Maajabu ya baadhi ya makanisa: Wapo radhi kumwabudu na kumheshimu Mwamposa lakini siyo Bikira Maria kama vile alifanya kosa kubwa sana kumzaa Yesu

Maajabu ya baadhi ya makanisa: Wapo radhi kumwabudu na kumheshimu Mwamposa lakini siyo Bikira Maria kama vile alifanya kosa kubwa sana kumzaa Yesu

Unajua kabla walokole hawajakushangaa Yesu Kristo anakushangaa?
Soma alichowaambia watu wale waliotaka aache Kuhubiri Mkutano Neno la Mungu akamsikilize mama yake!🤔🤔
(Luka8:19-21)-Wakamwendea mama yake na ndugu zake, wasiweze kumkaribia kwa sababu ya MKUTANO.
20 Akaletewa habari akiambiwa, Mama yako na ndugu zako wamesimama nje wakitaka kuonana nawe.
21 Akawajibu akasema, Mama yangu na ndugu zangu ndio hao walisikiao neno la Mungu na kulifanya.
Sasa kati ya Mchungaji anayefanya kazi ya kuhubiri Neno la Mungu na Mama yake Yesu nani mkubwa?
Harafu fahamu Mariamu hakuwa bikra tena baada ya kumzaa Yesu,Mariam alizaa watoto wengine ndugu zake Yesu,(Mathayo13:53-55)
Mwisho Mariam alishakufa na yeye anangoja Ufufuo,na hakuna anayejua atafufuka ufufuo gani kama ni wa Uzima au wa Hukumu! Hilo anajua Yesu Kristo mwenyewe!
(Yohana5:28-29)
Hawa wajomba ndio waliouchakachua Ukristo.
Kuna mafundisho mengi tu ya kipagani wameyatumbukiza kwenye Ukristo. Lakini hoja yao kubwa husema kanisa lao ndio la kwanza
 
Mimi ni hai, na ninawaombea Kwa Mungu aliye hai Yesu Kristo aliyefufuka.

Wapi pameandikwa tuombe Kwa Jina la Mariam?
Tumechagua bikra maria atuombee kama nyie mlivyochagua mwamposa awaombee. It is the matter of choice
 
Sasa mbona unaenda kanisani si ungekaa nyumbani ukaomba. Au nyumbani kwako mungu hayupo
Neno la Mungu limetuasa tusiache kukusanyika pamoja kwa Ibada.

Waebrania 10
25 wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia.

Pia ni muhimu kuabudu pamoja Ili kufundishana neno la Mungu kwa pamoja Ili tuweze kukua kiroho
 
Sasa kama alizaa na bikira ikaondoka kanisa katoliki linapata ujasiri wapi wa kuendelea kumuita Bikira Maria kama sio utapeli.
Kuna mtu ametoka kusema Wakristu wote wanamuheshimu Bikira Maria, nikamwambia huenda hawajui vizuri walokole. Afadhali mlokole umejitokeza na kuthibitisha kauli yangu
 
Alizaa kwa uwezo wa roho mtakatifu so theoretically bado ni bikra.
Yesu alizaliwa kupitia mdomoni au kwenye masikio ya Maria ili Maria abaki bikira? Na kuendelea kuitwa Bikira Maria?

Mtoto Yesu hakuzaliwa kutoka tumboni kupitia kizazi cha kike cha Maria?

Kwa hiyo Yesu alizal8wa theoretically sio physically? Kuwa Yesu sio mtu halisia bali ni theory? Sio physically being?
 
Neno la Mungu limetuasa tusiache kukusanyika pamoja kwa Ibada.

Waebrania 10
25 wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia.

