Maadhimisho ya miaka 100 ya Shule ya Sekondari ya Old Moshi. Tukutane Wahandisi tuliosoma hapo

Shule inaitwa MOSHI SEKONDARI, ukarabati kwenye zile shule kongwe zilizokarabatiwa sidhani kama hii iliachwa I hope itakaua ilikarabatiwa.

Mazingira ya shule hii ni mzuri Ila nilishangaa majengo yake na ramani yake inafanana Na Same Sekondari.
 
Kwahyo Hali unayoiyona sashv Ni sawa na ya mwaka 1950 mkuu

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Kuna wakati ukienda Muhimbili wote wametoka Old Moshi (PCB) na COET ni kutoka Old Moshi (PCM). Kilichokuwa kinasaidia ni KUBUNDI na ndama kumletea Uji na chakula ng'ombe! Hiyo ni miaka ya 1973! Moshi Sec we acha tu
 
Nimekaa siti ya mbele kabisa hapa toka dormitory ya Mawenzi 1.

PCB CLASS lenye chata lake "Msitu ule ule ila nyani ni wapya" Nimesoma hapo 2012-2014.

Zikianza mvua zikianza tope lake pale lilikuwa sio poa bwenini inakuwa marufuku kuingia na viatu.
 
Kumbe kinunda wa zamani hivo...katupigia mathematics 2008-2010 pcm
 
Wengi aliopita pale Ni mainjinia

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
My young brother pia amepiga Advance pale, amegraduate pale 2005,now yuko Shanghai na Ph'D ya pharmacy anagonga mishe zake, nimemtembelea sana pale miaka hio na kitu ambacho nilikua nacheka kila nikifika pale ni maandish ya ukuta wa getini yaloandikwa OLD MOSHI SECONDARY, ila madogo kwa ununda wao wakaongeza herufi G pale mwanzoni ikawa inasomeka GOLD MOSHI SECONDARY😂😂😂nitamrushia link ili akipenda aje humu achangie chochote.
 

Shikamoo Baba
 
Reactions: EEX
Wanafunzi wao siku hizi wanabeba mabegi yao na kwenda kusomea chuo cha ushirika ili waonekane ni wanachuo au kung'oa pisi za chuo...wameendekeza uasherati zaid ya masomo

Borderless school. Nilikua naenda kusoma Library baada ya lunch. Kulikua na utaratibu wa kurudi darasani Kwa lazima mnatozwa 10,000/- .
 
Inachukua wanafunz wenye uhitaj maalumu ila miundombinu wezeshi kwa watoto hao haikidhi mahitaji yao....na hili wakaliangalie

Kuna jamaa ilikua ukiingia tu Kwa sauti za nyayo zako, anakuita jina lako, au ukimshika Mkono anajua Hutu ni flani. Kuna wakati napiga nae stori machozi yananilengalenga, nawaza ambavyo huyu jamaa haoni mnaenda nae kanisani, anasikia tu lakini hajawahi kuona vitu vinafananaje. Mungu amewajalia wale jamaa kwenye utambuzi
 
Hawa huwa Mungu anawapa cha ziada na wanakuwa na uwezo mkubwa sanaa...mm nna rafik yangu huwa kaka yake haoni...ila akichukua computer hata mimi nnaeona kwa macho mawili simfikii hata robo...anaendesha ma NGO'S ya nje huko kupitia online....
 
Nimesoma hapo nikalala Mawenzi 10.

Namkumbuka Mr Msami (PDidy) mkali sana wa Physics...mpole sana na anajua. Sijui yuko wapi.

Alikuwepo babu mmoja mkali wa Pure Maths, mama mmoja mkali wa Chemistry.
Mwl mmoja akiitwa Lisapita.
Old Moshi My School
 
Nimekumbuka Bangaluu la KIBO 5
 
Sawa Mainjinia mmesaidia vp kuboresha mfumo wa elimu??
 
Nimesoma hapo nikalala Mawenzi 10.

Namkumbuka Mr Msami (PDidy) mkali sana wa Physics...mpole sana na anajua. Sijui yuko wapi.

Alikuwepo babu mmoja mkali wa Pure Maths, mama mmoja mkali wa Chemistry.
Mwl mmoja akiitwa Lisapita.
Old Moshi My School
Yule mama wa Chemistry sijawahi kujua jina lake halisi zaidi ya "Madam Quantum"😀😀
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…