DOKEZO Maafisa Elimu wawe wanapitia Shule zao kukagua Chakula wanafunzi Mashuleni

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Kumekuwa na changamoto mashuleni inayohusu chakula wanachokula wanafunzi kuwa na dawa ya kuhifadhia nafaka.

Hii hutokana na utaratibu mbovu wa kuhifadhi mahindi unaofanywa na baadhi ya shule kiasi kwamba mahindi husagwa yakiwa na dawa na kupelekea kwa shule wanazokula dona au mahindi yaliyosagwa bila kukobolewa

Hali hii ni hatari kwa afya ya wanafunzi na walimu kiasi kwamba ina uwezekano wa kupelekea matatizo mbalimbali ya kiafya ikiwa ni pamoja na matatizo ya kichwa, macho na hata kansa ya utumbo kwa kula chakula chenye dawa.

Jambo hili si vyema kupuuzia kwakuwa linaharibu kizazi kijacho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…