Maajabu: Furaha ya CCM ni kwa Nyalandu kuondoka CHADEMA na si kujiunga na CCM?

Maajabu: Furaha ya CCM ni kwa Nyalandu kuondoka CHADEMA na si kujiunga na CCM?

Mpiga dili karudi kwenye chama cha wapiga dili, halafu kuna misukule wanashangilia tu wao wamesharidhika kuwa wanawashangilia wenzao wakija kupewa vyeo wao wapo tu.
Kama chama kisicho cha wapiga dili kinakubali kuwapokea wapiga dili na kuwapa nafasi za uongozi ni wazi hapo hicho chama kimekosa tu hizo dili ila zingekuwepo hizo dili nacho kingekuwa chama cha wapiga dili pia. Huwezi ukasema unauchukia wizi halafu ukawa unawapa hifadhi wezi na huku ukijua ni wezi.
 
Jamaa karudi Ccm baada ya deal yake kukubalika.
Karudishiwa kitalu chake cha uwindaji kule Lake Natron(Grern Miles) /kama condition ya kurudi Ccm.
Mtakumbuka baada ya kuachishwa uwaziri kitalu hiki kilizushiwa mizengwe hadi kufungiwa. Kilikuwa cha jamaa.
Kumbe hafai kabisa.
Kazi inaendelea.
Amandla....
 
Wacheza kamari wana msemo wao Kamanda, husema HEADS I WIN TAILS YOU LOSE. Hii kaka hata uiweke kivipi (ujifurahishe nafsi yako) ni pigo kubwa. Inaonyesha dhahiri chademathink jinsi ilivyo. Wenzenu CCM wamekupeni kachero nambariwani kawasambaratisha ukawa na kuipoteza zanzibar baada ya kuwajulia mbinu za CUF. Huyu ni bonner, always a bonner. Yaani inaonyesha kwamba wote nyie saizi yenu ni Nyalandu kama aliweza kuwahoodwink.
Unajua lakini maana ya "bonner"?

Amandla...
 
Kwanza tumeambiwa Nyalandu ndie aliyemhifadhi Lissu Ubelgiji kwenye nyumba yake.
Sasa ndie aliyewalipa mshahara wakina Mnyika.
Itafuata hela zote za dhamana alikuwa anatoa yeye.
Halafu, kampeni yote ya Lissu aliifadhili yeye.
Mwisho, pesa ya kuanzisha chama aliitoa yeye.
Kuweni basi hata na aibu kidogo.

Amandla...
Huyo jamaa ni mwezi mchanga halafu asivyojitambua na pombe anakunywa unafikiri kitabaki nini kichwani kama siyo makamasi.
 
Mpiga dili karudi kwenye chama cha wapiga dili, halafu kuna misukule wanashangilia tu wao wamesharidhika kuwa wanawashangilia wenzao wakija kupewa vyeo wao wapo tu.
Hiyo mimba uliyodungwa chato itakutoa roho
 
Kama wenye akili ni aina ya Nyalandu wakimbie tu. Kitendo cha cdm kuendelea kukubalika na wananchi ni jinamizi kubwa sana kwa ccm, mpaka wanaccm wasio na impact yoyote ndani ya cdm wanaporudi ccm eti wanafurahi! Wamerudi akina Lowassa, Sumaye nk Lakini ccm bado imezidi kutegemea vyombo vya dola kutangazwa washindi. Inabidi uwe mwendawazimu kuona Nyalandu kurudi ccm ni pigo kwa Cdm.

Nimesema sentensi zako mbili tu na nikakupa “like”!! CCM bado wana hofu kubwa na Chadema! Wanatamani hata kisingekuwepo (rejea onyo la Msajiri kutaka kufuta vyama ambavyo havijafanya chaguzi), kuzuia hata mikutano ya ndani iliyokuwa ikihidhuriwa na viongozi wa kitaifa, kukalisha Bungeni wanawake 19 ili tu kukomoa uongozi huku Spika akionya wasifanywe chochote!!

CCM ana hofu kubwa na Chadema!! Ni kwa sababu CCM huogopa mawazo yoyote kinzani! Utofauti ndio msingi wa demokrasia. Inatosha kusema demokrasia ina tafsiri tofauti kwa CCM.
 
Chadema inatakiwa kukimbiwa na kila mwenye akili.
Hivyo ukiona watu wanafurahi nyalandu kuondoka jua kuwa wanafurahi chadema kukimbiwa

Mtasubiria sana mithili ya fisi aliyemnyemelea binadamu kwa matumaini kuwa karibu ataangusha angalau mkono mmoja.

Hiiiiii bagosha!
 
Chadema wameumia sana Nyalandu kuwaacha mwisho wa mwezi!

Nakazia:

"Ajabu ni kuwa furaha zimeelekezwa kwenye kuwa bwana huyu asiyekuwa na jina ndani ya Chadema, ametoka Chadema wala si kuwa kajiunga na CCM!"

Hapo ndipo yalipo maajabu ya Mussa.
 
Kwanini mtu uumie hivi hadi uanzishe mada kabisa ya mtu kuhama chama ulicho wewe?!?
Hii ni kutotambua kuwa mtu anaingia kwenye siasa mainly kwa ajili ya nafsi yake either kwa ajili ya kipato, power au umaarufu na sio kwa ajili ya kukuburudisha wewe na nafsi yako. Ukijua hilo utaacha kukimbiza na wanasiasa kuapizana...oh wasalitii...

Mkuu huu uzi hauna maumivu mahali popote bali ni full observations.

