension yako ya uzeeni .
-usihangaike na mtu ambaye ahangaiki na wewe.
- tamaa mbele mauti nyuma,ogopa cha mtu.
 
Back
Top Bottom