Pia ni muhimu kuabudu pamoja Ili kufundishana neno la Mungu kwa pamoja Ili tuweze kukua kiroho
Sasa ndo ujue hata mimi naweza kukuombea na kukuelekeza uganyeje ili kumfilia mungu vivyo hivyo kwa mbarikiwa bikra maria. We do the same in a highly formal way
 
Tumechagua bikra maria atuombee kama nyie mlivyochagua mwamposa awaombee. It is the matter of choice
Kumbe mna uwezo wa kuombewa na wafu, Mariam Si amekufa?

Halafu hayo yameandikwa wapi?
 
Mwamposa week hii munamwandama kisa ile nyomi nimeamini binadamu hatupendani kabisa. ile nyomi imewavuruga sana watu huko makanisani wachungaji wanajikuta wanazungumzia tu ule mkesha
 
Imeandikwa kuwa bikra maria ni mama wangu na alipomtembelea elizabeth kitoto kichanga kiliruka ruka ndani ya tumbo lake kimaanisha bikra maria hakuwa w kawaida. Ndo mana elizabeth alisema imekuwaje mama wa bwana wangu anijilie mimi.
Sijakukatalia ni mama wa Bwana wetu lakini kwanini apewe sifa? Sifa zipo reserved for the creator only. Mungu anaruhusu tushee utukufu wake tukiwa ndani yake maana kwa unyenyekevu tunaumrudishia wote yeye. Ukisoma Paulo anaelezea namna Yesu baada ya vyote kuwekwa chini yake na yeye atajiweka chini ya Baba. Utukufu wa Yesu upo ndani ya Mungu, je wa Maria upo kwa wapi? Na kumbuka Yesu ni Mungu. Halafu je unajua pamoja na Mama Maria kupokea uvuvio wa uvuli wa Roho Mtakatifu wakati wote wa mimba ya Yesu lakini alikua kati ya wale 120 walio mpokea Roho Mtakatifu alipowashukia kwenye kile chumba kidogo cha Sala Yerusalemu baada ya kupaa Bwana?Kwa nini apokee ahadi sawasawa na sisi halafu tumpe sifa?
 
Yaani unakuta mtu anamtukana mama yake Yesu alafu anaenda kumuomba Yesu amsaidie. Hivi kweli mtu anaweza akamtukana mama yako alafu ukamsaidia? WAJIRATIBU

USOME INJILI YA:

LUKA 1: 40-56

40 Baada ya siku chache, Mariamu aliharakisha kwenda mji mmoja katika milima ya Yudea. Akaingia nyumbani kwa Zakaria akamsalimu Elizabeti.

41 Naye aliposikia salaamu za Mariamu, mtoto aliyekuwa tumboni mwake aliruka. Elizabeti akajazwa na Roho Mtakatifu,

42 akasema kwa sauti kubwa: “Umebarikiwa wewe zaidi ya wanawake wengine wote, naye mtoto utakayemzaa amebari kiwa.

43 Sikustahili heshima hii ya kutembelewa na mama wa Bwana wangu!

44 Mara tu niliposikia salaamu zako, mtoto aliyeko tum boni mwangu aliruka kwa furaha.

45 Wewe umebarikiwa kwa kuwa uliamini kwamba Bwana atatimiza yale aliyokuambia.”

46 Mariamu akasema: “Namtukuza Bwana,

47 na roho yangu inamfurahia Mungu Mwokozi wangu.

48 Kwa kuwa ameutambua unyonge wa mtumishi wake. Tangu sasa vizazi vyote wataniita niliyebarikiwa.

49 Kwa maana, yeye Mwenye Uwezo, amenitendea mambo ya ajabu! Jina lake ni taka tifu.

50 Rehema zake hudumu vizazi hata vizazi kwao wamchao.

51 Kwa mkono wake ametenda mambo makuu. Wenye kiburi mioyoni mwao amewatawanya.

52 Amewaangusha wafalme kutoka katika viti vyao vya enzi na kuwainua wanyonge.

53 Amewashibisha wenye njaa kwa vitu vizuri na matajiri amewafukuza mikono mitupu.

54 Amemsaidia mtumishi wake Israeli, akiikumbuka rehema yake,

55 kama alivyowaahidi baba zetu Ibrahimu na uzao wake daima.”

