Hali halisi leo tarehe 26 April 2024 kutoka uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Tanzania katika Maadhimisho ya miaka 60 ya toka Muungano wa kidugu kuasisiwa kisheria baina ya nchi mbili za kiafrika za Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu Wa Zanzibar
Tukumbuke kuwa mahusiano ya mataifa haya mawili yalianza kabla ya mwaka 1964 ambapo kwa miongo mingi raia wa pande hizo mbili walishirikiana kiuchumi, kielimu kidini na burudani bila vikwazo vyovyote.
Watu kutoka Tanganyika walikwenda soma katika skuli za elimu ya juu enzi hizo zinapatikana Zanzibar tu, kutoka sehemu mbalimbali za Tanganyika mfano mkoa wa Tanga uliokuwa na shule kongwe za mwanzo lakini hazikuwa na madarasa ya juu hivyo baadhi yao kulazimika kuvuka na kwenda Zanzibar kumalizia elimu zao za sekondari.
Upande wa biashara, Zanzibar ilikuwa kitovu cha majahazi kuleta mali kutoka bara Arabuni na India pamoja na ulaya hivyo wafanyabiashara wa kutoka Tanganyika walimiminika kutafuta bidhaa hizo Zanzibar.
Zao la karafuu na mbata (nazi)wakati wa msimu wa mavuno mashambani Pemba na Zanzibar yalihitaji mikono mingi ya wavunaji, wakwezi na wafua nazi na kulazimu kupata mikono hiyo kutoka Tanganyika ya usukumani na unyamwezi hivyo waTanganyika hao kupata ajira za muda za ujira wa kukimu maisha yao na familia.
Mahusiano mengi kama Zanzibar kuwa daraja la kupeleka imani ngeni za kuja kwa majahazi na merikebu, kwanza zilitupa nanga Zanzibar kuongea na wajuvi wa safari za ndani ndani Tanganyika watafikaje. Ndipo ndugu zetu wa Zanzibar wakaaaongoza maalimu na baadaye wamisionari kueneza imani za dini.
Mambo ni mengi na miaka mingi baadaye wanasiasa wakaona muingiliano huu wa kiuchumi, kielimu na kijamii tayari umeweka kila kitu sawa hivyo ni heri kufanya mambo kisheria na hivyo kusiliba muungano huu usio rasmi unaotambulika kwa kuutia ndani ya karatasi ya mkataba kuwa Muungano rasmi mwaka 1964.
Hivyo Julius Nyerere na mwenzie Mzee Abeid Karume wakaona wafanye mambo kiusasa na Muungano wa wananchi hawa wa karne kibao kuwekwa katika utambulisho wa Muungano kikatiba kuhitimisha walichoanzisha wananchi wenyewe kwa miaka mingi.
Leo katika historia April 7: Undani wa hayati abeid amani karume kuzaliwa mpaka kifo Bwana Abeid Amani Karume muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar alizaliwa katika kitongoji cha Pongwe, Mudiria ya Mwera kisiwani Unguja tarehe 4 Agosti 1905. Karume ni mtoto wa kwanza kuzaliwa katika familia ya...