Tetesi: Maafisa Utumishi wanawabadilishia watu wenye vyeti feki data zao

Mkuu Umbeya Itakusaidia Nn?Hatakama Wakifukuzwa Wote Bdo Km Huna Bahati Huna Tu,mm Mbona Nimejiajiri Tu Mwenyewe Na Ni Make Mapesa,wala Sina Wivu Na Watumishi,waache Wenzako Wapige Kazi
 
Asante sana kwa taarifa. Watanzania tuache umangumashi ili tupate maendeleo halisi,
 
Umbeya wakati mwingine aulipi. Uhakiki ulifanyikaje, kwani Baraza ndiyo lilikuwa linavifuata hivyo vyeti au vilipelekwa na maafisa utumihi unaowasema? Kama kulikuwa na utaratibu sioni ni kwa nini uwe na wasiwasi.
Umbeya wakati mwingine aulipi. Uhakiki ulifanyikaje, kwani Baraza ndiyo lilikuwa linavifuata hivyo vyeti au vilipelekwa na maafisa utumihi unaowasema? Kama kulikuwa na utaratibu sioni ni kwa nini uwe na wasiwasi.
Nyie ndio vichaa mnaolirudisha nyuma taifa hili, maisha ya ujanja ujanja awamu hii hakuna. Mlizoea mpaka weekly test ya sekondari mnaingia na vibomu vya kupigia chabo.
Umbea hapa upo wapi huku mtu kaeleza hali halisi?
 
Mzee ingekuwa na idea ya IT usinge andika huo umbeya sababu afisa utumishi ni end user hawezi kubadilisha vitu vyote kwenye system bila kuwa na full access ya systems. Pia ukifanya auditing ya database unaweza jua nani kabadikisha nini kwenye system kama ndiyo hivyo hao watakamatwa wote.
 
Nchi hii viongozi mpk raia wote makanjanja tu.
 
Kwa nini usiseme masijala ndio wanacheza na file unasema HR? Pili inawezekana vipi kama taharifa za watumishi ziko kwenye system (lawson) na wenye access ni wachache ambao chochote watakacho change kitajulikana? Kwanza nilishangaa why serikali iliwaambia watumishi wapeleke vyeti. Hilo tamko tu liliwapa chance walio smart kucheza makaratee. Wangetumia vilivyo kwenye system.
 
Naona kuna watu hawajamwelewa mleta uzi. Mimi nimemuelewa hivi:
Hawa watumishi walikabidhi vyeti feki(vilivyomodolewa) wakati wanaajiriwa. Mf. mtu form four alipata div. 4, na cheti chake kinaonekana ana div 4. Lakini alikimodoa hadi akawa na cheti cha div 2 au 3 ambacho ndo alikitumia kujiendeleza kielimu hadi kuja kuajiriwa. Kwa hiyo, kile cha div 4 alikificha kabatini na kukikabidhi cheti cha kumodoa kwa mwajiri, na faili lake lina nakala ya cheti hiki.

Wakati wa uhakiki, idara ilipeleka Necta cheti kilichomodolewa. Necta wakaona ni cheti feki. Watumishi hawa kwa sasa wanafanya mojawapo kati ya haya mawili ili wafanikiwa kukata rufaa yao dhidi ya serikali:
  1. Wanashirikiana na maafisa utumishi kuviondoa vyeti vya kumodoa kwenye mafaili yao na kuviweka vile halisi (kama faili lilikuwa na cheti cha div.3 ya kumodoa, kinaondolewa na kuwekwa halisi chenye div 4)
  2. Watumishi hao sasa wanaiba mafaili yao, wanabadilisha vyeti (vya kumodoa kwa halisi) na kuyarudisha mafaili bila maafisa utumishi kujua.
Mleta uzi anawatahadharisha maafisa utu kuwa makini.
Sijui watu wanatokwa na povu kwa nini?
 
Ovyo kabisa wewe! Konachokuuna sana ni nini.
 
Nimeona niliweke hili wazi . .Huu kchezo wa unaofanywa na maafisa utumishi unalenga kuwachafulia watu wa baraza ili waonekane wamefanya kazi ya kuhakiki vyeti vibaya na hawakuwa makini.
.
Kama Bashite ameachwa kwanini na wao wasiachwe? Unafikiria kuna kiongozi atakubali kuona sheria inabagua?
 
Hata wakifanya hivyo hakuna shida maana NECTA wanavyo vyeti na matokeo ya watu wote na hata hivyo vyeti vilivyo hakikiwa awali ndivyo vitapelekwa tena kwa hiyo wanao fanya hivyo wanajisumbua tuu...NECTA wana matokeo ya kila mtu hao wote wana jisumbua tuu....
 
Tatizo liko kwenye ile orodha ambayo haijawekwa wazi bado. Maana zinatolewa kwa awamu. Ile ya watu elfu 11. Yenye incomplete information, ile imejaa vigogo maana wao hawakuweka baadhi ya vyeti kwenye uhakiki wao ambayo ni feki wakaweka vichache vya vyuoni. Hawakuonyesha vya kidato cha nne au cha sita au vyote viwili. Hayo majina yatolewe nayo wazi
 
Wabongo chochote kinawezekana, computer yenye database itabidi ilindwe maana wanaweza kuichapa.....
 
Imetolewa kwa hisani ya.............?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…