Maadili tunayoyaamini yanatokana na kitu gani?

Wahadzabe, Watindiga, Wasandawe na Bushmen huko maporini hawana dini wala imani za ukristo na uislamu. Ila wana maadili.

Sasa hapa automatically, Dini sio kigezo cha watu kuwa na maadili.
Ulishayaona maadili ya Watindiga/Wahadzabe? Mwanaume akienda kuwinda akiua mnyama mkubwa kijiji kizima kinahamia kwake na analala na wanawake wote kijijini hapo, je hayo ndiyo maadili? Maadili yote tunayofuata yanatokana na miongozo ya Kanisa Katoliki!
 
Kama wao wanaona sawa hayo ni maadili kwao ya jamii yao.

Kuna maadili ambayo yapo automatically kwa kila binadamu mwenye utimamu.

Halafu kuna yale maadili ya kijamii mliyokubaliana kama wanajamii.

Mfano kwa jamii za kiislamu mwanamke kuvaa hijabu wanachukulia ni maadili kwao.

Lakini haimaanishi kwamba asipovaa hiyo hijabu hana maadili ya kibinadamu.
 
Kwa ivo kusingekuwepo na dini kusingekuwa na maadili?
Ndio kwa kiasi kikubwa.

Mfano: Waarabu zamani walikuwa wanaua watoto wao wa kike na ilikuwa ni Mila iloyozoeleka kwao na hakuna mtu aliyeshangaa, ulikuwa ndo utaratibu wao, Ilipokuja katazo katika Uislamu ikageuka kuwa jambo ovu na watu wakaanza kulichukia.
 
Kwenye jamii zetu unaona kabisa Kuna mifumo mbalimbali inayotumiwa kutunza kitu kinachoitwa maadili.

Lakini ili hayo maadili yawe maadili, chanzo chake huwa ni nini hasa.

Kwa nini watu washangae mtu kuwa na mahusiano na baba/mama yake au kaka/dada yake?

Kwani Baba, mama, kaka au dada, si wanawake au wanaume kama wengine? Kwa nini watu waone kama ni kinyume cha maadili?

Hivi mtu akiiba kitu kwa nini ionekane ni kinyume cha maadili. Hivi wizi si uwezo wa kuchukua kitu cha mwingine kwa kumzidi akili?

Hivi chanzo cha kuwepo kwa haya maadili ni nini. Na haya maadili yalianzaje anzaje?

CC: Kiranga , Infropreneur
Unataka kutuambia unachapa dada yako ewe kijana au?
 
Wote hata hao
Waarabu wameiga maadili kutoka kwa Wakatoliki!
Kwenye Uislamu kuna sheria ya kuoa wake Hadi wanne, wakatoliki wanayo!?.

Kwenye Uislamu kuna sheria ya kuswali swala tano, wakatoliki wanayo!?.

Kwenye Uislamu kuna sheria ya kumuabudu Mungu Mmoja pekee, wakatoliki wanayo!?.
 
Ulishayaona maadili ya Watindiga/Wahadzabe? Mwanaume akienda kuwinda akiua mnyama mkubwa kijiji kizima kinahamia kwake na analala na wanawake wote kijijini hapo, je hayo ndiyo maadili? Maadili yote tunayofuata yanatokana na miongozo ya Kanisa Katoliki!
Kwahy Hadi walio olewa!?. Au hicho Kijiji wanaishi wasio olewa na wasio oa!?.
 
Ni swali zuri...linahitaji mjadala uliokwenda shule hasa.
Tunaweza kusema kwamba kuna "Darwinian" explanation kama chanzo cha maadili. Kwa maneno mengine vile vinasaba vinavyofungamanishwa na sifa /"traits" zinazodhihirisha "maadili" vilikuwa vikitunzwa na kuzalishwa tena vizazi na vizazi........

Nadharia ya kwamba dini ndio chanzo cha maadili ni dhaifu....sababu maadili yamekuwepo kabla ya dini...pia maadili ni universal,....unlike dini.....
 
Kwani dini imezalishwa lini!?. Unajua dini ni nini!?.

Ina maana binadamu wa kwanza Hawa na Adamu hawakuwa na dini!?.

Waliwezaje kuendesha maisha Yao kama hawakuwa na dini!?.
 