56 Mariamu akakaa na Elizabeti karibu miezi mitatu, kisha akarudi nyum bani kwake.
Maria ana heshima kama mama wa mkombozi alimaliza kazi ya kumzaa mwana.
Apaswi kuombwa sababu hana nguvu
 
Sasa ndo ujue hata mimi naweza kukuombea na kukuelekeza uganyeje ili kumfilia mungu vivyo hivyo kwa mbarikiwa bikra maria. We do the same in a highly formal way
Kwanini Maria akuombee na sio Eliya (ambaye hakufa kabisa) au Musa ?
 
Sijakukatalia ni mama wa Bwana wetu lakini kwanini apewe sifa? Sifa zipo reserved for the creator only. Mungu anaruhusu tushee utukufu wake tukiwa ndani yake maana kwa unyenyekevu tunaumrudishia wote yeye. Ukisoma Paulo anaelezea namna Yesu baada ya vyote kuwekwa chini yake na yeye atajiweka chini ya Baba. Utukufu wa Yesu upo ndani ya Mungu, je wa Maria upo kwa wapi? Na kumbuka Yesu ni Mungu. Halafu je unajua pamoja na Mama Maria kupokea uvuvio wa uvuli wa Roho Mtakatifu wakati wote wa mimba ya Yesu lakini alikua kati ya wale 120 walio mpokea Roho Mtakatifu alipowashukia kwenye kile chumba kidogo cha Sala Yerusalemu baada ya kupaa Bwana?Kwa nini apokee ahadi sawasawa na sisi halafu tumpe sifa?
Tunampa sifa za kutuzalia mkombozi. Hakuna namna nyingine ya ku recognize huo ukwelii mtakatifu
 
Ajabu ni pale mtu anaposhangaa watu kwa Kuhukumu wakati yeye anahukumu.... Ingawa tukiongelea contradictions ulichotoa wewe sio contradiction haimaanishi sababu mtoto ni mwema na bora basi mama lazima awe bora na mwema if that was the case na wewe unaamini wote tulitokea kwa Adam na Eva au Hawa (whichever you believe) basi kungekuwa hakuna mtu mbaya unless Adam na Eva walikuwa wabaya...

All I can say when it comes to faith ' To each their Own...) ila usichanganye imani na facts (huwezi kuvipika kwenye chungu kimoja)
 
Mwamposa week hii munamwandama kisa ile nyomi nimeamini binadamu hatupendani kabisa. ile nyomi imewavuruga sana watu huko makanisani wachungaji wanajikuta wanazungumzia tu ule mkesha
Wote wale wapo tuition kwa mwamposa wamefata mazingaombwe lakini ni waumini wa makanisa yao.
Mwamposa hana kanisa hana washirika toka madhehebu mbali mbali wakristo kwa waislamu kwa wasio na dini pia.
 
Yesu alizaliwa kupitia mdomoni au kwenye masikio ya Maria ili Maria abaki bikira? Na kuendelea kuitwa Bikira Maria?

Mtoto Yesu hakuzaliwa kutoka tumboni kupitia kizazi cha kike cha Maria?

Kwa hiyo Yesu alizal8wa theoretically sio physically? Kuwa Yesu sio mtu halisia bali ni theory? Sio physically being?
Haya mambo ni ya rohoni zaidi. Kibidamu huwezi elewa hilo fumbo la imani. Ndo mana sisi tunasema hilo ni fumbo la imani mwisho tunaitimia tumshukuru mungu
 
Hao watakatifu ni wakuu kuliko Kristo au wapo sawa naye ?.

Kwanini usiombe kupitia Kristo?...
Nimeshajinu tauari kwamba hata wewe unaweza kuniombea in case of falling down ili nisirudie
 
Back
Top Bottom