Maadili tunayoyaamini yanatokana na kitu gani?

Maadili tunayoyaamini yanatokana na kitu gani?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Kwenye jamii zetu unaona kabisa Kuna mifumo mbalimbali inayotumiwa kutunza kitu kinachoitwa maadili.

Lakini ili hayo maadili yawe maadili, chanzo chake huwa ni nini hasa.

Kwa nini watu washangae mtu kuwa na mahusiano na baba/mama yake au kaka/dada yake?

Kwani Baba, mama, kaka au dada, si wanawake au wanaume kama wengine? Kwa nini watu waone kama ni kinyume cha maadili?

Hivi mtu akiiba kitu kwa nini ionekane ni kinyume cha maadili. Hivi wizi si uwezo wa kuchukua kitu cha mwingine kwa kumzidi akili?

Hivi chanzo cha kuwepo kwa haya maadili ni nini. Na haya maadili yalianzaje anzaje?

CC: Kiranga , Infropreneur
 
Chanzo cha maadili ni common sense tu.

Binadamu yeyote mwenye ufahamu na utimamu automatically lazima awe na utambuzi wa mambo ambayo yeye mwenyewe hataki afanyiwe na mtu yeyote yule.

Vivyo hivyo, Mambo hayo ambayo wewe binafsi hutaki kufanyiwa, Hupaswi kumfanyia mwenzako. Na Ndio maadili hayo.

Hebu fikiria binti yako anakuja na kukwambia "Baba njoo tusex wote" Yani hapa automatically ufahamu wako uta react kwa hasira kali sana. Kwamba hilo jambo si la kawaida.

Ni kinyume na utambuzi wako wa kifikra kulala na mwanao, binti yako. Yani common sense tu itakufanya u react vibaya mno kukemea hicho kitendo. Labda kama dishi lako liwe limeyumba ndio utakubali kufanya hivyo.

Na hapa ndipo chanzo cha maadili huanzia. Through common sense tu.

Kitu ambacho wewe hutaki kufanyiwa, Huwezi kumfanyia mwenzako.

Na mambo hayo ndio maadili.
 
Kwa ivo "Common sense" ili zi- react mwanao akitaka kungonoka na wewe ufahamu wako hukumbushwa nini kuwa si sahihi baba kungonoka na Binti yake?

Na hiyo "common sense" Iko wapi? Kwenye Akili, roho, nafsi au Inapatikanaje?
 
Kwenye jamii zetu unaona kabisa Kuna mifumo mbalimbali inayotumiwa kutunza kitu kinachoitwa maadili.

Lakini ili hayo maadili yawe maadili, chanzo chake huwa ni nini hasa.

Kwa nini watu washangae mtu kuwa na mahusiano na baba/mama yake au kaka/dada yake?

Kwani Baba, mama, kaka au dada, si wanawake au wanaume kama wengine? Kwa nini watu waone kama ni kinyume cha maadili?

Hivi mtu akiiba kitu kwa nini ionekane ni kinyume cha maadili. Hivi wizi si uwezo wa kuchukua kitu cha mwingine kwa kumzidi akili?

Hivi chanzo cha kuwepo kwa haya maadili ni nini. Na haya maadili yalianzaje anzaje?

CC: Kiranga , Infropreneur
Maadili Huwa ni utaratibu wa maisha ambayo watu wa jamii Fulani wamejiwekea kutokana na Imani zao au mienendo Yao.

Maadili hupangwa na watu kama ambavyo watu walikaa wakaandika katiba, tunataka katika jamii yetu tuishi kwa mtindo huu na huu, nini tunataka na nini hatutaki, kama ambavyo nyumbani pengine uliwahi kuambiwa.

"Kurudi hapa kwangu mwisho saa 12" ni utaratibu ambao baba au mama Yako waliuweka na huna budi kuufata.

Maadili pia yaliletwa na dini. Dini zilikuja na sheria na taratibu zake mbalimbali, ukiwa muumini wa dini hiyo basi huna budi kufata sheria na kanuni zilizowekwa, ndipo tukajikuta tunapata maadili.

Mfano: Uislamu na Ukristo unakataza kuoa dada, mama Yako. Ni kinyume na utu wa mtu.

Waumini wa Imani hizi wakiwa wengi na kujaza jamii unakuta zinakuwa sheria na zinaingizwa katika maadili ya jamii husika, na ukienda kinyume umeenda kinyume na maadili.

Kwa jinsi ninavyoelewa mimi maadili.
 
Kwa ivo "Common sense" ili zi- react mwanao akitaka kungonoka na wewe ufahamu wako hukumbushwa nini kuwa si sahihi baba kungonoka na Binti yake?
Ufahamu una operate wenyewe automatically.

Hatuwezi kujua tusivyo vijua ila tunaendelea kupunguza tusivyo vijua

Maana hata sisi binadamu kuna vitu bado hatuvijui kuhusu huu huu ufahamu wetu jinsi unavyo operate.

Tanatumia ufahamu wetu kuchunguza ufahamu wetu tena ili kuujua kiundani zaidi.

Maana kuna vitu hatuvijui bado kutuhusu sisi wenyewe.

Mfano, Bado hatujui kitu gani kinatufanya tusahau vitu?

Bado hatujui kitu gani hutufanya tukumbuke kitu, tulichokuwa tumekisahau.

Yani tunashtukia tu, ufahamu wetu una ji operate wenyewe automatically bila hata ridhaa yetu.

Yani unashtukia tu umesahau kitu, Halafu ghafla umekumbuka.

Na process hii hutokea automatically.
Na hiyo "common sense" Iko wapi? Kwenye Akili, roho, nafsi au Inapatikanaje?
Common sense ipo katika ufahamu wetu kwenye vichwa vyetu.

