Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jiwe anataka tujifukize kwa centigrade 100. Hivi anaijua vizuri? Anataka tuive kama mahindi..?!!
Sema kuna sehemu binafsi sijamwelewa huyu Mtalaamu wetu!! Huku kujifukisha na mvuke mtu unatakiwa kujifukisha wakati gani?!Bingwa wa Kemia ametoa ushauri wa Kikemia kuwa vurusi vimeubwa kwa fat acid hivyo vinayeyushwa au kwa kunawa na maji tiririka, au sanitizers zenye alcohol ambazo zinawayeyusha au mvuke wa nyuzi joto kubwa.
Yaani Mchina anahangaika na kuimaliza Corona halafu apoteze muda tena kuijaza Corona kwenye Mask halafu awauwe haohao wa communist wenzake, hata kwa akili ya darasa la saba hili haliwezekani na tatizo huyu Bwana Mkubwa anapokea tu maneno mazima mazima na kuyatapika, Nchi za Ulaya walizokataa mask za mchina walisema hazina viwango lakini siyo kwamba vina CoronaHujamuelewa!
Hajasema hazifai, ila kasema kama zinatoka nje ziangaliwe zisije kuwa chanzo cha kueneza corona. Na akasema anawapongeza wale wanaojishonea wenyewe.
Sent using Jamii Forums mobile app
Natamani sana huyo bingwa wa kemia angekuepo humu JF, walau akukumbuke kwenye uteuzi. Ungependa uteuliwe kuwa nani ndugu Mayalla?Bingwa wa Kemia ametoa ushauri wa Kikemia kuwa vurusi vimeumbwa kwa fatty acid hivyo vinayeyushwa au kwa kunawa kwa sabuni na maji tiririka , au sanitizers zenye alcohol ambazo zinawayeyusha au mvuke wa nyuzi joto kubwa.
Bingwa wa Kemia amewataka Watanzania kutumia tiba mbalimbali za asili na tiba mbadala kupambana na Corona kwa kunywa tangawizi, vitunguu swaumu, au hata kujifukiza, vitu ambavyo Watanzania walipaswa kufundishwa na madaktari Bingwa wa tiba, badala yake sasa ni Bingwa wa Kemia ndio amekuwa mkombozi wa taifa letu katika vita hii dhidi ya Corona.
Ushauri huu wa Bingwa wa Kemia ndio ukombozi wa Taifa letu dhidi ya janga la Corona, kwasababu naamini kuna wengi wameugua Corona na wakajitibia kwa njia za asili na tiba mbadala na wakapona, hivyo kama kila Mtanzania akiona tuu dalili kwa mbali akaanza na huduma ya kwanza ya homeopathy treatment kwa kutumia natural treatments na alternative medicine tunaweza kuliokoa taifa letu zaidi kuliko kuwategemea hawa madaktari Bingwa wetu wa tiba ambao ni mabubu huku mabingwa wa Kemia ndio wakilisaidia taifa!.
Mpaka hapa nilipofikia, bado kuna haja ya mimi kumtaja huyu bingwa wa Kemia?
P
Wanabodi,
Hii vita ya Corona Tanzania inakumbana na twists and turns za ajabu ajabu!, kwa vile huu ni mlipuko wa ugonjwa, ilitegemewa madaktari Bingwa ndio wangekuwa wakombozi wa taifa letu kwenye janga hili, lakini kwa Tanzania ni maajabu matupu, badala ya Madaktari Bingwa wa Tiba! kuwa wakombozi wa taifa letu, Mkombozi wa kweli wa taifa letu kwenye hii vita ya Corona ni Bingwa wa Kemia, ndiye ametoa ushauri bora kabisa wa Kikemia wa namna bora ya kuikabiliana na janga hili la Corona ili kushinda vita hii.
Je, bingwa huyu wa Kemia ni nani na ametoa ushauri gani?
Andamana nami.
