Maadili tunayoyaamini yanatokana na kitu gani?

Maadili tunayoyaamini yanatokana na kitu gani?

Hao Adam na Hawa hawakuwahi kuwapo.

Huyo Mungu mwenyewe ni muhusika katika hadithi ya uongo ya kutungwa na watu tu.

Ndiyo maana hii hadithi ukiichunguza ina maswali yasiyojibika.

Ni hadithi yenye longolobgo nyingi za kuungwaungwa na watu tu, kamba nyiiingi za kijinga tu.
Kwahiyo mkuu unataka kuniambia sisi tumekujaje hapa duniani?
 
Mkuu issue sio kuwalaumu hao Miungu,, Issue ni kwamba dhana ya neno "Mungu" haijulikani kama ipo au haipo.

Hakuna anaeweza kuthibitisha kama yupo, Hakuna anaeweza kupinga kama Hayupo, Hakuna anaejua lolote kuhusu dhana ya neno "Mungu" ,,,,,,,,,,,,!
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote anaweza kuthibitishwa kimantiki kwamba hayupo.

Na kwa kuanzia huyo wengine wote wanaweza kuoneshwa kuwa likely ni uongo ule ule.
 
Kwahiyo mkuu unataka kuniambia sisi tumekujaje hapa duniani?
Suala la sisi tumekujaje hapa duniani ni zuri, kubwa na lina maelezo mengi ya kitaalamu.

Na tunaweza kwenda kulichambua.

Na katika kulichambua, kuna kitu kinaitwa "elimination method".

Elimination method inaanza kuondoa majibu yasiyo sahihi kabla ya kupata jibu sahihi.

Katika kuondoa majibu yasiyo sahihi naondoa jibu la Mungu, huyu hayupo.

Jibu sahihi lipo katika evolution. Watu wame evolve kuwa hivi walivyo, hawajaumbwa kuwa hivi na Mungu.

Wangeumbwa na Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote wasingekuwa na vilema wala kupewa mzigo wa kunyakunya na kujambajamba kila siku.

Mungu huyo angetuhurumia na kutuumba bila mizigo hiyo ya vilema, kunyakunya na kujambajamba kila siku.
 
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote anaweza kuthibitishwa kimantiki kwamba hayupo.

Na kwa kuanzia huyo wengine wote wanaweza kuoneshwa kuwa likely ni uongo ule ule.
Mimi mtu mmoja akiniambia Mungu yupo ntamwambia sawa, Au mwingine akasema Mungu hayupo nitamwambia sawa pia.

Baada ya hapo kila mmoja atatakiwa kwanza anielekeze maana ya dhana "Mungu" ni nini?

Maana huwezi ukasema kitu kipo halafu kisionekane na Huwezi kusema kitu hakipo wakati hujawahi kukiona, kukitazama,
kukifikiri na kukisikia.

Mfano mimi nikwambie "MOGHTRD" yupo, Au nikwambie "MOGHTRD" hayupo, utaniuliza swali gani?

Niijue hii dhana ndipo sasa aanze kuniambia hicho kitu "Kitu" au "Hakipo".

That's why ninasema hakuna anayejua hizo habari kama zipo au hazipo, Kama hakuna anayejua, hakuna haja ya kubishiana vitu Fictious.
 
Kwenye jamii zetu unaona kabisa Kuna mifumo mbalimbali inayotumiwa kutunza kitu kinachoitwa maadili.

Lakini ili hayo maadili yawe maadili, chanzo chake huwa ni nini hasa.

Kwa nini watu washangae mtu kuwa na mahusiano na baba/mama yake au kaka/dada yake?

Kwani Baba, mama, kaka au dada, si wanawake au wanaume kama wengine? Kwa nini watu waone kama ni kinyume cha maadili?

Hivi mtu akiiba kitu kwa nini ionekane ni kinyume cha maadili. Hivi wizi si uwezo wa kuchukua kitu cha mwingine kwa kumzidi akili?

Hivi chanzo cha kuwepo kwa haya maadili ni nini. Na haya maadili yalianzaje anzaje?

CC: Kiranga , Infropreneur

Maadili ni nini? Kuna document ya reference? Au ni perception ya mtu fulani tu? Au intuition?
 
Mimi mtu mmoja akiniambia Mungu yupo ntamwambia sawa, Au mwingine akasema Mungu hayupo nitamwambia sawa pia.

Baada ya hapo kila mmoja atatakiwa kwanza anielekeze maana ya dhana "Mungu" ni nini?

Maana huwezi ukasema kitu kipo halafu kisionekane na Huwezi kusema kitu hakipo wakati hujawahi kukiona, kukitazama na kukisikia.

Niijue hii dhana ndipo sasa aanze kuniambia hicho kitu "Kitu" au "Hakipo".

