Tetesi: Maafisa Utumishi wanawabadilishia watu wenye vyeti feki data zao

Naanza kuona hao maafisa utumish/tawala wana wakati mgum kwa sababu baadh ya waliofoji vyeti unakuta wana nyadhifa kubwa kwene taasisi.
 
Watulie utaratibu ufatwe wakianza kubadilisha badilisha vyeti malalamiko yao yatatupwa kapuni mwisho wawaponze ht waliotajwa kimakosa ilihali wanavyeti halisi.
Eti cheti kimemodolewa hahahahahaaaa
 
Kama ulisoma shule A na ulipata Div two haibadiliki hiyo data ktk mfumo pale Necta hata ukifariki

Na kama hukusoma shule A na kupata Div two kama cheti chako kinavyoonesha,taarifa hiyo haitakuwepo Necta milele yote.

Hao Maofisa utumishi wanajisumbua tu nothing they are going to get from what they are doing!
 
Mosi inaweza kuwa ni hisia tu au kama ni kweli labda ni mtu asiyejitambua. Kwanza entry qualification huwez kuwa na div4 halafu ukasoma Degree bila route ndefu hapo tu tayari ni mushkil. Na mifumo ya lawson iko tight huwez kuiingilia kiurahisi. Angalizo la mtoa mada limetolewa kama tahadhari. Lakini mtu aliyeajiriwa kama Daktari kwa mfano, aseme alitumia cheti cha Division 2 cha Form Four wakati alipata Div4 kiuhalisia,then assume alienda Form Six kwa Div2 ya kupikwa. Baadae akafaulu Form Six na kisha kwenda Muhimbili. Baadae akaajiriwa kama Daktari tuseme Mwananyamala Hospitali. Wakati wa Ajira atapeleka vyeti:-
1. Cha Form Four-Div2(Fake)
2.Cha Form Six-Div 2(Halali)
3. Cha Degree Muhimbili-Upper Second Class(Halali)!

Miaka kadhaa baada ya uhakiki anaonekana ana cheti Fake cha Form Four. Kwa kutumia Scenario ya Mtoa mada,anaamua kupeleka kile chake Halisi cha Form Four chenye Division 4! Hapa tayari mtiririko wa Elimu unaanza kugoma kabisa na inaonekana kuna udanganyifu wa dhahiri. Division Four huwez kwenda Kidato Cha Sita na Chuo Kikuu kiurahisi hivyo!Anadakwa hapo hapo.
 
Majana makubwa ya binadamu ni kufiwa,kufukuzwa kazi na kuuguliwa,
waache watoe msaada wa kiutu
 
PIA TAIFA HILI LIMEJAA WATU WANAOJUA KUFOJI
 
Kuna jamaa mmoja pia anashughulikia kubadilishiwa data kimya, wameelewana na Afisa Utumishi mmoja ampe kg 3. Nawaza sijui nivuruge deal au niache liende!
 
Kama kinachosemwa ndocho sitashangaa. Mfa maji haachi kutapatapa.
Mtu anakwenda na bomu kiunoni, likilipuka sawa, akipona maisha yanasonga.
Nchi hii aiishiwi vituko.
 
MKUU STORY YAKO INASADIFU TUKIO LILOTOKEA KATIKA HALMASHAURI YA MJI WA MBINGA.
MWALIMU MKUU S/M KIWANJANI WAKATI HUO HUO NI AFISA ELIMU KATA NDG LIOBA NDUNGURU IJUMAA YA 5.5.2017 ALISWEKWA NDANI KWA AMRI YA MKURUGENZI BAADA YA KUANZA KUKANA VYETI ALIVYOVIWASILISHA KWA AJILI YA UHAKIKI AMBAPO YUKO KWENYE ORODHA YA WALIOGUSHI VYETI.
ALIPOPEKULI ALIKUTWA NA VYETI 3 VINAVYOFANANA NA VYA NECTA ILA VIMETOLEWA MWAKA MMOJA.
 
Hawa tulishawajua mapema sana.

Tunawasubiri waendee wakanye debe huko Isupilo.

 

Ulitumwa na nani ufoji vyeti?
 
Tunahitaji watu kama nyinyi, wenye uelewa mpana.
 

yaani nyie munaombishia mtoa mada, nimegundua hamjamuelewa.
 

Wakati huohuo ukumbuke wapo baadhi walibadili matokeo kutoka div 3 kwenda div2 na 1. watu Wa aina hii lazima wao wahahe maana yeye akipeleka kile cha div 3 bado ataonekana alifaulu na alikuwa na vigezo
 
Uhakiki wa vyeti inaaminika ulifanywa kwa umakini mkubwa na kwa muda wa kutosha. Niliposikia kuna watu wako necta nikajua tayari fursa ya kipato kwa wengine na wengine kulizwa kwa kutapeliwa. Kusoma vyuoni kuna vigezo vya ufaulu na ajira serikalini pia zina vigezo vyake. Kurudisha alama za ufaulu utaweza. Utashindwa swali dogo la namna ulivyo enda chuo au kuajiriwa kwa ufaulu huo. Labda uwe kwenye rank ya uteule, huko utapona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…