1. Background, Professionalism
Tangu kuanza kwa janga hili la Corona, mimi kama Mtanzania Mzalendo nimeshiriki kikamilifu katika vita hii kikamilifu katika maeneo 5
Hivyo kwenye hayo maendeleo 5 nimeshiri kwa kutoa maoni mbalimbali, miongoni mwake ni ule ushauri wangu wa mwanzo kuwa zipo wizara zinaweza kuongozwa na Waziri mwanasiasa yoyote, lakini kuna wizara zinazo deal na technical issues, zinapaswa kuongozwa na ma professionals. Moja ya wizara ya Afya, ilipaswa kuongozwa na daktari bingwa na sio a layman kwenye medical field.
- Kama Mtanzania tuu wa kawaida
- Kama Mwana jf
- Kama mwandishi wa habari mzoefu
- Kama mtangazaji wa TV Nguli
- Kama mtu mwenye exposure.
Tulipoanza tuu ile siku Waziri wa Afya akiwa daktari Bingwa kwa jina la Janet akizungumzia kuvaa face mask, daktari huyo akiwa mbele ya Waziri wa Afya alisema face mask zitavaliwa na madaktari tuu wanaohudumia wagonjwa. Nikapandisha bandiko humu na kusema it's not right kwasababu kama inachukua siku 14 kuibaini Corona kwa aliyeambukizwa, how will one knows hivyo to be on a safe side ni watu wote wavae facemasks kama China. Waziri angekuwa daktari pale pale angejua.
Corona inatufundisha Tanzania tuna tatizo kuchanganya siasa na professionalism. Hongera Prof. Janabi kwa elimu uliyotoa, so far you are the best! - JamiiForums
2. Mazungumzo na Naibu Waziri wa Afya
Kuna siku nimezungumza na Naibu Waziri wa Afya, Dr. Faustine Ndugulile, kama ilivyo kawaida yangu, mimi huwa nina maswali magumu. Miongoni mwa maswali niliyomuuliza Dr. Ndugulile ni swali la kwa vile Corona haina dawa, jee anaweza kueleza hao wagonjwa kwenye vituo vya matibabu wanafanywa nini au wana hudumiwa huduma gani ili Watanzania wenye uwezo waweze kuwahudumia wagonjwa wao ambao hawajazidiwa ili kuzuia hospitali zisielemewe. Dr. Alinigomea!.
Kisha nikamuuliza kwa vile Corona ni mafua, kwanini Wizara ya Afya isihamasishe alternative medicine ya watu kujitibu ili wengine wamalizane nayo juu kwa juu bila kuisumbua serikali na kupelekwa vituo vya huduma?.
Pia swali hili alinigomea na kusisitiza kila mwenye dalili aripotiwe.
Kwa kutumia uzoefu wangu wa exposure, Naibu Waziri wa Afya, Dr. Faustine Ndugulile alikuwa ana majibu yote tena ya kidakitari, lakini kwa vile yeye sio Msemaji rasmi, Msemaji rasmi ni Waziri wake, na Waziri sio daktari, Dr. Ndugulile aliogopa kusema akapishana na Waziri wake, lakini Waziri wa Afya angekuwa ni daktari Bingwa, Dr. Ndugulile angezungumza.
Vita Janga la Corona: Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas, Naibu Waziri wa Afya, Dr. Faustine Ndungulile, kesho watakuwa live JLNH-Star TV - JamiiForums
Star TV: Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas na Naibu Wazuri wa Afya Dr. Faustine Ndungulile, Wanazungumzia Corona - JamiiForums
3. Bingwa wa Kemia Aingilia Kati
Hayo maswali mawili magumu niliyo muuliza Naibu Waziri wa Afya Dr. Faustine Ndugulile ambayo yalitakiwa kujibiwa na madaktari Bingwa wa tiba, leo yamepatiwa majibu badala ya kupatiwa majibu na madaktari Bingwa wa tiba, kitu cha ajabu sana kuhusu mapambano dhidi ya janga la Corona nchini Tanzania, maswali hayo yamepatiwa majibu na Bingwa wa Kemia.
Tanzania tulizoea viongozi wetu wakuu wa kisiasa huwa ni wanasiasa, hivyo ulipo tokea Bingwa wa Kemia alipoutaka urais, kiukweli kuna watu humu tulimshangaa!, tangu lini Bingwa wa Kemia akawa kiongozi wa siasa kuwa mkuu wa nchi?.
Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli - JamiiForums
4. Bingwa wa Kemia Atoa Ushauri wa Kikemia
Lakini kwa mara ya kwanza katika urais wa Tanzania, leo ndio tumeona umuhimu wa kiongozi wa nchi anapokuwa ni Bingwa wa Kemia kuutumia ubingwa wake wa kemia kulisaidia taifa lake kwa ushauri wa Kikemia wa jinsi ya kutumia Kemia kupambana na janga la Corona.
Bingwa wa Kemia ametoa ushauri wa Kikemia kuwa vurusi vimeubwa kwa fat acid hivyo vinayeyushwa au kwa kunawa na maji tiririka, au sanitizers zenye alcohol ambazo zinawayeyusha au mvuke wa nyuzi joto kubwa.
Bingwa wa Kemia amewataka Watanzania kutumia tiba mbalimbali za asili na tiba mbadala kupambana na Corona kwa kunywa tangawizi, vitunguu swaumu, au hata kujifukiza, vitu ambavyo Watanzania walipaswa kufundishwa na madaktari Bingwa wa tiba, badala yake sasa ni Bingwa wa Kemia ndio amekuwa mkombozi wa taifa letu katika vita hii dhidi ya Corona.
Ushauri huu wa Bingwa wa Kemia ndio ukombozi wa Taifa letu dhidi ya janga la Corona, kwasababu naamini kuna wengi wameugua Corona na wakajitibia kwa njia za asili na tiba mbadala na wakapona, hivyo kama kila Mtanzania akiona tuu dalili kwa mbali akaanza na huduma ya kwanza ya homeopathy treatment kwa kutumia natural treatments na alternative medicine tunaweza kuliokoa taifa letu zaidi kuliko kuwategemea hawa madaktari Bingwa wetu wa tiba ambao ni mabubu huku mabingwa wa Kemia ndio wakilisaidia taifa!.
Mpaka hapa nilipofikia, bado kuna haja ya mimi kumtaja huyu bingwa wa Kemia?
Paskali
I think kuna Intel kuhusu issue ya Corona -@Patrick Mayalla
Hapa nazungumza kikubwa ,kuna siri fulani duniani kuhusu hii issue ya Corona ,nyie watu wa investigation Journalism tusaidieni
Hujaelewa
Rudia tena kusoma au kumsikiliza
Kasisitiza kunawa na sabuni au sanitizer, wewe unasema hamna umuhimu,why?
Na alcohol aliyo isema jpm ndo hiyo sanitizer chief,msio jua kemia mnatabu sana😁😁
Natamani sana huyo bingwa wa kemia angekuepo humu JF, walau akukumbuke kwenye uteuzi. Ungependa uteuliwe kuwa nani ndugu Mayalla?
Sent using Jamii Forums mobile app
Picha kwa hisani ya Bingwa wa KemiaView attachment 1427303
Kwa post hii itakuwa huelewi hata lengo la kujifungia au Lockdown. Lengo sio kumaliza tatizo la COVID-19, bali kupunguza maambukizi wakati ufumbuzi wa kitabibu unashughulikiwa.Watakuja wanasiasa harakati kuhoji na kutia hofu WaTz kutafuta kiki ya kisiasa.
Mara nyingi nimesema Rais, Dr Magufuli, anawafundisha wanasiasa duniani maana iliyo sahihi ya siasa akitumia taaluma yake ya sayansi.
Ni ukweli ulio wazi virusi vya CORONA haviwezi kuisha kwa kujifungia ndani ya majumba yetu (lockdown) bali kwa kuviangamiza. Baadhi ya njia sahihi ya kufikia lengo ni hizo alizozitaja Rais, mkemia kitaaluma.
Ili tufanikiwe kumwondoa kirusi katika jamii yetu ni kwa kila mwananchi kufuata ushauri wa kitaalamu na kutumia dawa mbadala ya kuangamiza kirusi, kwa waliombukizwa au la.
KWA PAMOJA VITA HII TUTASHINDA.