Maajabu: Furaha ya CCM ni kwa Nyalandu kuondoka CHADEMA na si kujiunga na CCM?

Maajabu: Furaha ya CCM ni kwa Nyalandu kuondoka CHADEMA na si kujiunga na CCM?

In any case, CCM wao wanahesabu ushindi. Aliyeraise mpaka kwenye level ya kugombea teuzi za kusimamishwa kugombea urais sasa katoka CHADEMA na huko CCM hawampi hata ubalozi wa nyumba 10. Sio asset tena.

Huyu bwana hajawahi kuwa asset kwa Chadema. Kugombea nafasi yoyote katika Chadema ni haki ya kila mtu.

Nakazia:

"Ajabu ni kuwa furaha zimeelekezwa kwenye kuwa bwana huyu asiyekuwa na jina ndani ya Chadema, ametoka Chadema wala si kuwa kajiunga na CCM!"

Nadhani furaha za CCM hazina msingi wowote kwani:

Hadi sasa haionekani CCM itanufaika vipi na huyu bwana kama kusivyoonekana popote kuwa Chadema itapata hasara ipi kwa kuondokewa na huyu bwana.

Kwa maana nyingine makelele yote kuhusiana na huyu bwana ni zaidi makelele ya vyura tu!
 
Chadema inatakiwa kukimbiwa na kila mwenye akili.
Hivyo ukiona watu wanafurahi nyalandu kuondoka jua kuwa wanafurahi chadema kukimbiwa
Utakuwaje kwenye Chama miaka 60 maisha ni ya Umasikini Baba zako bado wanaishi kwenye nyumba zilizoezekwa Nyasi na Masufuria
 
Unaejichanganya ni wewe. Mwandishi ana maanisha kuwa CCM hawaoni faida yeyote ya wao kuwa na Nyalandu ila wamefurahi kuwa amewapa sababu ya kuwabeza CDM. Ni kama wakina Lijualikali. Wanafurahia tu wanachodhani ni msiba kwa jirani yao.

Kwa CCM chochote ambacho kitawapunguzia umaarufu CDM ni furaha kwao. Hata kama hawafaidiki moja kwa moja.

Amandla....

kiswahili kigumu
 
Back
Top Bottom