Maadili tunayoyaamini yanatokana na kitu gani?

Nadhani suala la mvutano lipo kutokana na kutofautiana mitazamo kiimani. Ila kwenye suala la maadili kila dini inatetea maadili kwa namna wanavyoyaainisha wao. Na kuna wanafalsafa ambao waliainisha nadharia tofauti kuhusu maadili, mfano Plato na Alstotle wanaamini maadili hutokana na tabia au sifa za mtu (virtue characters), ipo pia nadharia ya kwamba ili tujue kuwa kitendo fulani ni maadili tuzingatie matokeo ya maamuzi fulani, nk
Mfano Baba kumnyunda mtoto wake ni kinyume na maadili ya kibinadamu lakini Kuna wababa kadhaa Duniani wamewanyunda mabinti zao na imekuwa unyama tu, hakuna madhara yoyote waliyoyapata sanasana unakuta mtoto anautaka Tena au baba kanogewa.

Lakini kwenye common sense tunasema, mzee na mtoto wake wote ni hayawani, kwasababu ni kinyume na fahamu timamu za kibinadamu.
 
Una ushahidi hani kwamba maadili yalikuwepo kabla ya dini? Nipe mfano wa hayo maadili.
Organization ya maadili haihitaji order kubwa kama organization ya dini.

Organization ya maadili inaweza kufanyika kirahisi hata katika ngazi ya familia au watu wawili tu.

Watu wawili kugawana nyama haihitaji dini, inahitaji maadili ya kugawana nyama sawa tu.

Ila, kugawa chakula kingi kwa mamilioni ya watu na kuweka maadili watoto na wanawake wapewe upendeleo maalum sehemu ambayo chakula hakitoshi inawezekana pakahitajika dini.

Kadiri watu wanavyoongezeka na competition inavyoongezeka hapo ndipo jamii inahitaji uwepo wa dini.

Ukisoma historia utakutana na hilo jambo.

Msome Francis Fukuyama katika kitabu chake "The Origins of Political Order: From Prehuman Times to the French Revolution" kaelezea vizuri suala hili.
 
We jamaa wewe.
 
Hapo maadili ni neno ambalo ndilo lipo katika wigo mpana.

Lakini nachoweza kusema chanzo cha maadili kinatokana na utu.

Ndani ya "utu" kuna kitu kinaitwa "empathy".

Empathy ni uwezo wa ku share hisia za mwingine kwa kujiweka katika nafasi yake dhidi ya jambo fulani ili kujua namna anavyo jiskia.

Empathy ni namna ya kujua mambo ya kweli kuhusu wengine. Pale ambapo huwezi kuhisi wanacho hisi basi Empathy ndio ufunguo wa kuweza kujua how they feel.

Yani ile hali ya kumfanyia mtu mazuri ambayo ungependa na wewe ufanyiwe. Na kutomfanyia mtu yale ambayo wewe mwenyewe usingependa ufanyiwe.

Empathy kwa lugha rahisi ni namna ya kuweza kuvaa viatu vya mwingine kwa lengo la kupima mzani wa jambo ambalo lipo mbele yake.

Mfano kwa kinachoendelea hivi saizi hapa nchini kuhusiana na maswala ya utekaji ambao wahanga wamekuwa wakikutwa wamejeruhiwa au kuuawa na sometimes kupotezwa kabisa.

Then katika moment hiyo tunaona baadhi ya watu wakisema kuwa sio kweli kuwa kuna utekaji bali ni watu wanajiteka ili kutengeneza drama.

So hao watu wanaokana kuwa hakuna utekaji wangetumia empathy wangeweza kuwaza namna hii "vipi kama ingenitokea ni mimi nimetekwa halafu nikasikia kuna watu wanatoa kauli za kebehi kuwa nimejiteka"

"Vipi kama angekuwa ndio mtoto wangu ameuawa halafu nikasikia watu wanaleta dhihaka kuwa ni drama"

Je ningejiskia vizuri? Jibu ni hapana.

Swali linakuja "kwanini nitoe maneno ya dhihaka kwa muhanga wa hayo matatizo huku nikijua kabisa kwa kufanya hivyo nitaenda kumuongezea maumivu zaidi??

"Je mimi ningependa kufanyiwa nini iwapo situation hiyo ingenikuta"
Then baada ya hapo ndio unafanya maamuzi.

Tujifunze sana hii kitu ni muhimu sometimes situation inaweza kutokea ambapo kitu pekee kitachojalisha ni wewe na namna ambavyo umeweza kuzihisi hizo feelings, utajikuta unawaumiza wengine kwasababu ya upumbavu wako.
 
