Maadhimisho ya Uhuru wa Tanganyika, na nafasi ya Kanisa Katoliki

Maadhimisho ya Uhuru wa Tanganyika, na nafasi ya Kanisa Katoliki

Wakatoliki wamesomesha kina Mkapa, Kahama, Kazaura na wazazi wetu katika shule zao na hao waliosomeshwa ndio waliokuja kuwa wataalam wa kwanza baada ya Tanzania kuwa huru.

Kupigania uhuru sio lazima mtu ampikie chakula Mwalimu Nyerere ndipo eti awe anafaa kuitwa mpigania uhuru.
Kupikia mtu na kusomesha yote hayana uhusiano moja kwa moja na kudai uhuru
 
Kusomesha hata Agha Khan amesomesha
 
Usikariri mambo. Vatican imejitoa kuendesha makanisa na shughuli zote zenye kumilikiwa na kanisa katoliki tangu miaka ya 2000 mwanzoni.

Ndio maana kila mwaka kanisa limeanzisha utaratibu wa harambee maalum inayoitwa mavuno.

Tarehe ya mavuno inapangwa na parokia husika ingawa mara nyingi makanisa yote hupanga tarwhe za mwisho wa Novemba au Desemba mwanzoni.
Unataka kusema sasa pesa haziendi Vatican siyo? zinatumika hapahapa.kama ni kweli ni jambo la kushukuru pesa na kodi za wa Tanzania zitumike hapahapa.
 
Kupikia mtu na kusomesha yote hayana uhusiano moja kwa moja na kudai uhuru
Nyerere asingesomeshwa na wazungu mimi na wewe tungemjua? asingekuwa na elimu ya Tabora nani angemjua?.

Mkapa asingesomeshwa kule Ndanda mimi na wewe tungemjua?. Acheni siasa zenye kuficha udini ndani yake.

Kahama, Kazaura, Kikenya na wazee wengi wa kaskazini waliosomea shule za wakatoliki kama wasingesoma nchi hii ingekuwa na wataalam awamu ile ya kwanza?.

Unajenga hoja nyepesi kwamba kanisa katoliki halikuwa na msaada kwa kupatikana uhuru wetu huku mkisahau maelfu ya waliosomeshwa enzi hizo ambao baadae mchango wao kwa taifa hili ni mkubwa tu.

Sisi hatukupigana kwa maana ya kuingia misituni nchi yetu iliwekwa kwenye udhamini wa Muingereza hivyo hakuhitaji hata kutumia sindano katika kutuachia uhuru wetu.
 
Kusomesha hata Agha Khan amesomesha
Ndio mtulize vichwa muachane na siasa za chuki dhidi ya ukatoliki na ukristo kwa ujumla.

Halafu unasahau kuwa uislamu uliambatana na mababu zetu kuvalishwa minyororo shingoni kutoka Kigoma mpaka mikoa ya Pwani.

Ukiishi kwa kinyongo cha nini kilitokea miaka iliyopita utakosa ujasiri wa kuitazama kesho na keshokutwa.
 
Unataka kusema sasa pesa haziendi Vatican siyo? zinatumika hapahapa.kama ni kweli ni jambo la kushukuru pesa na kodi za wa Tanzania zitumike hapahapa.
Vatican hawashughuliki tena na masuala ya ndani ya ukatoliki wa Tanzania, tunajitegemea kwani sisi ni watu wa maendeleo.

Popote utakapokuta ukatoliki upo utakuta kuna mahospitali, kuna shule za msingi na sekondari, utakuta uwepo wa maisha chanya, huwa tunaendeleza mahali tunapohamia.
 
HOVYO KABISA kanisa lenyewe ni mkoloni iweje ajitoe mwenyewe
 
Waliosoma historia vizuri wanaelewa nafasi ya KANISA katika kueneza UKOLONI. Makanisa yalikuwa ni makazi ya mawakala wa Ukoloni kwa mgongo wa WAPELELEZI, WAFANYABIASHARA NA WAGUNDUZI. Pia kanisa bado likafanya jitihada za kuondolewa kwa biashara ya UTUMWA.
 
Vatican hawashughuliki tena na masuala ya ndani ya ukatoliki wa Tanzania, tunajitegemea kwani sisi ni watu wa maendeleo.

Popote utakapokuta ukatoliki upo utakuta kuna mahospitali, kuna shule za msingi na sekondari, utakuta uwepo wa maisha chanya, huwa tunaendeleza mahali tunapohamia.
Tatizo siyo uwekezaji kama kuwekeza hata wakoloni waliwekeza kwenye shule,afya,miundombinu nk,tatizo nani anafaidika kwa gharama za nani? Na kwa malengo gani?
 