Kwenye jamii zetu unaona kabisa Kuna mifumo mbalimbali inayotumiwa kutunza kitu kinachoitwa maadili.

Lakini ili hayo maadili yawe maadili, chanzo chake huwa ni nini hasa.

Kwa nini watu washangae mtu kuwa na mahusiano na baba/mama yake au kaka/dada yake?

Kwani Baba, mama, kaka au dada, si wanawake au wanaume kama wengine? Kwa nini watu waone kama ni kinyume cha maadili?

Hivi mtu akiiba kitu kwa nini ionekane ni kinyume cha maadili. Hivi wizi si uwezo wa kuchukua kitu cha mwingine kwa kumzidi akili?

Hivi chanzo cha kuwepo kwa haya maadili ni nini. Na haya maadili yalianzaje anzaje?

CC: Kiranga , Infropreneur
Maadili mengi yanatokana na sababu practical.

Mfano, kulikuwa na Mafarao wa Misri waliamimi familia zao ni takatifu za kimungu walioana wenyewe kwa wenyewe, matokeo yake, kutokana na gene pool kuwa ndogo, waliishia kupata magonjwa mengi ya genetic.

Wenye busara wakaangalia wakaona kuwa kuoana ndugu si kitu kizuri, kinaleta matatizo.

Wizi umeonekana kuwa unaondoa order katika jamii, unaumiza watu waliochuma mali zao kihalali, ni kitu ambacho watu wengi hawapendi kufanyiwa, hivyo ikaoneoana kuwa ni kitu kibaya jamii isikiruhusu.

Ndivyo maadili yalivyoanza, jamii isiyo na misingi mizuri ya kimaadili haitaweza ku survive. Na inawezekana jamii hizo zilikuwepo na sasa hazipo, kwa sababu hazikuwa na order.

Jamii zilizoweza kuwa na order ndizo zilizoweza ku survive.

Hivi ndivyo maadili yalivyoanza na kuingia kwenye uongozi, kwenye dini mpaka kwenye sheria.

This is necessary for society to function and survive.
 
Kuna vyanzo kadhaa vya maadili (sourses of ethics) miingoni mwake ni
1. Dini kupitia maadiko matakatifu kama vile Biblia na Quran. Mfano kwa wakristu wana zile amri 10 za Mungu ambazo kila amri moja una tafsri pana inayolenga kulinda maadili.

2. Elimu: mashuleni au vyuoni ufundishwa kuhusu maadili
3. Familia
4. Tamaduni za jamii husika (culture background)
5. Wanafalsafa mbalimbali nk
Hizo ni miingoni mwa vyanzo vya maadili nimeandika kwa ufupi sana
 
Maadili mengi yanatokana na sababu practical.

Mfano, kulikuwa na Mafarao wa Misri waliamimi familia zao ni takatifu za kimungu walioana wenyewe kwa wenyewe, matokeo yake, kutokana na gene pool kuwa ndogo, waliishia kupata magonjwa mengi ya genetic.

Wenye busara wakaangalia wakaona kuwa kuoana ndugu si kitu kizuri, kinaleta matatizo.

Wizi umeonekana kuwa unaondoa order katika jamii, unaumiza watu waliochuma mali zao kihalali, ni kitu ambacho watu wengi hawapendi kufanyiwa, hivyo ikaoneoana kuwa ni kitu kibaya jamii isikiruhusu.

Ndivyo maadili yalivyoanza, jamii isiyo na misingi mizuri ya kimaadili haitaweza ku survive. Na inawezekana jamii hizo zilikuwepo na sasa hazipo, kwa sababu hazikuwa na order.

Jamii zilizoweza kuwa na order ndizo zilizoweza ku survive.

Hivi ndivyo maadili yalivyoanza na kuingia kwenye uongozi, kwenye dini mpaka kwenye sheria.

This is necessary for society to function and survive.
Kwahy maadili yamejumuishwa kwenye dini!?. Na dini haikujumuisha maadili!?.

Kwa lugha nyepesi maadili ndo yalianza Kisha dini zikaongeza hayo maadili katika sheria na taratibu zao!?.
 
Maadili ndiyo yalianza halafu wajanja wakaangalia haya maadili tuyawekeje ili iwe lazima watu wayafuate?

Tukisema tu haya ni maadili yetu tumejiwekea watu, kuna wabishi hawatayafuata.