Unapozungumzia maadili unazungumzia "Kutenda mema".

Kwanza nini kinafanya tutenganishe kwamba jambo hili ni jema na jambo hili ni baya?

Jambo linaweza kutajwa kama ni jema ikiwa halina upendeleo na uonevu, linaleta manufaa kwa watu wengi lakini linaibua hisia nzuri kama vile furaha, amani, kuridhika, upendo n.k

Jambo linaweza kutajwa kama baya ikiwa linahatarisha ustawi wa wengine, lina madhara yasiyo epukika au pengine litasababisha kuibua hisia za chuki, lawama, hasira, hofu, Aibu, majuto, unyoge n.k

Wanafalsafa wa zamani kina Plato, Aristotle, Zeno, Epicurus,
na Socrates walitumia njia tofauti kugundua kanuni za maadili mfano;

•Epicurus wa "Epicureanism" alitumia mbinu ya kuangalia matokeo ya jambo/mambo, hivyo akagundua "vitendo vyote vinapaswa kua na madhumuni ya kupunguza maumivu na kuongeza furaha" Hivyo akaandika falsafa yote katika matiki hiyo.

Plato, mwanafunzi wa Socrates aligundua kuwa "Maadili" hutokea pale kila mtu anapowajibika na kile anachopaswa kukifanya katika jamii, kwamba haki inapatikana pale kila mmoja anapopata kile anachostahili toka kwa mwingine.

Epictetus na Seneca wa "Stoicism", Walitumia mbinu ya kupima usawa. Waligundua kuwa maadili yanapatikana pale jamii ikitendeana kwa usawa na kuwa na tabia ya kujali wengine bila kujali hali ya jamii husika kiuchumi, kuafya, kimaumbile n.k

•Ukiangalia hawa babu zetu waanzishi wafalsafa, Waliumiza sana akili zao kuhakikisha wanakuja na solution itayofanya jamii yetu iwe na Usawa "Maadili".

•Katika gunduzi zao tunapata kujifunza kwamba wote walitumia karibu vipimo sawa hivyo tukijumuisha mawazo yao wote tunaipata kanuni moja kuu ya msingi wa Maadili inaitwa - GOLDEN RULE.

GOLDEN RULE - Watendee wengine sawa na unavyopenda kutendewa.

•Kwahiyo watu wote tunatumia hii sheria kama msingi mkuu wa Maadili, Hakuna mtu anaependa kuchukiwa, kugombezwa, kuonewa wivu, kudanganywa, kudhurumiwa, kudharauliwa, kupuuzwa n.k

Bali kila mtu anapenda kusifiwa, kuheshimiwa, Kusaidiwa, kuonewa huruma, kusikilizwa, kuaminika, kufurahi n.k

Kwahiyo unapotenda matendo ambayo yanawafurahisha na sio kuwaumiza wengine, ndiyo watenda "Maadili" hivyo.

"Golden rule" ndiyo msingi mkuu wa Maadili kwa jamii za mahala pote mpaka wasomi na wanazuoni walio andika vitabu vya dini walielewa hili fundisho ijapo wao wakaweka kama vile Miungu yao ndiyo inataka hivyo, Mfano:

WAISLAMU:
Surah An-Nisa (4:36)
"Muabuduni Allah, wala msimshirikishe na yeyote; na mtendee wema wazazi, jamaa, mayatima, masikini, jirani aliye karibu, jirani mgeni, rafiki wa kando, msafiri, na wale wanaokufanyia kazi. Hakika Allah hawapendi wale wanaojiinua na kujivuna."

WAKRISTO:
Luka 6:31 (Tafsiri ya Kiswahili):
"Kama vile mnavyotaka watende nini, ninyi nanyi mtende vivyo hivyo kwao.

WAHINDI/HINDUISM:
"Mtu hapaswi kutenda kwa wengine kwa njia ambayo inasababisha maumivu kwake mwenyewe." (Mahabharata 5:1517)

WABUDHA :
"Usitendee wengine kwa njia ambayo wewe mwenyewe ungefikiria kuwa ni mbaya (Dhammapada 1:7)

Mtu kama ZENO amegundua falsafa "stoicism" ambayo ni falsada bora kuliko fundisho la dini yeyote kabla hata biblia haijaanza kuandikwa.