Nazungumzia faida inayopatikana kwenye uwekezaji? Hayo ya vizazi kufaidika hata shule za private wanaweza kusema hivyo hivyo lakini faida inakwenda wenye umiliki
Faida ya uwekezaji inakwenda kwa uongozi wa kanisa katoliki Tanzania. Hayo mawazo yako kwamba miradi yote ya kikatoliki inapeleka faida nje ya nchi ni mawazo yaliyopitwa na wakati yaondoe kichwani mwako.

Nimekwambia kuwa tangu mwanzoni mwa miaka ya 2000 Vatican haichukui chochote kutoka nchi nyingi za dunia hii.

Kanisa linajiendesha kwa pesa ya mavuno na sadaka za kila misa.

Mfano mavuno ya Saint Joseph posta ya zamani mwaka huu zimekusanywa milioni 200 na zaidi kidogo. Sijaongelea Saint Peters na parokia nyingine kubwa za Mbezi Beach.
 
Hakizungumzii mapambano dhidi ya ukoloni bali wakoloni kutawala Tanganyika kupitia dini kama hivi sasa,leo askofu kwenda dodoma toka Shinyanga anateuliwa na Baba mtakatifu vatican,Hospitali kama yetu ya Bugando ina ruzuku,hailipi kodi,wafanyakazi wanalipwa na Serikali bado ni ghali,hiyo super profit nani wanachukua? Ni paskali,Pengo au zinaenda Vaticagn? Haishangazi kanisa katoliki ni tajiri zaidi duniani lakini pia haliwajibiki kwa yoyote! Pascal Mayalla
Ngoja nikupe shule kuhusiana na hospitali ya bugando na hospitali zingine za Makanisa zinazoitwa hospitali teule.
Mfumo huu umeanza Ktk awamu ya nne kuimarisha PPP yaan public private partinership ubia baina ya serikali na mashirika binafsi ktk kutoa huduma
Serikali haikua na hospitali ya rufaa ya kanda ya ziwa. Wakaona gharama kubwa sana kujenga hospital wakaamua kuingia ubia na kanisa bamboo 60% ya staff wanalipwa na serikal
 
Na faida wanagawana vipi? Na Cag anakagua share za serikali?
 
Na faida wanagawana vipi? Na Cag anakagua share za serikali?
Hospitali sio sehemu ya biashara kupata faida bali ni sehemu ya kutoa huduma kwa jamii. Serikali inatoa basket fund kwa ajili ya kuongezea Dawa na vifaa tiba, pia serikali inalipa mishahara ya watumishi 60%. Gharama za matibabu ukifuata utaratibu wa rufaa hauna tofauti na Muhimbili ila ukienda bila kufuata mfumo wa rufaa unachajiwa kiwango ch juu kwa maana kua serikali haijakuchangia hiyo ipo mpaka Muhimbili. Hospitali ya bugando ki hadhi ni zaidi ya Agha Khani lakini jaribu kulinganisha bei za Agha Khani na Bugando. mfano Agha Khani kujifungua mama mjamzito kwa kawaida ni milion 1 na nusu. wakati Bugando ni elfu 70.
Faida inaenda wapi
Hapo zamani hospitali za makanisa ziliendeshwa kwa misaada kutoka nje. tuliotibiwa enzi hizo tulikua tunapata dawa bure mpaka lishe. na kuna wakati tulipewa mpaka nguo tulipokua tunaenda kutibiwa
Kwa sasa hakuna misaada tena kutoka nje, kipato wanachokipata ndo wanakitumia kwa ajili ya kuwalipa wafanyakazi 40%. kununua dawa na vifaa tiba, kufanya ukarabati wa majengo, magari na miundo mbinu yote ya hospitali. Kulipa bills za maji, umeme, licenses nk
Kulipa bills za wagonjwa wa msamaha kuna wanaoshindwa kulipa bills watibiwapo hospitali inaingia risk kulipa.

NB
Kufanya kazi na serikali kuna changamoto kubwa sana. Mnakubaliana kua kila quarter wataleta basket fund mfano milion 150. zinapita mpaka quarter 3 haijaleta hata cent. unajiuliza wale wagonjwa wanaotibiwa bure kwa utaratibu wa serikali ambao wanakua coverd kwa hiyo basket fund ktk hizi quarter 3 ni nani aliyegharamia hizo gharama?
 
Hakizungumzii mapambano dhidi ya ukoloni bali wakoloni kutawala Tanganyika kupitia dini kama hivi sasa,leo askofu kwenda dodoma toka Shinyanga anateuliwa na Baba mtakatifu vatican,Hospitali kama yetu ya Bugando ina ruzuku,hailipi kodi,wafanyakazi wanalipwa na Serikali bado ni ghali,hiyo super profit nani wanachukua? Ni paskali,Pengo au zinaenda Vatican? Haishangazi kanisa katoliki ni tajiri zaidi duniani lakini pia haliwajibiki kwa yoyote! Pascal Mayalla
Linawajibika kwa Kristu pekee aliyelianzisha ...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom