Ma-jobless thread

Tukiacha utani hakuna kitu kinaumiza kama kuamka asubuhi huna kazi ya maana unaumiza kichwa ufanye nini upate hata hela ya kuishi, maisha ya kutikua na kazi ni fedheha nyie acheni unaeza kupata dharura huna hata mia mfukoni unaanza kupiga simu hata kama hupendi inabidi tu.
 
Ushauri mzuri sana kwakweli skuizi ujuzi unasaidia sana kuliko ma degree tulokua nayo hayana faida.
 
kwema majoblesi wenzangu

kwangu mimi mtaa umenichapa balaa ,nimechapika ila sija surrender najua stress na starvation ndio ugonjwa wetu tulio wengi.

kwangu mimi ili kusavaivu nimejiegesha kwenye ka kampuni kamoja kaulinzi hapa kwa jiji la chalamila. ila kutoa ruhusa tu ya kupiga sahili ni mtiti kanazingua balaa

majuzi kati nilikua utumishi kupiga pepa ,yule msimamizi itabidi afunguke tu hvii ww kwenye hii picha ndio wewe mfwende?

wanangu najua wapo walio give up,wapo wenye ahueni, tupo wengine tunaozidi kwenda ila imani ndio nguzo zetu. ni seme tu majoblesi MUNGU asimame na sisi daima kwenye msoto huu tunaopitia.
 
Liman Charlie acha tuendelee kukaza wakati wetu utafika tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…