Kihistoria inaonyesha Mwanafalsafa "CONFUSIOUS-561BC" amezaliwa kipindi sawa na kina "JEREMIAH - 570BC" na "EZEKIEL - 575BC" wa kwenye biblia.

Ila cha ajabu Mungu wa wakristo, Mungu wa haki na Upendo aliwapendelea maarifa manabii wake hao na kuwaacha kina Confusious wasugue vichwa vyao wenyewe kubuni kanuni nzuli za "Kiadili" na "Usawa".

HITIMISHO: Maadili msingi wake mkuu ni "Akili" , Hakuna spiritual being yeyote iliwahi kuhusika kuandaa na kugundua kanuni za kiadili na usawa.

,,,,,,,,,,,,,! 😎
 
Pamoja na maelezo marefu yenye faida ya Ibn Unuq hitimisho lake linafanana Kwa sehemu kubwa Sana na mtazamo wa Kiranga kuwa maadili yameanzishwa na binadamu kwa kuangalia mwenendo wa maisha yao na jinsi ya kudhibitiana.

Lakini Kiranga yeye kaongeza kitu kingine kuwa maadili yalianzishwa na binadamu nje ya dini na wajanja wakayaweka hayo maadili kwenye dini.

Kwa maelezo ya Kiranga ambayo kwa Karibu yanashabihiana na yale ya Ibn Unuq, binadamu walijitafakari kisha wakatunga maadili yao.

Na wote kimsingi wamesimama na hoja kuwa maadili hutokea pale mtu anapotakiwa kutowatendea wengine kile ambacho yeye asingependa kutendewa.

Na Kiranga pia ameleta hoja kuwa mipaka ya nani anamuoa nani ilitokana na uzowefu wa ndugu kujamiiana wenyewe Kwa wenyewe kisha yakatokea magonjwa ya vinasaba (Genetic disorder diseases) hivyo watu wakagutuka na kuweka mipaka ya kujamiiana.

Scars yeye amekuja na hoja kuwa maadili hutokana na utu. Utu ndiyo huzaa ile hali ya mtu kuhisi maumivu ya mwingine (empathy) hata kama si yeye anayetendewa ubaya anaotendewa mwingine.

Kwa mbali kwenye maelezo niliyoyasoma, naona kama vile binadamu ana hisia chanya na hasi. Yaani anao uwezo wa kutofautisha baya na Jema.

Kwa maana nyingine tunatakiwa kujua hizo hisia huna tu zenyewe toka kusikojulikana, huzaliwa nazo au hutokeaje.

Hisia za kumfanya mtu achukie kwa kufanyiwa mabaya au afurahi anapofanyiwa mema , hutoka wapi.

Nadhani hizi hisia ni chanzo cha maadili. Yaani maadili yapo ili hisia za watu zisiumizwe bali ziwe na furaha.

Jee mzizi wa hisia ni nini?
 
Hizo hisia ni lazima ziwepo kwa jamii complex.

Maana yake ni kwamba, jamii na species ambazo hazikuwa na hisia hizo, zilishauana na kumalizana na hazikuweza ku survive.

Jamii na species ambazo zimeweza kuwa na hisia hizo ndiyo zimeweza ku survive.
 
Mfumo wa Kibaolojia/Nature ya ubongo wa binadamu.

Ukiusoma vizuri Ubongo wa binadamu, kuna sehemu kama Amygdala, Hippocampus, PFC, Insula cortex, Cingulate cortex na Hypothalamus.

Hizo sehemu za ubongo ni maarufu kwa uwezo wake wa kutunza na kuratibu habari za kihisia.

Kemikali za Ubongo pia zinasababisha hisia [Neurotransmiters] kama
Dopamine, Serotonin, Oxytocin, Endorphine Adrenaline, GABA na nyinginezo kila moja ina kazi yake mwilini ya kuleta hisia za raha, karaha, minyegeresho, uchovu, maumivu, huzuni, furaha na nyinginezo.

Pia mwili wa binadamu wenyewe kama wenyewe una Homoni kama vile adrenaline na oxytocine, pia zinasababisha kuhisi.

Kwahiyo chanzo cha hisia kwa binadamu ni nature yenyewe ya ubongo wetu na mfumo wetu wa fahamu , ndiyo vyanzo vya miili yetu kuwa na uwezo wa kuchakata hisia.

Ndiyo maana watu wenye "Depression" uwezo wao wa kuhisi unashuka au unapotea kabisa.

Hisia zinazidi kubadilika siku hadi siku kulingana na saikolojia ya watu, Fikra, Imani, Maarifa, Mazingira na Sababu za kijenetiki "Genetic Inheritance".
 
