Maajabu ya Corona Tanzania: Badala ya Madaktari Bingwa wa tiba kuliokoa Taifa, ni Bingwa wa Kemia ndiye analiokoa Taifa kwa ushauri wa kikemia

Duh!.. noma sana, mpaka hili janga lipite tutasikia mengi sana kusema kweli.
 
Nimejiuliza maswali haya 10 sijapata majibu... Atakaye nijibu vizuri nampa zawadi ...(maana wabongo ukiahidi zawadi utajibiwa mpaka uombe poo)
1.) Kama ni kupuliza hata China,France nk walipuliza japo hatujajua nidawa gani walipuliza... Je, wale ni wapumbafu?
2.) Kusema kuna mask zinaletwa zawezakuwa na virusi je, haitofanya wanaotusaidia kurudi nyuma? hiyo kazi zakudhibiti ni za polisi alioongea nao?
3.) Duniani sijaona rais anayepambana na mitandao,wote wanajielekeza zaidi kwenye udhibiti,vifaa tiba, kuokoa maisha na mwisho uchumi. Je wote ni wapumbafu?
4.) Badala ya hamisha hamisha wizarani je,sio ingefaa maelekezo na majadiliano Mara kwa mara?
5.) Kuongea toka site yaani dar siyo bora na inaokoa pesa (tunazolia hatuna) kuliko kwenda kuongelea kijijini kwako nakutaka ufatwe na viongozi huko kwenu?
6.) Wafanyakazi wako wanakatwa mikopo ya mabank na bodi ya mikopo elimu ya juu (heslb) kiasi wanaishi kishida nawe hujawasamehe unataka wa nchi za nje na WB wakusamehe wewe,ni logic hiyo?
7.) Watu wangapi wakifa itashtua? Kusema najua wamekufa kumi bila kutoa pole na kusikitika maana yake sio issue?
8.) Kila jambo tunatumia majeshi? Tetemeko majeshi,korosho majeshi,madaraja majeshi,maandamano,mitandao, sasa hata korona? Mbona Kenya Leo rais kakaa na waandishi? Marekani vilevile? Hawa hawana majeshi?
9.) Karantini zinafanyika kila nchi na zinaonesha mafanikio je,kuzipuuza nijambo la busara kisa huko nje pia kunawagonjwa?
10.) Hakuna vikao vya Mara kwa Mara na vya dharura Dodoma ama dar kuhusu korona? Ukiwa kijijini ndipo utaweza kufuatilia janga hili kwa ukaribu? Au ikiwa hujaleta korona wewe na kwenye ilani hukuahidi korona basi hunahaja kuhangaika nayo sana?
Ni maswali tuu, watetezi msipanic
 
Mhubiri 4:13
Heri kijana maskini mwenye hekima Kuliko mfalme mzee mpumbavu. ambaye hajui tena kupokea maonyo.
 
Tumsikilize mkemia jiwe au daktari bingwa sasa?!
 

Attachments

  • IMG-20200422-WA0065.jpg
    41.4 KB · Views: 1
Paskali!! IGP kapewa maagizo leo shauri yako
 

Paskali,
Hii thread yako inafurahisha sana kiukweli! Kwamba bingwa wa Kemia amegeuka kuwa Daktari Bingwa wa Covid-19!!!! Inachekesha sana na kufurahisha sana kama siyo kusikitisha....!!!

Epicentre ya Covid-19 ni WUHAN huko nchini China ambako kuna Maprofesa wa Kemia na Kemikali waliobobea. Je, unataka kuniambia kuwa hao Maprofesa na Madaktari wa Kemia hawakuliona au kulijua hili kuwa kumbe Virusi va Corona ni FUTA ambalo ukijifukiza na MVUKE WA MAJI UNAOTOKANA na Boiling Point ya 100 degree Celcius Kirusi kinayeyuka kama SIAGI YA KULIA BOFULO🤣🤣🤣!!!
Huu ni ugunduzi unaohitaji Nobel Prize!
 
Jiwe anataka tujifukize kwa centigrade 100. Hivi anaijua vizuri? Anataka tuive kama mahindi..?!!
 
Bingwa wa kemia alionekana anakikohozi kikali Sana,kemia hapo haijawa applicable?

Hapa kila Mtz atumie akili yake tu
 
Nayajibu yote kwa mpigo.
WEWE NI MCHOCHEZI.
Haya tuma zawadi yangu fasta.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakumaanisha hivyo jamaa yangu! A!likuwa akiuelezea mvuke, na maana yake kiuhalisia!
Hivyo unawaza ni kiroboti! Maana roboti huwa halina akili yake bali kile kinacholishiwa kwalo tu! Samahani lakini kama nitakuwa nimekukwaza ndg!
Hebu tuweke Sawa ambao hatujaelewa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…