Mama Samia anahitaji watendaji madhubuti; Hivyo napenda kutumia wasaa huu kumuomba mama, iwapo itampendeza, kwenye mkeka wake wa ma DED, amteue Mariam Ngonyani kuwa DED wa Morogoro manispaa au Mvomero. Bi Mariam Ngonyani ni msomi wa chuo kikuu cha Dar Es Salaam fani ya biashara na sasa anafanya kazi Morogoro Manispaa akiwa na uzoefu wa miaka takrabini kumi kwenye mambo ya ushirika.
Bi Mariam Ngonyani ameolewa na ana watoto watatu. Natumai binti huyu atamuwakilisha vyema mama iwapo atapewa nafasi.
Pia ikimpendeza tena mama, namuomba amteue kwenye wadhifa kama huo bi Adelina Singano kwa wilaya ya Kisarawe. Bi Adelina naye ni msomi wa chuo kikuu cha UDSM fani ya biashara mwenye uzoefu wa takrabini miaka 10 nadhani kwa sasa yuko hapo hapo Kisarawe DC akisimamia mambo ya ushirika. Naamini naye atamuwakilisha mama vyema.