Maajabu ya CCM kutaka amani bila haki

Maajabu ya CCM kutaka amani bila haki

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Mabibi na mabwana heshima kwenu na moja kwa moja kwenye mada.

Nimefuatilia kauli takribani zote kuhusiana na uchaguzi mkuu zinazotokea katika chama hii kubwa.

Si katika uzinduzi wa kampeni si katika walioongea katika kampeni au popote kuhusiana na uchaguzi 2020. Hakuna wanaposema neno 'haki' bali wanasisitiza amani tu!

Labda kama mnataka kubadili usemi kuwa: "ukiyastajaabu ya Mussa utayaona ya CCM?"

Kwa nini ni vigumu kwenu kuhubiri haki? Tafadhalini hubirini haki kama wengine na amani itafuata mkondo wake.

Amani ni tunda la haki. Haki kwanza amani hufuata.

Ukweli mchungu, haipo amani bila haki!

Shime sote kwa umoja wetu tuwatake wasiopenda kutamka neno haki, wafanye hivyo. Tunalihitaji neno hilo sasa, wala si ombi tena.

Maendeleo hayana vyama.

Vinginevyo tuwafahamishe wajue wanakotaka kutupeleka tunapajua. Wala siko tunakopataka.

Kwa hakika tusingependa tufikie huko.
 
Ccm na Viongozi wao wa dini uchwara wamejaa unafki usio kifani.

Amani pasipo na haki ni uzwazwa.

Hatuna sababu ya kuangalia makunyanzi.

Tuwaeleze watu hao na vibaraka wao.

Tunataka haki!

Huwezi kushangilia ubunge Bila kupingwa kama kweli kwa dhati ya moyo unataka haki (na hili ni moja tu yapo lukuki).
 
Tutaendelea kuhubiri Aman tu , haki tunawaachia nyie . Mana tunajua kabisa tukihubiri haki na Aman, Sisi hatuna chetu kabisa kama tukihubiri haki .

Asante mkuu kwa kuusema ukweli pasipo na kuyangalia makunyanzi yenu. Kwani angalau unakuwa kibaraka mwerevu.
 
Asante baba Askofu Bagonza ulituambia lile kongamano lilikuwa la Amani.................. Sisi wa haki na amani tusubiri letu

Asante sana ujumbe ulikuwa na mantiki sana
 
Kamanda tupe link tumuone Rais wetu Lissu leo Arusha akitamka haki haki hakii 😁

Hata shetani siku akitamka neno haki itakuwa faraja. Nani ajuaye, labda atakuwa yu njiani kubadilika.

Wanayo thawabu wote wasisitizao haki.
 
Team lockdown naona magazeti umeyahamishia huku. Pole sana kila unapotetea unaangukiA za uso

#coronashwainiyake
 
Amani iwe kwako.

Yesu alisisitiza Amani hata pale walipomnyima haki yake ya kuishi.

Sikiliza dogo.
Unaposema Amani ni tunda la haki, hayo ni maelezo kutoka kwa viongozi fulani wa dini na kijamii wenye uchu wa kuona damu zisizo na hatia zinamwagika nchini. Hao viongozi (hasa wa kidini) ukiwauliza ni mstari gani wa msahafu unasema hayo hawaujui. Ni sawa na kusema kwamba MUNGU KASEMA JISAIDIE NAMI NITAKUSAIDIA.. ambapo hakuna mahali ambapo kuna mstari unaoelezea hayo

Amani ikiwepo kwanza haki huja baadaye. Huwezi kulazimisha haki iwepo mahala palipojaa udhalilishaji, matusi, mabezo na ghiliba za kishetani huku wakilazimisha uvunjwaji wa sheria kwa kigezo cha kudai haki... haiwezekani haiwezekani haiwezekani..

Amani ni tunda la Upendo
 
CCM ni sawa na Meli ya Maharamia inayopeperusha Bendera ya Amani
Mnalala CCM
Mnaamka CCM

Hamuinadi sera wala ilani yenu kutwa kuchwa ni kushambulia chama kinachotumia mpaka energy yake ya mwisho kwa manufaa ya wananchi.....
 
Mnalala CCM
Mnaamka CCM

Hamuinadi sera wala ilani yenu kutwa kuchwa ni kushambulia chama kinachotumia mpaka energy yake ya mwisho kwa manufaa ya wananchi.....
CCM ni Chama cha Maharamia unakumbuka Bashe alipokuwa analia Bungeni kuwa amebakwa kwa Energy ya Red bullna boksi la viagra hiyo nio Energy kwa manufaa ya wananchi
 
Mnalala CCM
Mnaamka CCM

Hamuinadi sera wala ilani yenu kutwa kuchwa ni kushambulia chama kinachotumia mpaka energy yake ya mwisho kwa manufaa ya wananchi.....

Mmeshapagawa? Hizi ndiyo zile za kuku mnazoshikiwa?

Dhuluma tu halafu mnataka watulie. Safari hii mtataga sana. Mayai ya bata!
 
Amani iwe kwako.

Yesu alisisitiza Amani hata pale walipomnyima haki yake ya kuishi.

Sikiliza dogo.
Unaposema Amani ni tunda la haki, hayo ni maelezo kutoka kwa viongozi fulani wa dini na kijamii wenye uchu wa kuona damu zisizo na hatia zinamwagika nchini. Hao viongozi (hasa wa kidini) ukiwauliza ni mstari gani wa msahafu unasema hayo hawaujui. Ni sawa na kusema kwamba MUNGU KASEMA JISAIDIE NAMI NITAKUSAIDIA.. ambapo hakuna mahali ambapo kuna mstari unaoelezea hayo

Amani ikiwepo kwanza haki huja baadaye. Huwezi kulazimisha haki iwepo mahala palipojaa udhalilishaji, matusi, mabezo na ghiliba za kishetani huku wakilazimisha uvunjwaji wa sheria kwa kigezo cha kudai haki... haiwezekani haiwezekani haiwezekani..

Amani ni tunda la Upendo

Wewe ni wale viongozi wa dini uchwara wenye kukariri vifungu vifungu?

Ndiyo nyie mnaotutaka tunapopigwa Kofi moja tugeuze na upande mwingine ili mpige tena?

Safari hii moto wake mtauona. kumbe mlizoea?

Safari hii yale ya jino kwa jino na jicho kwa jicho mtayashuhudia. Kumbe ndiyo lugha pekee mnayonekana kuielewa.

Kama wa kulaumiwa ni anayelipiza jino kwa jino lake au jicho kwa jicho lake, basi na iwe hivyo.

Safari hii utamu wa mkuki kwa nguruwe binadamu atauonja.
 
Hata shetani alipomjaribu Yesu alitumia maandiko
 
Back
Top Bottom