Kwahiyo ni kwamba:
A: kwa Maelezo ya dini na historia dhana ya "Mungu" ipo ila dini hazina uwezo wa kuthibitisha, linasimama tu kama dhana.
B: Kwa kigezo cha sifa za dhana, dhana "Mungu" haifikiriki, haibuniki, haithibitishiki wala haieleweki. Hivyo dhana "Mungu" haijulikani kama inatakiwa iwepo au isiwepo.
Huenda hapa ndipo Tofauti yetu ilipo lakini ni kidogo saana.
Dhana ya Mungu inafikirika, inabunika.
Ingekuwa haibuniki tusingeweza kuielezea.
Ingekuwa haifikiriki, isingekuwa dhana, kuweza kufikirika ndiko kunaifanya iwe dhana.
Mambo yasiyofikirika huwezi hata kuyaandika, kwa sababu unahitaji kuweza kuyafikiria ili uyaandike.
Ila, dhana ya Mungu (tukianza na muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote) ingawa inaeleweka, haieleweki kwa logical consistency, ukiipima kimantiki unaishia kuona contradictions ambazo haziwi resolved. Contradictions hizo zinaonesha kuwa hiyo dhana ni ya kuungaunga tu, haitokani na ukweli wa mambo nje ya ulikwengu wa hadithi za kutunga.
Kwa sababu hiyo hiyo, dhana hii haithibitishiki.
Mara nyingi mimi huwaukiza watu wanaosema habari za Mungu kuwapo wathibitishe.
Lakini, kuthibitisha Mungu yupo si muhimu sana. Kwa sababu inawezekana Mungu yupo ila hatuwezi kuthibitisha tu yupo.
Tatizo kubwa zaidi ya kuthibitisha ni contradictions na logical inconsistencies katika dhana ya kuwepo Mungu.
Kwa maneno mengine, kabla ya mimi kupinga uwepo wa Mungu, maelezo ya kuwepo Mungu yenyewe yanapinga uwepo wa Mungu.