Ili wayafuate, tuseme hizi ni sheria za Mungu, ukikiuka, utakufa, ukikiuka, utapata dhambi na kuchomwa moto wa milele, kasema Mungu hivyo.

Ndiyo dini zikazaliwa hapo.

Dini ziliwekwa kama chombo cha kustawisha maadili yaliyokuwapo kabla ya dini, maadili hayakutokea katika dini.
 
Anhaa, Sasa mbona kukawa na mvutano wa hzo dini na sheria zake, ikiwa ni watu walikaa wakaona wayaweke maadili katika dini ili watu waweze kuyafata kwa Ile hofu waliyowekewa!?.
 
Dunia imekuwa na mvutano siku zote.

Utaona kuwa hata kabla ya hayo maadili kuwekwa kwenye dini, kuna watu walikuwa hawataki kuyafuata ndiyo maana yakawekwa kwenye dini.

Hata baada ya maadili kuwekwa kwenye dini, kuna watu waliona ukweli na kusema kuwa hizi habari za Mungu kasema ni hadithi za watu tu.

Na kumbuka kuwa hii habari ya kuweka maadili kwenye dini haikufanyika sehemu moja. Wamisri wa kale walifanya hivyo, Wasumeria walifanya hivyo, Wachina wa kake wakifanya hivyo.

Kwa hiyo, dini na sheria zake zikaibuka na tabia za kiutamaduni za sehemu husika.

Ndiyo maana dini tofauti zina migongano inayoenda na tamaduni za sehemu tofauti.
 
Chanzo cha maadili ni common sense tu.

Binadamu yeyote mwenye ufahamu na utimamu automatically lazima awe na utambuzi wa mambo ambayo yeye mwenyewe hataki afanyiwe na mtu yeyote yule.

Vivyo hivyo, Mambo hayo ambayo wewe binafsi hutaki kufanyiwa, Huwezi kumfanyaia mwenzako. Na Ndio maadili hayo.

Hebu fikiria binti yako anakuja na kukwambia "Baba njoo tusex wote" Yani hapa automatically ufahamu wako uta react kwa hasira kali sana. Kwamba hilo jambo si la kawaida.

Ni kinyume na utambuzi wako wa kifikra kulala na mwanao, binti yako. Yani common sense tu itakufanya u react vibaya mno kukemea hicho kitendo. Labda kama dishi lako liwe limeyumba ndio utakubali kufanya hivyo.

Na hapa ndipo chanzo cha maadili huanzia. Through common sense tu.

Kitu ambacho wewe hutaki kufanyiwa, Huwezi kumfanyia mwenzako.

Na mambo hayo ndio maadili.
Hayawani pekee ndo anaweza kumkula mama yake au baba kumkula mtoto wake.
 
Anhaa, Sasa mbona kukawa na mvutano wa hzo dini na sheria zake, ikiwa ni watu walikaa wakaona wayaweke maadili katika dini ili watu waweze kuyafata kwa Ile hofu waliyowekewa!?.
Nadhani suala la mvutano lipo kutokana na kutofautiana mitazamo kiimani. Ila kwenye suala la maadili kila dini inatetea maadili kwa namna wanavyoyaainisha wao. Na kuna wanafalsafa ambao waliainisha nadharia tofauti kuhusu maadili, mfano Plato na Alstotle wanaamini maadili hutokana na tabia au sifa za mtu (virtue characters), ipo pia nadharia ya kwamba ili tujue kuwa kitendo fulani ni maadili tuzingatie matokeo ya maamuzi fulani, nk
 
Maadili ndiyo yalianza halafu wajanja wakaangalia haya maadili tuyawekeje ili iwe lazima watu wayafuate?

Tukisema tu haya ni maadili yetu tumejiwekea watu, kuna wabishi hawatayafuata.

Ili wayafuate, tuseme hizi ni sheria za Mungu, ukikiuka, utakufa, ukikiuka, utapata dhambi na kuchomwa moto wa milele, kasema Mungu hivyo.

Ndiyo dini zikazaliwa hapo.

Dini ziliwekwa kama chombo cha kustawisha maadili yaliyokuwapo kabla ya dini, maadili hayakutokea katika dini.
Una ushahidi hani kwamba maadili yalikuwepo kabla ya dini? Nipe mfano wa hayo maadili.
 
Back
Top Bottom