Hakuna neno maumivu wala implication to that effect. Bali kuna:

Waliofurahi kuwa kuna mtu katoka kule si kuwa kwa sababu kaja kwetu na pia waliofurahi pakacha limevuja.

Nakazia: bandiko lako ni kwa mada ipi mkuu?
 
Wacheza kamari wana msemo wao Kamanda, husema HEADS I WIN TAILS YOU LOSE. Hii kaka hata uiweke kivipi (ujifurahishe nafsi yako) ni pigo kubwa. Inaonyesha dhahiri chademathink jinsi ilivyo. Wenzenu CCM wamekupeni kachero nambariwani kawasambaratisha ukawa na kuipoteza zanzibar baada ya kuwajulia mbinu za CUF. Huyu ni bonner, always a bonner. Yaani inaonyesha kwamba wote nyie saizi yenu ni Nyalandu kama aliweza kuwahoodwink.

Sina hakika kama umeielewa mada vizuri:

1. CCM kafurahi bwana yule kuondoka Chadema (hiyo ni haki yao).
2. Chadema kafurahi bwana huyu kuondoka kwani ni kuvuja kwa pakacha (hiyo ni haki yao)

Haya mawili asili yake nini?

Huo ndiyo msingi pekee wa mada mkuu.

Iweje pigo kwa awaye yote mkuu kwenye jambo hili la furaha kwa wote?
 
Kama CDM watampokea yeyote toka CCM kwa mbwembwe, basi kitakua sio chama cha siasa bali ni kikundi cha kisanii.

Mkuu naheshimu maoni yako. Ila mada hii haifungamani na upande wowote. Pande zote mbili zina furaha kuu:

1. CCM wanafurahi bwana huyu katoka Chadema si kwa sababu kajiunga CCM.
2. Chadema wanafurahi pakacha limevuja.

Hoja ni kuwa kwa nini CCM wanafurahi Nyalandu kutoka chadema na si kujiunga na CCM?
 
Sugu amechukua mikoba ya Nyalandu!

Uko nje sana ya hoja bwashee.

Pamoja na kuwa naheshimu mno maoni yako. Ila mada hii haifungamani na upande wowote. Pande zote mbili mbona zina furaha kuu:

1. CCM wanafurahi bwana huyu katoka Chadema si kwa sababu kajiunga CCM.
2. Chadema wanafurahi kwa vile pakacha limevuja.

Hoja ni kuwa kwa nini CCM wanafurahi Nyalandu kutoka chadema na wala si kujiunga na CCM?

Ni hilo tu mkuu.
 
Wanasiasa wote wapo after matumbo yao, hulka ambayo kimsingi anayo kila mwanadamu very deep down.

Wote waliohama kutoka CCM kwenda CHADEMA then kurudi CCM wanahangaika hivyo katika kutafuta fursa za kupiga tu

Mkuu sina hakika kama umeona haya kwenye mada ambayo yote mawili ni kweli:

1. CCM wanafurahi sana kwamba, bwana huyu katoka Chadema wala si kwa sababu kajiunga CCM.
2. Chadema nao wanafurahi mno kwamba pakacha limevuja.

Hoja ni kuwa kwa nini CCM wanafurahi Nyalandu kutoka chadema na si kwa kujiunga na CCM?
 
Chadema inatakiwa kukimbiwa na kila mwenye akili.
Hivyo ukiona watu wanafurahi nyalandu kuondoka jua kuwa wanafurahi chadema kukimbiwa
Yes alafu baada ya hapo ndiyo ATCL itaanza ku-genarate faida na Udart itaanza kununua mabasi mapya 15 kila mwaka.
 
Jana Jk alikuwa na Furaha sana baada ya Waziri wake wa Mwisho wa Maliasili na Utalii kurejea Chamani, kashindwa kujizuia hadi wamekumbatiana!


Mkuu nakubaliana na wewe kuhusiana na na JK kafurahi sana. Ila sidhani kuwa JK wala eti kuwa kuna CCM yeyote kafurahi kwa sababu Nyalandu kabudi CCM. Kwani analeta nini CCM?

Ni wazi kuwa furaha ni kwa sababu katoka Chadema.

Mawili hapa chini ni dhahiri:

1. CCM wanafurahi bwana huyu katoka Chadema na si kwa sababu kajiunga CCM.
2. Chadema wanafurahi pakacha limevuja.

Hoja ni kuwa kwa nini CCM wanafurahi Nyalandu kutoka chadema?

Yawezekana kuna lililojificha.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Mbona wakati anahamia huko chadema mlishangilia na mkampa na cheo kabisa Cha mwenyekiti Kanda ya Kati na mjumbe wa kamati kuu? Kwa nini hawajakupa wewe mwenyeji?

Mkuu mbona hoja iko wazi?

1. CCM wanafuraha (jambo la kheri)
2. Chadema wanafuraha (jambo la kheri)

CCM wanafurahi kuwa bwana huyu katoka Chadema si kuwa kajiunga nao.

Chadema wanafurahi pakacha limevuja.

Kulikoni furaha ya CCM?
 
Hoja ni kuwa kwa nini CCM wanafurahi Nyalandu kutoka chadema na si kwa kujiunga na CCM?

In any case, CCM wao wanahesabu ushindi. Aliyeraise mpaka kwenye level ya kugombea teuzi za kusimamishwa kugombea urais sasa katoka CHADEMA na huko CCM hawampi hata ubalozi wa nyumba 10. Sio asset tena.
 
Back
Top Bottom