Maajabu ya Corona Tanzania: Badala ya Madaktari Bingwa wa tiba kuliokoa Taifa, ni Bingwa wa Kemia ndiye analiokoa Taifa kwa ushauri wa kikemia

Bingwa wa Kemia ametoa ushauri wa Kikemia kuwa vurusi vimeubwa kwa fat acid hivyo vinayeyushwa au kwa kunawa na maji tiririka, au sanitizers zenye alcohol ambazo zinawayeyusha au mvuke wa nyuzi joto kubwa.
Sema kuna sehemu binafsi sijamwelewa huyu Mtalaamu wetu!! Huku kujifukisha na mvuke mtu unatakiwa kujifukisha wakati gani?!

Ni kwamba kama tunavyotakiwa kunawa mikono kila wakati, ndivyo hivyo hivyo tunatakiwa kujifukisha na mvuke kila wakati ili kuviulia mbali tujivirus vilivyopo usoni, au?!

Au ukishajifukisha na mvuke at 100 degree centigrade, moto wake unaenda kuchoma hadi tuvirus tulikopenya na kuingia mwilini ndani?!

Au hutu tuvirusi huwa tunaishi nje tu ya mwili wa mwanadamu, hususani usoni na wala sio kwamba vinaingia mwilini ndani?!
 
Hujamuelewa!

Hajasema hazifai, ila kasema kama zinatoka nje ziangaliwe zisije kuwa chanzo cha kueneza corona. Na akasema anawapongeza wale wanaojishonea wenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani Mchina anahangaika na kuimaliza Corona halafu apoteze muda tena kuijaza Corona kwenye Mask halafu awauwe haohao wa communist wenzake, hata kwa akili ya darasa la saba hili haliwezekani na tatizo huyu Bwana Mkubwa anapokea tu maneno mazima mazima na kuyatapika, Nchi za Ulaya walizokataa mask za mchina walisema hazina viwango lakini siyo kwamba vina Corona
 
Natamani sana huyo bingwa wa kemia angekuepo humu JF, walau akukumbuke kwenye uteuzi. Ungependa uteuliwe kuwa nani ndugu Mayalla?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani unataka Ummy atolewe pawekwe Msukuma Tena? Hussein amekuwa Waziri wa Ulinzi Mzuri sana ni Mwanajeshi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
I think kuna Intel kuhusu issue ya Corona -@Patrick Mayalla

Hapa nazungumza kikubwa ,kuna siri fulani duniani kuhusu hii issue ya Corona ,nyie watu wa investigation Journalism tusaidieni

Hawa Watawala wa Africa Ni kituko...,!
Mwaka huu mbona tutasikia mengi!
 
Unataka hao madaktari waseme ilhali harusiwi mtu yeyote kuonge kuhusu korona kwenye media na ukifanya hivyo polisi hao hapo wanakudaka .

Ni Nani mwenye uthubutu wa kufungua kinywa chake wakati huo

Aisee duuh!!

M.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani wengi humu ni watoto sana ndiyo maana wanashangaaa issue ya kujifukiza. Wenye umri unaozidi 50 years wamemuelewa JPM.

Ni hili la tiba mbadala, ilitakiwa wizara iruhusu muda mrefu. Tumekuwa dependant mpaka tumekuwa wajinga Wa kutosha.

Hongera Rais
 
Watu wengi wanamuamini sana rais sababu ana vyombo vya kukusanya taarifa na kuchakata. Lakin ktk jambo hili la corona, hatuwez kumuacha rais aamue hatma ya maisha yetu. Wala hatupaswi kuwaachia wanasiasa waamue.

Rais sio malaika, anakosea pia. Niwakumbushe sakata la sukari na korosho. Nia ilikuwa njema lakin mpaka leo uamuzi wake umetuachia maumivu.

Pia rais hana historia ya kuwajali watu wake wakat wa majanga. Tetemeko la Kagera, Vifo vya askari saba wakat wa sakata la Mkiru. Vifo vya wanajeshi DRC, nk. Marais waliopita walijenga maghala ya chakula na kila mwaka walinunua tani za kutosha za nafaka kwa ajili ya akiba. Kaja yeye, kapunguza bajeti na kusema fanyeni kazi, yeye hatagawa chakula cha bure. Asiyefanya kazi na asile.

Conclusion: yuko kwenye ndoa tayari, somo tunalolipata ni kwamba hatukuwa makini wakat wa uchumba(uchaguzi). Tungekuwa makin, hii roho ya kikax tungeistukia.
 
Kwa post hii itakuwa huelewi hata lengo la kujifungia au Lockdown. Lengo sio kumaliza tatizo la COVID-19, bali kupunguza maambukizi wakati ufumbuzi wa kitabibu unashughulikiwa.

Kwani kuna ubaya gani kama utasoma tu post za wenzako ili ujifunze zaidi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…