That's why ninasema hakuna anayejua hizo habari kama zipo au hazipo, Kama hakuna anayejua hakuna haja ya kubishiana vitu Fictious.
Ndiyo maana nimeanza kwa kusema Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote.

Nimeweka defining characteristics za huyo Mungu kabla ya kusema hayupo.

Tatizo mara nyingi tunaenda kwenye mjadala wa Mungu bila hata ya kum define.
 
Huyo ni wa kwenye hadithi za kitabu cha biblia, anaitwa "Yehova".

Huyu huwa hata hahitaji mtu kutoa introduction ya maana ya "Mungu", huyu sifa zake hazijawahi kuendana na yeye alivyo.
 
Huyo ni wa kwenye hadithi za kitabu cha biblia, anaitwa "Yehova".

Huyu huwa hata hahitaji mtu kutoa introduction ya maana ya "Mungu", huyu sifa zake hazijawahi kuendana na yeye alivyo.
Si Yehova tu, hata Allah na wengi wengine wana sifa hizo.

Ukiyaangakia yale majina 99 ya Allah sifa zote hizo zimo.
 
Si Yehova tu, hata Allah na wengi wengine wana sifa hizo.

Ukiyaangakia yale majina 99 ya Allah sifa zote hizo zimo.
Hata Miungu ya wahindi: Mungu rahman, Vishnu, Shiva, Lakshmi, Durga, Ganesh na Saraswati.

Miungu ya wabudha iliyoletwa na wazee wa kale kina
buddha, Avalokiteshvara, Manjushri na Maitreya.

Yote ni Fictious sababu inaanza kutajwa pale inapoamuru kuiumba dunia "kitu fulani tokea" ila yenyewe haitajwi ilipotokea.

Hivyo hakuna anayeweza kua na uhakika na kuthibitisha dhana "Mungu" kama kweli ipo?

Au kama yupo atusaidie, ila ni vyema kabla hajafafanua aje na maana ya "Mungu" kwanza.
 
Dhana "Mungu" ipo, ndiyo hii tunayoijadili. Hii ni dhana.

Ila, Mungu anayeelezwa na hiyo dhana hayupo.
 
Maadili ni nini? Kuna document ya reference? Au ni perception ya mtu fulani tu? Au intuition?
Ndiyo tupo hapa tunajadili. Maana tukianza kuwa na mtazamo Fulani mitazamo ya wengine tunaona haifai Kwa mjadala.

Kila mtu anaruhusiwa kusema anavyoona yeye kuhusu maadili.
 
Ndiyo tupo hapa tunajadili. Maana tukianza kuwa na mtazamo Fulani mitazamo ya wengine tunaona haifai Kwa mjadala.

Kila mtu anaruhusiwa kusema anavyoona yeye kuhusu maadili.
I see this too subjective brother, bila definition tutajadili hewa, maadili ni neno ambalo linatumika vibaya sana nchini kwetu kuua vipaji, linatumika kutisha innovators kwa sababu tu watu wanataka wafit to their comfort zones, dunia inatuacha kwa kasi sana sisi tunabaki na ukaririsho ambao hauna hata evidence kwa jina la "maadili" the same thing ikifanywa na watu wengine wanapiga pesa na kusonga mbele!
 
Dhana "Mungu" ipo, ndiyo hii tunayoijadili. Hii ni dhana.

Ila, Mungu anayeelezwa na hiyo dhana hayupo.
Kama unakubali dhana "Mungu" ipo, unawezaje wakati huo huo kusema tena Mungu hayupo.

Maana dhana ina sifa ya kufafanulika, Kubadilika, kulinganishwa, kueleweka na kuwepo kimazingira na kihisia.
 
Kama unakubali dhana "Mungu" ipo, unawezaje wakati huo huo kusema tena Mungu hayupo.

Maana dhana ina sifa ya kufafanulika, Kubadilika, kulinganishwa, kueleweka na kuwepo kimazingira na kihisia.
Dhana ni dhana, abstract thought.

Mfano, naweza kufikiri dhana ya "pembetatu duara", pembetatu ambayo hapo hapo ni duara, katika Euclidean geometry, wakati kiuhalisia pembetatu ina nyuzi 180 na duara lina nyuzi 360 na pembetatu haiwezi kuwa duara.

Naweza kufikiri dhana ya "namba kubwa kuliko zote", hiyo dhana naweza kuifikiria, naweza hata kuipa symbol. Lakini kufikiria dhana hiyo haimaanishi namba hiyo ipo, kwa sababu namba yoyote nitakayosema ni kubwa kuliko zote, nikiongeza moja tu naonesha kuwa namba hiyo si kubwa kuliko zote.
 
Back
Top Bottom