Mabibi na mabwana heshima kwenu na moja kwa moja kwenye mada.
Nimefuatilia kauli takribani zote kuhusiana na uchaguzi mkuu zinazotokea katika chama hii kubwa.
Si katika uzinduzi wa kampeni si katika walioongea katika kampeni au popote kuhusiana na uchaguzi 2020. Hakuna wanaposema neno 'haki' bali wanasisitiza amani tu!
Labda kama mnataka kubadili usemi kuwa: "ukiyastajaabu ya Mussa utayaona ya CCM?"
Kwa nini ni vigumu kwenu kuhubiri haki? Tafadhalini hubirini haki kama wengine na amani itafuata mkondo wake.
Amani ni tunda la haki. Haki kwanza amani hufuata.
Ukweli mchungu, haipo amani bila haki!
Shime sote kwa umoja wetu tuwatake wasiopenda kutamka neno haki, wafanye hivyo. Tunalihitaji neno hilo sasa, wala si ombi tena.
Maendeleo hayana vyama.
Vinginevyo tuwafahamishe wajue wanakotaka kutupeleka tunapajua. Wala siko tunakopataka.
Kwa hakika tusingependa tufikie huko.