Maajabu ya baadhi ya Wana-JamiiForums kwa Utawala wa Awamu ya 6

Maajabu ya baadhi ya Wana-JamiiForums kwa Utawala wa Awamu ya 6

Ameanza na mguu mbovu! Ni dhahiri kazungukwa na wajanja wajanja! Anabomoa kila kitu kwa kauli na matendo.

Afahamu tunamsikiliza na wengi wanabaki na mshangao! Kama mwendo ndio huu tutegemee anguko la CCM tukipata wapinzani serious! Hope wapinzani watakuwa huru zaidi sasa [emoji41]
Pole sana Sukuka Gang
 
Swadakta,hakika imebaki stori tu nw hawajui washike wap
Kuna aya ya Qur'an inasema: "wamakru wamakaraAllahu wallahu khairu-lmaakiriin". yaani wao wanapanga yao na Allah anapanga yake, na yeye Allah ndie mbora wa wanaopanga mipango.
Tayari walikuwa wanapanga kumuweka JIWE litawale milele ili atuumizie zaidi lakini na Mungu alipanga yake!
Kwa kweli Allah ni mbora wa mipango!
 
Mama akifanya vibaya, furaha kwa wanasiompenda 😀

Mama akifanya vizuri, kisirani kwa wanaomchukia 😀

Binadamu ndivyo tulivyo, No one is perfect except God...

Mimi namuombea tu, Mungu amuongoze na amfanyie wepesi kwenye majukumu yake.
AMEN
 
Samia ni zao la mfumo.sijui una umri gani na alimu gani na ulisoma wapi ukakulia wapi? CCM ni ileile
Mfumo si mfumo mpaka ukubalike kuwa mfumo na watu husika.
Jiulize mfumo ni nini kiundani kabisa??? Ni watu!! km jibu ni hilo... Na huyu nae ni mtu ana watu nyuma yake.

Kumbuka mfumo una uhai......that means. ...
unazaliwa..
unakua na mwishowe
una kufa.
 
Ameanza na mguu mbovu! Ni dhahiri kazungukwa na wajanja wajanja! Anabomoa kila kitu kwa kauli na matendo.

Afahamu tunamsikiliza na wengi wanabaki na mshangao! Kama mwendo ndio huu tutegemee anguko la CCM tukipata wapinzani serious! Hope wapinzani watakuwa huru zaidi sasa [emoji41]
Ccm ife mara ngapi? Mbona sisi tunachoona ni dola tu, ccm iko wapi? Ilipo ccm kuna dola na ilipo dola ndipo kuna ccm. Where is this moribund party??
 
tumwombe Mungu kwa kweli...kuna minong'ono nasikia sikia. Mama inabidi awe kiongozi mwenye maamuzi na msimano. wanaomsifia wana lao jambo...avunje kwanza vikundi vyote vya zamani va vipya vya wahujumu uchumi na walaghai. Nchi ina wasaliti wengi ambao wanapokea sapoti kwa wakolonio...hatutaki ukoloni mamboleo sisi.
Mmeiga Western politics/ mfumo wa vyama vingi, uchumi mnawategemea, soko la dunia wanalimiliki, games na sports kila siku man utd, arsenal, Liverpool Madrid, etc hamuachi kuzungumzia, misaada kila siku hadi magari ya serikali yameandikwa DFP, ukoloni mamboleo bado unaoperate kwa kiasi kikubwa, Cha kujifunza ni kuwa na utawala bora tena yenye hatua dhabiti kwa nchi, hata kiongozi ambaye sio charismatic lakini visionary leader, kwa Africa bado hawajazaliwa.

Sent from my Infinix X652 using JamiiForums mobile app
 
Rais hana msimamo, leo anateua huyu kesho anatengua, mara atangaze hivi kesho akanushe, hii biashara gani ya kubahatisha ameipeleka ikulu, hapa watu wasilete habari za anashawishiwa na remnants wa awamu iliyopita, kama anakubali kushawishiwa maana yake she is weak, hafai kukaa ikulu kama mtu hana msimamo wake binafsi.

Hii nchi inaenda kugeuzwa shamba la bibi muda sio mrefu, dalili zote zinanionesha hilo, ile ikulu yetu ina vacuum.

Tuombe Mungu First Gentleman asiwe mtu mwenye kupenda kuwa na influence katika utawala wa nchi. Vinginevyo, tujiandae kwa decisions zitazofanyika bedroom!
 
Mmeiga Western politics/ mfumo wa vyama vingi, uchumi mnawategemea, soko la dunia wanalimiliki, games na sports kila siku man utd, arsenal, Liverpool Madrid, etc hamuachi kuzungumzia, misaada kila siku hadi magari ya serikali yameandikwa DFP, ukoloni mamboleo bado unaoperate kwa kiasi kikubwa, Cha kujifunza ni kuwa na utawala bora tena yenye hatua dhabiti kwa nchi, hata kiongozi ambaye sio charismatic lakini visionary leader, kwa Africa bado hawajazaliwa.