Akili, roho na nafsi yote haya ni majina ya kubuniwa tu. Hayapo katika uhalisia.
 
Maadili Huwa ni utaratibu wa maisha ambayo watu wa jamii Fulani wamejiwekea kutokana na Imani zao au mienendo Yao.
Kwa ivo kwanza kabisa unaamini maadili yanatokana na mambo ya Imani fulani au mwenendo wa jamii husika
Maadili pia yaliletwa na dini. Dini zilikuja na sheria na taratibu zake mbalimbali, ukiwa muumini wa dini hiyo basi huna budi kufata sheria na kanuni zilizowekwa, ndipo tukajikuta tunapata maadili.
Pia maadili chanzo chake ni Imani za kidini.
Mfano: Uislamu na Ukristo unakataza
kuoa dada, mama Yako. Ni kinyume na utu wa mtu.
Makatazi ya dini ya Kikristo na Kiislamu ndiyo huleta maadili?

Kwa maelezo yako wewe inaonekana hukubaliani na hoja ya Infropreneur kuwa maadili hutokezwa na "Common sense" tu.
 
Infropreneur Kwa mfano kuwe na mtu/watu wanaoona ni sawa Wanandugu kungonoka. Sasa Hawa jamii ifanye nini dhidi Yao?

Yaani waachiwe familia Moja waoane wenyewe Kwa wenyewe ama nini kifanyike ili common sense zao zizinduke kujua baba au mama na mtoto haifai kungonoka?
 
Kwa ivo kwanza kabisa unaamini maadili yanatokana na mambo ya Imani fulani au mwenendo wa jamii husika

Pia maadili chanzo chake ni Imani za kidini.

Makatazi ya dini ya Kikristo na Kiislamu ndiyo huleta maadili?

Kwa maelezo yako wewe inaonekana hukubaliani na hoja ya Infropreneur kuwa maadili hutokezwa na "Common sense" tu.
Wahadzabe, Watindiga, Wasandawe na Bushmen huko maporini hawana dini wala imani za ukristo na uislamu. Ila wana maadili.

Sasa hapa automatically, Dini sio kigezo cha watu kuwa na maadili.
 
Wahadzabe, Watindiga, Wasandawe na Bushmen huko maporini hawana dini wala imani za ukristo na uislamu. Ila wana maadili.

Sasa hapa automatically, Dini sio kigezo cha watu kuwa na maadili.
Labda dini ni nini?Maana Inawezekana wana dini zao ambazo si uislamu Wala ukristo.

Tukijua dini ni nini itatusaidia Sana kwenye mjadala huu.
 
Kwa ivo kwanza kabisa unaamini maadili yanatokana na mambo ya Imani fulani au mwenendo wa jamii husika

Pia maadili chanzo chake ni Imani za kidini.

Makatazi ya dini ya Kikristo na Kiislamu ndiyo huleta maadili?

Kwa maelezo yako wewe inaonekana hukubaliani na hoja ya Infropreneur kuwa maadili hutokezwa na "Common sense" tu.
Hayo ni mawazo yake infropreneur . Mm yangu ndo hayo kama unaswali katika hoja zangu ntajaribu kukujibu kadri ntavyoweza.

Ndio , dini kwa kiasi kikubwa ndo zimeleta maadili.
 
Labda dini ni nini?Maana Inawezekana wana dini zao ambazo si uislamu Wala ukristo.

Tukijua dini ni nini itatusaidia Sana kwenye mjadala huu.
Dini ni utaratibu wa maisha aishio mtu.
Hakuna mtu asiye na dini.
Utaratibu unaouishi ndo dini Yako.
Ukiamka asubuhi ni kuzurura mpka jioni, huamini kama mungu yupo , unaishi utakavyo wewe. Hiyo ndo dini Yako, ndo utaratibu wako wa maisha uliojiwekea.
 
Dini na evolution,
Mfano kutofanya mapenzi kati ya ndugu ni sababu za evolution zaidi ili kuepusha magonjwa ya kurithi
Sasa hii ya kuepusha magonjwa ya kurithi ilianza lini? Au maana yake mtu asiyeogopa magonjwa ya kurithi akingonoka na nduguye jamii imchukuliaje?
 
Infropreneur Kwa mfano kuwe na mtu/watu wanaoona ni sawa Wanandugu kungonoka. Sasa Hawa jamii ifanye nini dhidi Yao?
Inategemeana na wanandugu maana kuna mila za watu mabinamu watoto wa mashangazi na wajomba wanaweza kuoana. Na hiyo wanaona sawa tu.

Ila sijawahi kuona mila ya wazazi kulala na watoto wao. Na mila hiyo ionekane ni sawa tu.

Ukiona mtu anaona sawa wana ndugu wa karibu sana kama wazazi na watoto kongonoka huyo hana common sense na dishi lake limeyumba.

Huo utakuwa ni ukichaa sio ufahamu.

Awaishwe akafanyiwe mental rehabilitation therapy.
Yaani waachiwe familia Moja waoane wenyewe Kwa wenyewe ama nini kifanyike ili common sense zao zizinduke kujua baba au mama na mtoto haifai kungonoka?
Huwezi kukubali kulala na mzazi wako au binti yako kwa common sense zilizo timamu.

Hapo lazima dishi limeyumba au ujitoe ufahamu ndio utaweza kufanya hivyo.

Na hapo hutakuwa na common sense tena bali ukichaa.
 
Maadili yapo tu... Naweza sema binadamu hana influence kwenye Maadili kwa namna yoyote.
Kuna Natural Power inayosimamia uwepo wa Wastrabu, Wezi, Akili nyingi, wenye akili ndogo, Vibaka, Wachungaji n.k na lazima wote wawepo
 
Back
Top Bottom