Ma-TO walipofunikwa na Sylivester Mwageni (True mathematician)

Umesema point mkuu chukuwa like oyoo...
 
mm mwenyew TO ila mvivu kusoma
 
Umeongea ukweli mtupu.Kuwa kuna watu Wana uwezo mkubwa sema mambo mengi Na hawataki kujitaabisha.Hata mie naamini O level Ningejitaabisha vya kutosha huenda ningepata kijiti cha Single Digit.
Ila ndiyo hivyo,mara kuandika Barua kwa mademu,mara kuwaza ifike siku ya mpira ukacheze.Unasoma kwa kugusa gusa tu.
Darasani kwetu aliyetuburuza O level Na aliingia Top Ten jamaa alikuwa anasoma balaa Na hapotezi muda japo pia kichwa chake kilikuwa kimebarikiwa maana alikuwa anajua vitu vingi kasoro kucheza mpira ndio ilikuwa shida..
Ila mambo ya kucheza Piano,kujua lugha (English,kiitaliano,French Na akaanza kujifunza kijerumani ) haikuwa tatizo kwake.

Ila tukubali pia wengine hata wasome vipi wataishia kupata marks Za kawaida.Kuna washikaji nawajua wazee wa kubundi.Wanasoma mpaka unawaonea huruma lkn mwisho wa siku wanapata marks Za kawaida tu Na wengine nusura combinations zigome.
Msuli tembo mafanikio Sisimizi
 
Bila kusoma Top Ten huingiii mkuu,wafuatilie vizuri ratiba zao waliowahi kuingia Top Ten utagundua licha ya vipaji vyao walikuwa smart katika kusoma.
Hawa jamaa wamebarikiwa wakisoma kidogo Na wakielekezwa wanaelewa haraka plus msuli wa kusoma ndio hapo wanaiingia Top Ten.
 
Mbali na uTO wapo wapi na wanafanya nn kupitia ugenius wao au ndo imebaki story tu za uTO???
Kuna mshikaji aliingia Top Ten O level,Akaenda Mzumbe,Advance hakuwepo Top Ten Japo alifanya vizuri.Jamaa alikuwa na Interest Na Computer Toka kitambo alisema naenda Kusoma Computer Science UDSM .Alifanya hivyo.Alivyomaliza Chuo alifanyafanya kazi kidogo chuo wakati watu wanahangaika Na Ajira ye akasema siwezi Tunis maarifa yangu kiasi hiki halafu nikaendelea kulipwa hela kiduchu.Jamaa akaacha kazi chuo akasema staki tena kuajiriwa.Mpaka Leo namuona tu mtaani sijui hata ishu anayofanya Ila naona jamaa maisha yanamuendea vizuri mambo ni mazuri kwelikweli.Kamuachisha kazi mke wake alikuwa mikoa ya mbali huko.Jamaa hii Dunia anazunguka kama Mimi ninavyotumia 650 kwenye mwendokasi
 
Mbali na uTO wapo wapi na wanafanya nn kupitia ugenius wao au ndo imebaki story tu za uTO???
Kuna MaTO wengine wa Nyanja nyingine kama akina Bakhresa.

By the way unataka maTO wafanye nini wakati hakuna tena Madesa ya kubukua/Kukremu? TO mpe Desa atakuonyesha ye ni Nani.Kusema afanye something special hiyo ni another case.

We hujawahi ona kwenye Shule za mchepuo wa Sayansi Na Sanaa watu wanaokuwaga watundu wa utundu wa ufundi Huwa ni wa Arts? Unakuta shule ina wanafunzi wa Arts Na Science lkn wachawi wa vitu vya Electronics ni from arts?
 
Ndo ilivyo hivyo OT mwisho wake huwa ni tofauti sana na matarajio ya wengi wachache sana wanapita njia ile ile waliyoanza nayo
 
Nilichelewa sana kujijua kuwa kamwe nisingekaa niwe genius.
Ila nilivyokutanaga na vichwa kama hivi, niliishia kushukuru Mungu kwa pumzi aliyonipa na kuacha kabisa kuota kupiku njemba hizi.

Umenikumbusha mbaali sana.
 
2006 t.o
 
Nilichelewa sana kujijua kuwa kamwe nisingekaa niwe genius.
Ila nilivyokutanaga na vichwa kama hivi, niliishia kushukuru Mungu kwa pumzi aliyonipa na kuacha kabisa kuota kupiku njemba hizi.

Umenikumbusha mbaali sana.
tupe story kidogo mkuu, it seems that you have something to share with us..
 
Story nzuri sana,Yaani tuliosoma kipindi icho tunaelewa namna hali ilivyokua, sihaba wengine hatujawa pata div one kabisa, no two mwanzo mwisho lakini tumekua tunaishi ndoto zetu. ..pongezi kwa hao vijana nilikua nikiona wanavyong'aa kwenye mbao za matangazo sana...
 

yeah ni kweli, kuna wengine uwezo wao wa kiakili ni mdogo hata wasome vipi, labda Mungu aingilie kati Super Sub Steve
 

hao ma T.O unaosema hawakuwa wasomaji kivile, labda wakati wanasoma ww haupo, au walikudanganya kuwa hawasomi ili uwaone ma-genius, necta bila kusoma sana huwezi pata div 1 ya single digit asilani Complex
 
hao ma T.O unaosema hawakuwa wasomaji kivile, labda wakati wanasoma ww haupo, au walikudanganya kuwa hawasomi ili uwaone ma-genius, necta bila kusoma sana huwezi pata div 1 ya single digit asilani Complex

Mzee nilichokiongea hapo juu ni kwamba kuna mtu hapo juu anawaaminisha watu kwamba kwa yeyote yule anayesoma anaweza kuwa TO na kuwa Ma TO si lolote si chochote na kwamba kusoma kwao ndo kunawafanya wawe maTO. Na by the way how usijue ratiba ya mtu ya kusoma na mtu unasoma naye darasa moja na unakaa naye cube moja.? My friend, nimepata bahati ya kuwa nao karibu baadhi ya hawa watu. Neno moja tuu ninaloweza sema ni kwamba, pamoja na kusoma hawa watu wanasomething special. Kusoma tuu pekee hakuwezi kukufanya uwe T.O ingawaje ni one of the variable katika equation.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…