Infropreneur Kwa mfano kuwe na mtu/watu wanaoona ni sawa Wanandugu kungonoka. Sasa Hawa jamii ifanye nini dhidi Yao?

Yaani waachiwe familia Moja waoane wenyewe Kwa wenyewe ama nini kifanyike ili common sense zao zizinduke kujua baba au mama na mtoto haifai kungonoka?
Tunaambiwa kwamba Binadamu wa kwanza ni Adam na Hawa. Ndio waanzilishi wa hiki kizazi...hii inamaana kuwa watoto wao walifanya tendo ili kuendeleza kizazi. Au nakosea mkuu?
Mungu aliruhusu vipi jambo kama hili?
 
Kwenye jamii zetu unaona kabisa Kuna mifumo mbalimbali inayotumiwa kutunza kitu kinachoitwa maadili.

Lakini ili hayo maadili yawe maadili, chanzo chake huwa ni nini hasa.

Kwa nini watu washangae mtu kuwa na mahusiano na baba/mama yake au kaka/dada yake?

Kwani Baba, mama, kaka au dada, si wanawake au wanaume kama wengine? Kwa nini watu waone kama ni kinyume cha maadili?

Hivi mtu akiiba kitu kwa nini ionekane ni kinyume cha maadili. Hivi wizi si uwezo wa kuchukua kitu cha mwingine kwa kumzidi akili?

Hivi chanzo cha kuwepo kwa haya maadili ni nini. Na haya maadili yalianzaje anzaje?

CC: Kiranga , Infropreneur
Maadili chanzo chake ni ufahamu wa mtu(common sense) huo ufahamu unampelekea kujua hiki ni sahihi, hiki sio sahihi, na huo ufahamu unatengeneza utaratibu wa namna ya kwenda au namna ya kuishi, huo utaratibu unaitwa maadili, kwa mfano hakuna sehemu pameandikwa ukiwakuta watu wazima uwasalimie, lakini utaona mzazi analazimika kumfundisha mtoto wake kuwa na huo utaratibu,na lengo la huo utaratibu ni kuhakikisha jamii inaishi kistaarabu uwepo wa haki na amani, kumbuka kwenye jamii tunaishi watu wa aina tofauti
 
Tunaambiwa kwamba Binadamu wa kwanza ni Adam na Hawa. Ndio waanzilishi wa hiki kizazi...hii inamaana kuwa watoto wao walifanya tendo ili kuendeleza kizazi. Au nakosea mkuu?
Mungu aliruhusu vipi jambo kama hili?
Mkuu issue sio kuwalaumu hao Miungu,, Issue ni kwamba dhana ya neno "Mungu" haijulikani kama ipo au haipo.

Hakuna anaeweza kuthibitisha kama yupo, Hakuna anaeweza kupinga kama Hayupo, Hakuna anaejua lolote kuhusu dhana ya neno "Mungu" ,,,,,,,,,,,,!
 
Sasa hii ya kuepusha magonjwa ya kurithi ilianza lini? Au maana yake mtu asiyeogopa magonjwa ya kurithi akingonoka na nduguye jamii imchukuliaje?
Binadamu wengi sio rahisi kupata tamaa ya kufanya mapenzi na wazazi wao au ndugu zao wa karibu, evolutionists wanasema hiyo ni mfumo wa ndani wa binadamu uliojijenga kwa muda mrefu kuepusha magonjwa ya kurithi kwa sababu huko nyuma inbreeding haikuwa beneficial trait kwa kuendeleza kizazi cha binadamu.

Ni kama vile ambavyo binadamu ana hofu kwa nyoka wote, wenye sumu na wasio na sumu bila hata kufundishwa kuwa na hiyo hofu na yeyote.
 
Tunaambiwa kwamba Binadamu wa kwanza ni Adam na Hawa. Ndio waanzilishi wa hiki kizazi...hii inamaana kuwa watoto wao walifanya tendo ili kuendeleza kizazi. Au nakosea mkuu?
Mungu aliruhusu vipi jambo kama hili?
Hao Adam na Hawa hawakuwahi kuwapo.

Huyo Mungu mwenyewe ni muhusika katika hadithi ya uongo ya kutungwa na watu tu.

Ndiyo maana hii hadithi ukiichunguza ina maswali yasiyojibika.

Ni hadithi yenye longolobgo nyingi za kuungwaungwa na watu tu, kamba nyiiingi za kijinga tu.
 
Back
Top Bottom