Sent from my Infinix X652 using JamiiForums mobile app
Sasa inabidi hiki kizazi chetuu kifanye mabadiliko. N a siyo kitu rahisi kwa sababu mabadiliko mengine huambatana na kafara na mapinduzi ya kweliu yanahitaji kujitoa. ni kwanini tusiwe tunatoa rai kwa viongozi wetu yaani hata iwekwe siku maalum ya mjadala kuhusu jambo fulani . lakini pia naamini kama raisi Magufuli na raisi Samilia walivyokuwa wanawamini wabunge basi hata wabunge wangechapa kazi kwa mwendo ule ule,...waangalie maslahi ya wananchi waliowachagua na kusimami ahaki zao kitaifa,,,,mbona ingekuwa bandika bandua!
 
Wasalam...!

Kwanza lazima tukubali tu kuwa kwa sasa tuna Rais mwingine na ni Awamu nyingine kuanza kutafuta kuokoteza maneno maneno na kuyaanzishia thread za kukosoa Utawala wa Awamu ya 6 chini ya mama shupavu SSH ni kukosa hoja na kuonesha kuwa kuna watu walikuwa wanafaidika moja kwa moja.

Lakini kama tunakubali ni utawala mwingine basi lazima pia tukubali kuwa, sasa ni zamu ya Mama kupanga safu ya watu ambao anaona atafanya nao kazi ya kuipeleka nchi mbele Zaidi. Tunashukuru kwa kazi ya Mwendazake lakini tuache mama afanye kazi yake kwa sababu ni zamu yake. Sijaona mama akitoa kauli za kuudhi na kudhalilisha UTU wa wengine kama zile za kuwashwa washwa au Mpambuvu (Rejea maneno ya JPM kwa wastaafu na kauli ya JPM kwa Mkurugenzi wa Nachingwea).

Kikubwa ninachomkubali mama huyu anashaurika na hilo ndio jambo kubwa, Tanzania ni yetu sote na kila mtu anaitakia mema nchi hii isipokuwa wachache tu (Rejea utenguzi wa Mwesigwa mstaafu wa TPDC ambaye hakuona hata vitasa vya ofisi yake mpya). Ingekuwa ndio JPM ametoa book lile angemtetea yule waziri wa Sheria wa UDOSO mpaka MATAGA wangeimba pambio na hata asingemtengua, rejea wateuliwa wake jinsi walivyokuwa wanalalamikiwa na hakuchukua hatua zozote.

Mama anatueleza ya sirini ambayo tulikuwa hatuyajui. mfano wote sisi hatujaona mikataba ya madini lakini tunaanza kusema ya Mwendazake ilikuwa mizuri, uzuri ulikuwa kwenye nini? watu wanashindwa kutoa majibu. Haya suala la utoroshaji wa Madini, unafikiri mama hana watu wa kumuambia kuhusu utoshaji wa madini?

Mwisho, kati ya 2016 mpaka 2020 ziliibuka Ids nyingi sana humu na zote zilikuwa zinamtetea Mwendazake, ila leo walewale wameanza kumshambulia mama SHUPAVU kwa kasi sana tena sana. Sasa sijajua wale watu walikuwa ni wanachama au kikundi cha watu kilichoratibiwa na Mwendazake?

Nawakumbusha tu, Chama ni kile kile na kiongozi anatekeleza Ilani ile ile anachokifanya ni kuamua tu kusema ukweli wa mambo ulivyo, hivyo tuendelee kusifia na kupamba kama kawaida. Wengi wanakuja na hoja za alikuwa mshauri wa RAIS, hivi unaanzaje kumshauri mtu ambaye amesema yeye JIWE na hashauriki kwani kufanya hivyo ni kuharibu na hapangiwi na MTU? Jaribu kutafakari kauli ya “SIPANGIWI NA SISHAURIKI”.

Kama ambavyo mlianza michakato yenu huko Bungeni ya kumlazimisha Rais ATAKE ASITAKE lazima mumuongezee muda, nawaomba musiache endeleeni hivyo hivyo na we POLEPOLE ile kazi ambayo alikupa Mwendazake huko Bungeni ya kuwa-monitor wabunge ili ujue nani anaenda kinyume katika mipango yenu dhalimu endelea hivyo hivyo.

“Mimi naondoka lakini ile miaka ambayo mlipanga kuniongezea mimi, sasa mumpatie huyu mama”.
Mheshimiwa Samia Suluhu anasema" tukiona bango umekwenda!" Tukisikia umemzuia mtu kuonyesha Bango umekwenda.! Obviously huyu Rais mahiri anataka kumpiku Magufuli katika fukuza fukuza.
Sasa,kweli,unaweza kusema huyu Rais yuko serious?
Pia kasema madini yanaibiwa Mererani wakati CDF yupo pale pale Mererani. Haionekani kama tutapiga miayo katika Awamu hii.
 
Back
Top Bottom