Wasalam...!
Kwanza lazima tukubali tu kuwa kwa sasa tuna Rais mwingine na ni Awamu nyingine kuanza kutafuta kuokoteza maneno maneno na kuyaanzishia thread za kukosoa Utawala wa Awamu ya 6 chini ya mama shupavu SSH ni kukosa hoja na kuonesha kuwa kuna watu walikuwa wanafaidika moja kwa moja.
Lakini kama tunakubali ni utawala mwingine basi lazima pia tukubali kuwa, sasa ni zamu ya Mama kupanga safu ya watu ambao anaona atafanya nao kazi ya kuipeleka nchi mbele Zaidi. Tunashukuru kwa kazi ya Mwendazake lakini tuache mama afanye kazi yake kwa sababu ni zamu yake. Sijaona mama akitoa kauli za kuudhi na kudhalilisha UTU wa wengine kama zile za kuwashwa washwa au Mpambuvu (Rejea maneno ya JPM kwa wastaafu na kauli ya JPM kwa Mkurugenzi wa Nachingwea).
Kikubwa ninachomkubali mama huyu anashaurika na hilo ndio jambo kubwa, Tanzania ni yetu sote na kila mtu anaitakia mema nchi hii isipokuwa wachache tu (Rejea utenguzi wa Mwesigwa mstaafu wa TPDC ambaye hakuona hata vitasa vya ofisi yake mpya). Ingekuwa ndio JPM ametoa book lile angemtetea yule waziri wa Sheria wa UDOSO mpaka MATAGA wangeimba pambio na hata asingemtengua, rejea wateuliwa wake jinsi walivyokuwa wanalalamikiwa na hakuchukua hatua zozote.
Mama anatueleza ya sirini ambayo tulikuwa hatuyajui. mfano wote sisi hatujaona mikataba ya madini lakini tunaanza kusema ya Mwendazake ilikuwa mizuri, uzuri ulikuwa kwenye nini? watu wanashindwa kutoa majibu. Haya suala la utoroshaji wa Madini, unafikiri mama hana watu wa kumuambia kuhusu utoshaji wa madini?
Mwisho, kati ya 2016 mpaka 2020 ziliibuka Ids nyingi sana humu na zote zilikuwa zinamtetea Mwendazake, ila leo walewale wameanza kumshambulia mama SHUPAVU kwa kasi sana tena sana. Sasa sijajua wale watu walikuwa ni wanachama au kikundi cha watu kilichoratibiwa na Mwendazake?
Nawakumbusha tu, Chama ni kile kile na kiongozi anatekeleza Ilani ile ile anachokifanya ni kuamua tu kusema ukweli wa mambo ulivyo, hivyo tuendelee kusifia na kupamba kama kawaida. Wengi wanakuja na hoja za alikuwa mshauri wa RAIS, hivi unaanzaje kumshauri mtu ambaye amesema yeye JIWE na hashauriki kwani kufanya hivyo ni kuharibu na hapangiwi na MTU? Jaribu kutafakari kauli ya “SIPANGIWI NA SISHAURIKI”.
Kama ambavyo mlianza michakato yenu huko Bungeni ya kumlazimisha Rais ATAKE ASITAKE lazima mumuongezee muda, nawaomba musiache endeleeni hivyo hivyo na we POLEPOLE ile kazi ambayo alikupa Mwendazake huko Bungeni ya kuwa-monitor wabunge ili ujue nani anaenda kinyume katika mipango yenu dhalimu endelea hivyo hivyo.
“Mimi naondoka lakini ile miaka ambayo mlipanga kuniongezea mimi, sasa mumpatie huyu mama”.